Google PlusRSS FeedEmail
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananfunzi wa vyuo vya elimu ya Juu nchini CCM, mkoa wa Dar es salaam Ndugu Asenga Damian Abuubakar, akibebwa juu juu na wapambe wake, baada ya kushinda nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa akiwakilisha wilaya ya Ifakara. Kijana huyo ambaye ni kada mkubwa wa Chama anawakilisha kundi kubwa la vijana wenye ari, uwezo na nia ya dhati ya kukisimamia Chama Cha Mapinduzi na kukiongezea nguvu na fikra mpya za Vijana ili kukijenga zaidi na kukiongezea ustawi.

ASENGA ASHINDA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA MKOA UVCCM MOROGORO..

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananfunzi wa vyuo vya elimu ya Juu nchini CCM, mkoa wa Dar es salaam Ndugu Asenga Damian Abuubakar, akibebwa juu j... [Read More]

Makamu wa Rais Dkt Bilala ahutubia Mkutano mkuu wa 16 wa wakuu wa nchi na serikali zisizofungamana na upande wowote Iran

Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilali akihutubia Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Siasa ya Upande ... [Read More]

Aggrey Marealle agombea Ujumbe wa NEC ya CCM.

Mjumbe   wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi, ( CCM ), na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Moshi mjini, Aggrey Marealle (kushoto) a... [Read More]

Dkt. Mohammed Gharib Bilal Audhuria mkutano Iran.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano mkuu wa 16 wa kim... [Read More]

DC WA ZAMANI HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA

[Read More]

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (Kulia)  akisalimiana na akina mama wa Kijiji cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo wakati wa  ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mwaseni, Athuman Mbange (CUF) na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtanza.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (wa pili kukushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Kata ya Mwaseni, akikagua maendeleo ya ujenzi wa chumba cha darasa wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Bibi Fatuma Mazengo akiangua kilio mbele ya waziri alipokuwa akieleza jinsi mkwe wake na mjuu wake walivyouawa kinyama na Askari wa Wanyapori katika Hifadhi ya Mbuga ya Selou mpakani mwa kiji cha Mloka, Rufiji. Watu hao waliuawa walipokwenda kuvua samaki katika ziwa la Mzizizmia kwa ajili ya kitoweo
Akina mama wa Kijiji cha Mibuyu Saba  wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri

Mkazi wa Kijiji cha Mtanza, Yusufu Nyamgumi, akihoji kwenye mkutano kitendo cha Diwani wao, Athuman Mbange (CUF) kutokuwa na tabia ya kuwatembelea kujua matatizo yao, (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DK. RASHID WILAYANI RUFIJI

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (Kulia)  akisalimiana na akina ma... [Read More]

