Google PlusRSS FeedEmail
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
Rais Omar Bongo katika mjadala huo
Kijana akichangia
Vijana wakichangia mjadala

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala

Kijana akichangia katika mjadala
Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala



Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
Wageni mbalimbali katika mkutano huo
Ujumbe wa Swaziland
Ujumbe wa Tanzania
Meza kuu
Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza


Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha

Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni

UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dia... [Read More]

BNlXP2uCQAAypL0
Na Mwandishi Wetu
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
      Kwa mujibu wa Jarida hilo la Forbes African Magazine MO   amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
    Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
     Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
    “Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 50 za kimarekani hadi dola Billioni 2.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

JARIDA LA KIMATAIFA LAMFAGILIA MOHAMMED DEWJI KWA UJARIAMALI

Na Mwandishi Wetu Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabili... [Read More]

MPAMBANO WA MASUMBWI UBINGWA WA DUNIA

[Read More]


MWENYEKITI UVCCM TAIFA
ARUSHA, Tanzania

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.

“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"

Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.




Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika  kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.

“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema




Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.

“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa


Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.

Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa


Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro


Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM


Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya


Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro

 

MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI SERIKALI MFUMO WA SERIKALI TATU

MWENYEKITI UVCCM TAIFA ARUSHA, Tanzania MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vi... [Read More]

MEYA WA JIJI LA KAMPALA HOI BAADA YA KUTUOPIWA BOMU LA MACHOZI AKIWA KWENYE MAANDAMANO

Meya wa mji wa Kampala, nchini Uganda, Erias Lukwago, amelazwa hospitalini nchini humo, baada kutupigwa bomu la machozi akiwa ndani ya gari ... [Read More]

Dr. Asha-Rose Migiro
DAR ES SALAAM, Tanzania
NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.

Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.

"Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;

"Mmoja wa Watanzania hawa naomba  nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.

Kaoneka alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk. Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na mchanganyiko wa neno la Kiinereza hata moja.

Katika kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.

Walisema, athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri  ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.

Kaoneka aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni 'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni 'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati usahihi ni "nafanyakazi benki".

Alifafanua kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki wanafanya kazi pamoja. IMEYATARISHWA NA 
BASHIR NKOROMO

DK. ASHA-ROSE MIGIRO AFAGILIWA KWA UMAHIRI WA KISWAHILI

Dr. Asha-Rose Migiro DAR ES SALAAM, Tanzania NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa ku... [Read More]

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA 
Chama cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chadema uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu watatu na zaidi ya watu 40 kujeruhiwa. Tunatoa pole zetu za dhati kwa familia za wafiwa na kwa wale wote waliojeruhiwa katika janga hili la kikatili na kuwatakia uponaji wa haraka. Tukio hili limefuata badala ya lile la awali lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu Joseph mnamo tarehe 5 mei mwaka huu jijini Arusha, ambapo pia lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya watu 60.

 Ni imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Tanzania ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji wa amani. Tunawasihi Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana pasipo sababu.

Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi au umaarufu wa kisiasa . Tunawasihi WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.

Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi CCM UINGEREZA – UK.

MERGEFORMATINET TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1 Contacts Phone +44 74 04 863333, E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org

CCM UK WAGUSWA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA HIVI KARIBUNI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA  Chama cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali t... [Read More]

GEORGE BUSH
DAR ES SALAAM, Tanzania
Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo watahutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake za marais katika kuinua wanawake duniani.

Taasisi ya George Bush  ndiyo imeandaa kongamano  hilo litakalofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 3.

Taarifa iliyotolewa jana na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari, ilisema kongamano hilo, litahudhuriwa pia na mke wa Rais Barack Obama wa Marekani, Michelle na  muasisi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair.

Wake wengine wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji),  Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.

Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake za marais  kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.

“Kongamano hili litakutanisha pamoja wake za marais, maofisa wa Serikali, mashirika binafsi, Asasi Zisizo za Serikali (AZISE) na wasomi kujadili mambo muhimu ya kuchukuliwa hatua ili kunufaisha wanawake,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha, mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika kongamano hilo ni kuinua wajasiriamali wanawake kiuchumi kupitia mafunzo na teknolojia, kupatia fursa wanawake wakulima kwa kupewa mafunzo ya kilimo cha kisasa, mafunzo kuhusu saratani ya matiti na umuhimu wa elimu kwa wanawake.