Jumla ya vijana 47 waliokuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika kata ya Tandala wilayani Makete wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katani hapo
Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Makete mkoani Njombe Edwin Mushi anaripoti kuwa ,wakizungumza katika mkutano huo vijana hao wamesema wameamua kwa mapenzi yao kukihama chama hicho kutokana na kutoelewa sera zake na kujiona wakizidi kurudi nyuma kimaendeleo kutokana na ahadi walizoahidiwa wakati wanajiunga na CHADEMA kutotekelezeka
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Nahom Dovisiana Sanga amesema alijiunga na Chadema mwaka 2011 lakini ahadi alizoahidiwa ikiwa ni pamoja na kusaidiwa kiuchumi haijatekelezwa na ndio maana ameamua kutoka kwenye chama hicho
Naye Imani Nyamike ambaye ni mkazi wa kata hiyo naye amesema kwa upande wake amejiona kama amepotea kutokana na kukosa ushirikiano kwa viongozi wa chama hicho hivyo kujiona mpweke tangu alipojiunga na chama hicho
“Mimi napenda kuwaasa vijana wenzangu ambao mmmedanganyika na CHADEMA ndugu zangu huu ni muda wa kurudi CCM, bibi na babu yangu wapo CCM, baba na mama yangu wapo CCM na mimi nimerudi CCM na nitakufa ndani ya CCM” alisema Nyamike
Akizungumza mkutanoni hapo Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amesema chama chake kimefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na vijana hao ya kujiunga na CCM na kusema wao kama chama cha mapinduzi wako tayari kuwasaidia vijana hao na kuwataka kujiunga na kuwa kikundi kimoja ili waweze kupatiwa mikopo ya riba nafuu ili wakuze mitaji ya bishara zao
Amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya vijana kujiunga na vyama vyenye sera za uongo pasipo kujua madhara yanayokuja kuwapata mbele na huku akisistiza wananchi waliofika kenye mkutano huo kubakia chama cha mapinduzi ambacho kimepewa dhamana na wananchi kutekeleza sera zake ndani ya wilaya hiyo
“Ndugu zangu naomba niseme CHADEMA hawana adabu, hivi hakuna ambayo jema lililofanywa na CCM hata mkapongeza? Ninyi kila siku ni matusi tu majukwaani, hata kitendo cha wao kuishi kwa uhuru hadi sasa ni jitihada za serikali ya CCM, bado nalo si jema kwenu?” alisema Mtaturu
Mtaturu alitoa bendera za CCM kwa vijana hao na kusema kuwa kwa kuwa tukio hilo la kuhamia CCM limetokea ghafla, atajipanga ndani ya chama chake kufanya sherehe ya kuwakabidhi rasmi kadi za CCM na kuongeza kuwa zoezi hilo litafanywa na uongozi wa mkoa ama taifa
Katika hatua nyingine Mtaturu aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa wanaoendelea na zoezi la kuhesabu watu katani humo kwani zoezi hilo bado linaendelea kwa siku saba mfululizo pamoja na wananchi hao kujiandaa kutoa maoni ya katiba mpya pindi tume ya kukusanya maoni itakapofika katani hapo
Naye diwani wa kata ya Tandala Mh. Egnatio Mtawa amewashukuru wananchi wa kata yake kwa ushirikiano wanaompa pamoja na kumuomba katibu wa CCm kusaidia kushughulikia suala la umeme wa gridi ya taifa kufika katani Tandala
Amesema huo ni mpango wa siku nyingi wa serikali kuhakikisha umeme unawaka Tandala hivyo anaombwa kusaidia kuimkumbusha serikali ili mpango huo ukamilike mapema

CHADEMA WAPATA PIGO MAKETE

Jumla ya vijana 47 waliokuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika kata ya Tandala wilayani Makete wamekihama cha... [Read More]

* Yagoma kuomba raidhi, yasema tuhuma itazithibitisha mahakamani
* Yamtaka Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja

* Ni kwa kudai CCM inaingiza siala nchini.
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje  ya nchi tena bila kulipia ushuru.

Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kweneye mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam.

"Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti nimesema Chama hicho kinapata  mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala wasisubiri hizo siku saba", alisema Nape.

Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani badala ya kuomba radhi.

"Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama chao kinafutwa", alisema.

Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk. Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda mahakamani.

"Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3 na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini tena", alisema Nape.

CCM YAIKOMALIZA CHADEMA

* Yagoma kuomba raidhi, yasema tuhuma itazithibitisha mahakamani * Yamtaka Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja * Ni kwa kudai CCM in... [Read More]


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na familia yao, wakati Rais Kikwete akihojiwa na  kujibu maswali kutoka kwa karani wa sensa ya watu na makazi, Clement Ngalaba,  Rais alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililoanza kufanyika leo Agosti 26, 2012, nchi nzima. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE NA FAMILIA YAKE WAHESABIWA KATIKA SENSA YA WATU NA MAKAZI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na familia yao, wakati Rais Kikwete akihojiwa na  kujibu maswali kutoka kwa k... [Read More]

CHADEMA kimekuwa kikikosa watu kutokana na kudaiwa kutokuwa na jipya la kuwaambia wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ya mara kwa mara yenye lengo la kujaribu kukijenga chama hicho mkoani Morogoro.Pichani, ni hali ya mahudhurio ya wananchi kwenye mkutano wa Chadema uliofanyika jana jioni eneo la Kingorwila mkoani humo. (Na Mpigapicha Wetu).

CHADEMA YAKOSA MVUTO MOROGORO

CHADEMA kimekuwa kikikosa watu kutokana na kudaiwa kutokuwa na jipya la kuwaambia wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ya mara kwa mara ... [Read More]

 Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 Diwani Omary Kariati akizungumza na wananchi wa Kata yake wakatiwakati wa harambee ya kuchangisha fedha za kufufua mradi wa maji katika kata hiyo. Sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana. Pia gunia 37 za alizeti zenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe zilichangwa kwa ajili hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.  akihamasisha uchangiaji wa mradi wa maji katika kata hiyo,
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo.
 Wakazi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutokana na miundombinu iliyozinduliwa mwaka 1973, na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,  wakati wa uhai wake,  kufa kwa kukosa uangalizi. Pichani Diwani wa
Kata hiyo, Omary Kariati (wapili kulia) na Msaidizi wake  Bakari Ndee wakionyesha tangi la maji lililozinduliwa na Baba wa Taifa ambalo sasa halifanyi kazi
 Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro uliochimbwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo
ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200 wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na sasa diwani huyo anaunganisha nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa ina watu 11,800.

 Wananchi wa Kwadelo wakiwa kwenye mkutano wa harambee ya kuchangishana fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji uliokufa miaka 20 sasa, bada ya kuzinduliwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake mwaka 1973
 Kariati akiwakaribisha nyumbani kwao waandishi wa habari aliofika nao Kwadelo kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya kata hiyo.
 Msichana wa Kwadelo mkoani Dodoma akitumia baiskeli kusaka maji
 Trekta la Kilimo Kwanza nyumbani kwa Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Alhaji Omary Kariati
Wazee wa Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono kumuaga Diwani wa Kata hiyo, Omary Kariati, alipokuwa anaondoka baada ya kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji

DIWANI KATA YA KWADELO AHAMASISHA MAENDELEO KIAINA

 Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma,... [Read More]

RAIS KIKWETE AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiendesha kikao cha Kamati Kuu cha CCM, kilichofanyika leo mchana ji... [Read More]

MPANGO WA KASI YA UWEZESHAJI WA WANAWAKE WAZINDULIWA LEO

Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali (kulia) Mama Zakhi... [Read More]

Bwana Abdallah Bulembo akikabidhiwa fomu ya kugombea Nafasi hiyo ya Mwenyekiti katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, yaliyopo Kariakoo, Dar es salaam.



KATIBU mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Suleiman Dadi (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo Majura ambaye pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini.

Na: Dina Ismail
Bulembo ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA) na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alichukua fomu hizo na kuzirejesha jana hiyohiyo.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hizo, Bulembo alisema kwamba amelazimika kuwania nafasi hiyo ili kuifanyia makubwa jumuiya hiyo kwani ni mwanachama halali wa CCM na mwenye sifa hivyo anawajibu wa kuwania nafasi yoyote inayomfaa kwa lengo la kuendeleza mikakati iliyopo ndani ya jumuiya hiyo.

Hata hivyo, Bulembo ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea nafasi hiyo na kushika nafasi ya pili nyuma ya Balozi Athuman Juma Mhina ambaye sasa ni marehemu, alisema ataweka wazi mikakati yake pindi atakapopitishwa na halmashauri kuu ya CCM.

Bulembo anakuwa mgombea wa saba kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo awali wanachama waliojitosa ni pamoja na John Edward Machemba, Said Ramadhan Bwanamdogo, Salim Hamis Chikago, Jasson Samson Rweikiza, Alfred Joseph Mwambeleko na Alphonce John Siwale.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Hamis Suleiman Dadi,alisema zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu wa nafasi mbalimbali katika jumuiya hiyo lililoanza Agosti 22 litafikia tamati Agosti 29 mwaka huu.