Kongamano hilo linafanyika sambamba na ujio wa Rais Obama anayetarajiwa kuwasili nchini mwanzoni mwa mwezi ujao.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo kiongozi huyo atazuru katika ziara itakayoanza Juni 26 hadi Julai 2. Nchi nyingine ni Senegal na Afrika Kusini.

Ziara za kiongozi huyo na Bush, inafanya Tanzania mwaka huu kushuhudia ugeni wa watu mashuhuri mfululizo, baada ya Rais Xi Jiping wa China Machi 28, ambapo Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kutembelea Afrika tangu achaguliwe kuwa Rais Machi 14.
Amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia  ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuvutia viongozi hao wa kimataifa kuja nchini.

Wapo  wengine ambao katika maoni yao juu ya ujio wa viongozi hao, wamekuwa wakisema ugunduzi wa rasilimali za asili kama vile gesi, mafuta na madini ya urani ni sababu nyingine ya Tanzania kutembelewa.

Hata hivyo, Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt alikaririwa hivi karibuni akifafanua, kwamba ziara ya Obama haina ajenda yoyote ya kuchukua rasilimali za Tanzania, bali ni ya uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo.

BUSH NA MKEWE KUJA NCHINI MWEZI UJAO

GEORGE BUSH DAR ES SALAAM, Tanzania Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo... [Read More]

E83A0580Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) manispaa ya Singida, Hassan Mazala akizungumza juzi kwenye halfa ya uzinduzi wa hotel ya ya Chemuchemu park na shina la wakereketwa wa CCM wa hoteli hiyo mpya.
E83A0552
Mfanyabiashara maarufu mjini Singida, Mushi Kimboka (aliyweshika maiki) akitoa taarifa yake kwa mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala(aliyevaa miwani) juu ya ujenzi wake wa hotel ya Chemuchemu Park iliyoko katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
E83A0584
Mkurugenzi mtendaji wa hotel ya kitalii ya Stanley Motel, Eward Malya maarufu kwa jina la Hali Ngumu akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliyopo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.Hali Ngumu amewataka wafanyabiashara kufanya biashara halali kwa bidii na kisha wabane matumizi kwa madai kuwa 'hali ni ngumu'.
E83A0553
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala akizindua rasmi hotel ya Chemuchemu Park iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
E83A0563
Wanachama wapya wa CCM baada ya kukabidhiwa kadi juzi na mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa Hassan Mazala (hayupo kwenye picha).
E83A0542
Kikundi cha burudani cha kijiji cha Manguanjuki kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM katika hotel ya Chemuchemu park.
E83A0555
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala (wa tano kushoto mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliypo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida Hassan Mazala, amewahimiza wafanyabiashara wa ngazi zote kujiunga na CCM, kwa madai kuwa ni chama pekee kinachowajengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu.
Mazala ametoa wito huo muda mfupi baada ya kuzindua tawi la wakereketwa wa hotel mpya na ya kisasa ya Chemuchemu Park, iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na CCM kwa muda mrefu na hali hiyo inapaswa kuendelezwa kwa sababu inazinufaisha pande zote mbili.
Akifafanua zaidi amesema amani na utulivu ndio inayopelekea wafanyabiashara na Watanzania wengine wote, wafanye shughuli zao halali kwa uhuru mpana zaidi na ambao hauathiri sheria zilizowekwa.
MNEC huyo amesema CHADEMA inaonyesha ilani yake ni kupandikiza chuki, hasira, kuchonganisha watu na upotoshaji uliopitiliza, na kwa hali hiyo, CHADEMA sio mahali rafiki kwa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mazala ametumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi/watendaji wa CCM na wa serikali yake, kuwa karibu na wafanyabiashara ili kujua matatizo/kero wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa upande wa wafanyabiashara, amewataka wafanye kazi halali kwa bidii na kwa ubunifu mkubwa na kuhakikisha wanabana matumizi au wawe na nidhamu ya matumizi.

MAZALA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA NGAZI ZOTE MKOANI SINGIDA KUJIUNGA NA CCM ILI KUPATA MAFANIKIO

Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) manispaa ya Singida, Hassan Mazala akizungumza juzi kwenye halfa ya uzinduzi wa hotel ya ya Chemuchemu p... [Read More]