Alisema mbali na nafasi ya uenyekiti, tayari baadhi wa wanachama wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongoizi katika jumuiya hiyo kwa upande wa Bara na Visiwani.

Alizitaja nafasi nyingine ni pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Bara na Zanzibar, Wajumbe wa Kamati Kuu Wazazi kwa upande wa Bana na Visiwani, Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Vijana (CCM)

ABDALLAH BULEMBO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA CCM.

Bwana Abdallah Bulembo akikabidhiwa fomu ya kugombea Nafasi hiyo ya Mwenyekiti katika Ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, yaliyopo Kariako... [Read More]

CCM YAMTEUA NDG HUSSEIN I. MAKUNGU KUGOMBEA BUBUBU.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UTEUZI WA MGOMBEA BUBUBU Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyofanya kikao chake leo tarehe 24/8/2012 im... [Read More]

DR MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BANDARI.

waziri wa uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe.      Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsi... [Read More]

HARAKATI ZA UCHAGUZI WA CCM WILAYA NA MKOA WA LINDI WAANZA.

Mgombea Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini,Muhsin Rafii Ismail akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Wanachama wa CCM Wilaya hiyo kumcha... [Read More]

UMOJA WA VIJANA (UVCCM) WILAYA YA LINDI MJINI WAFANYA UCHAGUZI.

Mkuu wa wilaya ya Lindi Mjini Mheshimiwa Dr Nassor Hamid akihutubia hadhira ya wajumbe ambao wapiga kura katika uchaguzi huo wa Wilaya yake ... [Read More]

NA BASHIR NKOROMO, DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Peter Dalally Kafumu.

Taarifa iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali,  kitakata rufani.

"Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo". imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Nape.

Jana Jaji  Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa Dk. Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.

Dk. Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga, katika uchaguzi mdogo uliofanyika, Septemba mwaka jana, baada ya kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.

CCM KUKATA RUFANI KUTENGULIWA USHINDI WA MBUNGE WA IGUNGA

NA BASHIR NKOROMO, DAR ES SALAAM, TANZANIA Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya... [Read More]

ARUSHA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha kimesema, kimefanikiwa kukamilisha uchaguzi wake wa Chama na Jumuiya katika ngazi za mashina,matawi na kata kwa asilimia 90 kwa mkoa mzima.

Katibu wa siasa na uenezi wa mkoa huo, Loota Sanare alisema hayo leo alipokua akizungumza na vyombo vya habari ili kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi huo ambao umeonyesha kuungwa mkono na vijana walio wengi.

Alisema asilimia 10 za matawi,mashina na kata ambazo hazijafanya uchaguzi wake zimetokana na malalamiko mbalimbali ya wanachama waliogombea kwa madai tofauti yakiwemo ya kuchezewa rafu kwa majina yao kukatwa.

Alisema hata hivyo chama kimeshaagiza nafasi hizo kujazwa mara moja kwa kufanyiwa marekebisho ya makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika uchaguzi huo ili kuwezesha kupatikana kwa viongozi halali kupitia chaguzi hizo.

Sanare alisema katika chaguzi za ngazi za wilaya na mikoa nafasi zinazowaniwa ni uenyekiti,wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya,mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa,mwenezi na mchumi wa wilaya,wajumbe wa mkutano mkuu taifa na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.

Alisema zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi hizo limeanza leo Agosti 22 na litakamilika Agosti 29 ambapo aliwataka wanachama wote wa CCM wenye sifa za kuwania nafasi hizo kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo.

Aidha Sanare alizungumzia kinyang’anyiro cha chaguzi ndogo mbili za udiwani katika kata ya Daraja mbili jijini Arusha na Bang’ata wilayani Arumeru ambapo tayari zoezi la kupatikana kwa wagombea ndani ya chama limeshaanza.

Akizungumzia kata ya Daraja mbili Sanare alisema mgombea ameshapatikana Philipo Mushi kupitia vikao mbalimbali vya chama ambapo wagombea walijitokeza watatu kuchukua fomu lakini ni mmoja tu ndiye aliyerejesha hali ambayo inampa nafasi ya moja kwa moja kuwa mgombea kwakua wenzake wote wanamuunga mkono.

Kuhusu kata ya Bang’ata alisema mchakato uko ndani ya vikao kwaajili ya kujadiliwa kwa majina matatu yaliyopo ili kupatikana jina moja kupitia kamati ya siasa ya wilaya inayokutana kesho ili kupitisha jina hilo.

Alitaja majina matatu yanayojadiliwa kuwa ni Ezekiel Mollel,David Mollel na Olais Mfele ambapo mgombea atajulikana kupitia kikao hicho cha kamati ya siasa ya wilaya inayokutana kesho.

CCM ARUSHA WAKAMILISHA UCHAGUZI KWA ASILIMIA 90

ARUSHA, TANZANIA Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha kimesema, kimefanikiwa kukamilisha uchaguzi wake wa Chama na Jumuiya katika ngazi z... [Read More]

Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape akizungumza leo
DAR ES SALAAM, TANZANIA
KATIBU  wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nauye amemshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, kufuatia kauli aliyoitoa mkoani Morogoro kwamba Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiingiza silaha nchini.

"Kauli hii inaonyesha ni vipi Dk. Slaa ameanza kuzeeka vibaya, na sasa kazi ya siasa inamshinda hivyo awaachie vijana" alisema Nape na kuongeza kwamba anatambua kuwa uzee siyo laana kama unamwingia mtu vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Nape amesema, mbali na kuzeeka vibaya, hatua ya Dk. Slaa kuizushia CCM kwamba imekuwa ikiingiza siala kinyemela ni dalili kwamba ameona kuwa sasa operesheni ya mikutano ya Chadema hasa ya Morogoro zinazorota.

Kwa mujibu wa Nape, Dk. Slaa amesikika akitangaza mjini Morogoro kwamba, CCM imekuwa ikiingiza siala nchini na kuwapa vijana wazitumie wawapo kwenye makambi ya Umoja wa Vijana wa CCM.

"Kwanza huyu Mzee inaonyesha ni jinsi gani ufuatiliaji wake wa mambo ni vinyu, kutoa madai kwamba tumeagiza siala kinyemela kwa ajili ya makambi ya vijana wetu, wakati inafahamika kwamba wakati huu CCM imo katika uchaguzi mkuu hatuwezi kabisa kuandaa wala kufanya makambi ya vijana", alisema Nape.

"Kutokana na kauli hizi za uzushi, tunazitaka mamlaka zinazosimamia ulinzi na usalama kumtaka Dk. Slaa awapatie ushahidi wa kina kuhusu mtu au tasisi yoyote ambayo inaingiza silaha nchini kinyemela, na kama ushahidi wake utawezesha kupatikana yeyote basi ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria", alisema.

"Huyu Mzee imekuwa kawaida yake kuandaa uongo kila anapoona kwamba anakabia kushindwa katika operesheni au mipango yake au ya Chama chake kisiasa. Wakati ule wa Uchaguzi mkuu, alipoona kwamba atashindwa, alizusha kwamba CCM imeingiza kura nchini kutoka nje ya Nchi, lakini ikabainika kuwa ni uzushi", alisema.

Alisema, hatua ya Dk. Slaa kuzusha uongo ni njama ya kuandaa fujo zitakazofanywa watu walioandaliwa na Chadema, kufanya fujo mitaani wakati wa mikutano wa chama hicho mkoani Morogoro. " sasa anatoa uongo huu, ili watu wao waliokusanya watakapofanya fujo azushe kwamba ni vijana waliotumwa na  CCM".

CCM YAMSHUKIA DK. SLAA, YAKANUSHA KUINGIZA SILAHA NCHINI

Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape akizungumza leo DAR ES SALAAM, TANZANIA KATIBU  wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape N... [Read More]

MBARONI KWA KUHAMASISHA WANANCHI WASUSIE ZOEZI LA SENSA TANGA

 TANGA, TANZANIA Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korog... [Read More]

MWILI WA MPIGANAJI ALFRED MBOGORA WASAFIRISHWA LEO

Mamia ya Wanahabari leo walikusanyika  nyumbani kwa marehemu Alfred Mbogora ,kuaga mwili wa mwandishi mwenzao amabye anaaminika ni moja ya w... [Read More]

EID MUBARAK

[Read More]

MWANZA, TANZANIA
Baada ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA wilayani Ilemela, kuupiga ‘stop’ uongozi wake wa wilaya, sasa unatishia kuwang’oa madiwani wake saba, wanaodaiwa kushindwa kulinda kiti cha Meya wa jiji la Mwanza.

Madiwani hao wanadaiwa kukisariti chama hicho kwa kuongoza harakati za kumng’o aliyekuwa Meya wa jiji hilo , Jacton Manyerere, mwezi uliopita baada ya kuungana na madiwani wa vyama vingine kumpigia kura za kutokuwa na imani naye.

Habari zilizopatikana hapa kutoka ndani ya Chadema zimetonya  kuwa, Mkutano Mkuu wa wilaya ya Ilemela, uliofanyika Agosti 12 mwaka huu katika hoteli ya PK wilayani humo, ‘uliwaka moto’ baada ya kuibua hoja ya kutokuwa na imani na viongozi wa mkoa pia madiwani hao.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajumbe na viongozi wapya wa wilaya hiyo watatoana macho na uongozi wa mkoa ambao unadaiwa kutafuna fedha za ruzuku zilizotolewa mkoani Mwanza.

Imedaiwa kwamba, moja ya mambo yaliyohojiwa katika mkutano huo na kusababisha uwake ‘moto’ ni pamoja na ruzuku hiyo, ambayo Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, Wilson Mushumbusi ameshindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi yake katika vikao husika.

“Hadi kieleweke vinginevyo tutatona macho kama mapato na matumizi ya ruzuku hayataeleweka.” Kilisema chanzo kimoja kutoka ndani ya uongozi wa wilaya hiyo na kudai kuwa wajumbe wengi wa kikao hicho wanataka Madiwani hao wakiwemo wawili wa Viti Maalum, walioshindwa kulinda kiti cha Meya wa jiji hilo , wang'olewe.

“Waliungana na madiwani wa CCM na CUF kumpigia kura za kutokuwa na imani naye mheshimiwa Manyerere aliyekuwa Meya wetu, ni wasaliti hawafai, wamekiangusha chama, wanapaswa kuwajibishwa kama ulivyong’olewa uongozi wa wilaya hii.” Kilifafanua chanzo hicho.

Madiwani hao walitajwa kuwa ni Abukari Kapera(Nyamanoro), Hamis Kijuu (Mbugani), Adamu Chagulani (Igoma), Henry Matata (Kitangiri), Marietta Chenyenge (Ilemela), Lucy Kazungu na Upendo Robert, wote viti maalum.

Hoja nyingine iliyoibuliwa katika Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wapatao 94 na kuzua taflani iliyosababisha kutimuliwa uongozi wa wilaya hiyo ni pamoja na kutaka kujua kwanini Wabunge wake wana mamlaka makubwa kuliko viongozi wa Chadema wa wilaya na mkoa. KWA HABARI ZAIDI SOMA MZALENDO KESHO

CHADEMA MWANZA SASA WATISHANA KUNG'OANA

MWANZA, TANZANIA Baada ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA wilayani Ilemela, kuupiga ‘stop’ uongozi wake wa wilaya, sasa unatishia kuwang’oa madiwani... [Read More]

d
1.   MWENYEKITI  TAIFA
1
Asila Ali SALIM
2
Jamal K. ALI
3
Lulu Mcham ABDALLAH
4
Lusekelo W. MALEMA
5
Mbarouk M. MBAROUK
6
Mwana Amina Haji FARUK
7
Nadra Juma MOHAMED
8
Rashid Simai  MSARAKA
9
Sadifa  Juma KHAMIS
10
Thabit Jecha KOMBO

2.   MAKAMU MWENYEKITI WA TAIFA
1
Abubakari Damiani ASENGA
2
Adolph Florian MILUNGA
3
Ally Salum HAPI
4
Antony MAVUNDE
5
Augustino Oscar MATEFU
6
Daniel Moses ZENDA
7
Daud Paulo MSUNGU
8
Donatus T. RUTAGIMBWA
9
Faidha Suleiman SALIM
10
Felician MTAHENGERWA
11
Godwin E. KUNAMBI
12
Goodhance R. MSANGI
13
Idd Yasini MAJUTO
14
Innocent MELECK
15
Jackson KANGOYE
16
John Maurice DEYA
17
Joseph Kulwa MALONGO
18
Langton ZACHARIA
19
Masoud Hamis MASOUD
20
Mboni MHITA
21
Odilia Abraham BATHLOMEO
22
Paul Christian MAKONDA
23
Peter H. LUENA
24
Salum Halfan MTELELA
25
Sango I. Gungu KASERA
25
Silanda MGOMBELO
26
Theresia Adrian MTEWELE
27
Zangina S. ZANGINA

3.   HALMASHAURI KUUYA  CCM TAIFA – NAFASI SITA - BARA
1
Abubakari Damiani ASENGA
2
Adolph Florian MILUNGA
3
 Ahmed Mustafa NYANG’ANYI
4
 Ally Mussa SAMIZI
5
Ally Salum HAPI
6
Amani Wilfred NDUHIJE
7
Angella Onesmo MWANRI
8
 Augustino P. NDIMBO
9
 Augustine S. SIMWIYA
10
 Bertha Yona MINGA
11
Busoro Mohamed PAZI
12
Daud Babu MRINDOKO
13
Daud Paulo MSUNGU
14
Edna Erasto KWILASA
15
Emma Julius MEDDA
16
Emmanuel John SHILANTU
17
Faidha Suleiman SALIM
18
Faidha Suleiman SALIM
19
Fatma Jumbe MWALIM
20
Gilead John TERI
21
Godwin E. KUNAMBI
22
Halima BULEMBO
23
Hadija Mtambi SAID
24
Hassan H. CHAMSHAMA
25
Idrisa Washngton MCHOME
26
Jonas Estomih NKYA
27
Joyce Judith MARTINE
28
Kaeni Edwin NJUNWA
29
Kelvin MBOGO
30
Kheri L. WILLIAM
31
Luhende Richard LUHENDE
32
Lulu Abbas MTEMVU
33
Lusekelo Williard MALEMA
34
Modesta KAMONA
35
Mohamed A. KAPUFI
36
Mohamed Omary MASENGA
37
Mboni Mohamed MHITA
38
Neema K. NYANGALILO
39
Olivia Herry SANARE
41
Peter Isaya KASERA
42
Rahim Juma NG’WANANG’WAKA
43
Rashid GEWA
44
Richard Raymond MBILINYI
45
Salim Rajab KISEBENGO
46
Sango  Issaya G. KASERA
47
Saul Thom MWAISENYA
48
Suleiman H. J. SERERA
49
Stephen J. NYAGONDE
50
Theresia Adrian MTEWELE
51
Vaileth Elias SAMBILWA
52
Zuberi Said BUNDALA
53
Lumola Stephen KAHUNDI




















































4.   BARAZA KUU VITI VITANO - BARA
1
Abubakari Damiani ASENGA
5
 Ally Mussa SAMIZI
6
Ally Salum HAPI
7
Amani Wilfred NDUHIJE
8
 Augustine S. SIMWIYA
 8
Baraka NKATURA
9
 Bertha Yona MINGA
10
Dotnatus T. RUTAGIMBWA
11
Benson Peter MOLLEL
12
Kaeni Edwin NJUNWA
13
Mohamed A. KAPUFI
14
Fatma Jumbe MWALIM
15
Felician MTAHENGERWA
16
Halima BULEMBO
17
Adinani Selemani LIVAMBA
18
David MWAKIPOSA
19
Ester Charles MAMBALI
20
Emmanuel John SHILANTU
21
Kelvin MBOGO
22
Kheri L. WILLIAM
23
Luhende Richard LUHENDE
24
Mboni MHITA
25
Mwita I. NYAGONDE
26
Nassor Ally CHUMA
27
Salum Rajab KISEBENGO
28
Olivia Herry SANARE
29
Mohamed Omary MASENYA
30
Masoud Hamis MASOUD
29
Sango  Issaya G. KASERA
30
Neema Kumba NYANGALILO
31
Saul Thom MWAISENYA
32
Lusekelo Williard MALEMA
33
Peter Isaya KASERA
34
Rahim Juma NG’WANANG’WAKA
35
Rashid Semindu PAWA

36
Rashid GEWA
37
Shedrack Gabriel MBOGOYE
38
Joyce Judith MARTINE
39
Busoro Mohamed PAZI
40
Richard Raymond MBILINYI
41
Stephen J. NYAGONDE
42
Suleiman H. J. SERERA
43
Vaileth Elias SAMBILWA
44
Theresia Adrian MTEWELE
45
Yohana Haruni MUNEMA
46
Zuberi Said BUNDALA
47
Isane Njale MAZWILE
48
Cretus  MPIGA
49
Jerome Raymond TINGISI



5.   NAFASI MOJA UWAKILISHI UWT

1
Frida WILFRED
2
Joyce Judith MARTINE
3
 Josephine S. MWAGOSE
4
Hawa Mchafu CHAKOMA
5
Mboni Mohamed MHITA
6
Neema K. NYANGALILO
7
Vaileth Elias SAMBILWA
8
Rabia Abdalla HAMID          

6.   NAFASI MOJA UWAKILISHI WAZAZI

1
David John MWAKIPOSA
2
Karim Furaha LICHELA
3
 Yusuph Masige LIMA
4
Salum Salum MGAYA
5
Yohana Haruni MUNEMA

     WAGOMBEA WAHALMASHAURI KUU CCM TAIFA - VITI VINNE ZANZIBAR
1.
Abubakari Ali HAMDANI
2.
Asha Juma OTHMAN
3.
Asha Khamis ABDALLAH
4.
Asha Mohamed OMARI
5.
Ashura Abdallah SIMAI
6.
Bakari Musa VUAI
7.
Bukheri Juma SULEIMAN
8.
Chirstina Joram ANTHON
9.
Daudi K. J. ISMAIL
10.
Fahym  Ally MWINYI
11.
Fadhila Nassor ABDI
12.
Haji Shabani MWALIMU
13.
Ismail Malick MOHAMED
14.
Jumanne Alli HAJI
15.
Khamis Juma KHATIBU
16.
Khamis Mtumwa ALI
17.
Khamisi Rashid KHEIR
18.
Latifa Kassim MABROUK
19.
Lulu Mshami ABDULLAH
20.
Mihayo J. S. N’HUNGA
21.
Mwatima Salum HAMED
22.
Nadra Ghulam RASHID
23.
Omar Juma AMEIR
24.
Omari Sleiman MOHAMED
25.
Rabia Abdalla HAMID
26.
Ramadhan A. SLEIMANI
27.
Sadifa Juma KHAMIS
28.
Salumu Khamis HAJI
29.
Samra Bakari YUSUF
30.
Shaka Hamdu SHAKA
31.
Suna Jumanne SALEH
32.
Thabit Jecha KOMBO

MAJINA YA WAGOMBEA UVCCM "UPDATED"

d 1.    MWENYEKITI   TAIFA 1 Asila Ali SALIM 2 Jamal K. ALI 3 Lulu Mcham ABDALLAH 4 Lusekelo W. MALEMA 5 ... [Read More]