Google PlusRSS FeedEmail

CCM BLOG YAWATAKIA HERI NA FANAKA WADAU WOTE KATIKA MWAKA HUU MPYA WA 2014

[Read More]

Mdau hizi ni salamu zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu, Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani) katika kuhitimisha mwaka 2013 na kukaribisha mwaka huu mpya wa 2014, ni muhimu sana, jipe muda uzisome kwa makini ili uweze kuelewa maudhui yake kwa undani hatua kwa hatua bila presha.
Mdau, kusoma hotuba ya salamu hizo, Tafadhali ingia kwenye ukurasa wa Hotuba, Makala na Maoni binafsi au usiende mbali>> BOFYA HAPA

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA, TAREHE 31 DESEMBA, 2013

Mdau hizi ni salamu zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu, Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani) katika kuhitimisha mwaka... [Read More]

BASHIR NKOROMO, DARES SALAAM
Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu vinaowapendekeza wafikiriwe kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu pia Dar es Salaam, imesema taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).

Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.

Makundi ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.

Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.

Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania,   Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania,  Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru,  Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.

Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.

 Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.

KUELEKEA KATIBA MPYA: TASISI ZA KIJAMII, VYAMA VYA SIASA NA VYA KITAALUMA WAPELEKA KWA RAIS WANAOPENDEKEZA WAWEMO BUNGE LA KATIBA

BASHIR NKOROMO, DARES SALAAM Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba ... [Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki baada ya kumwapisha katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali mpya wa Polisi (IGP) Ernest Mangu na Naibu IGP Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali, Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali mpya wa Polisi (IGP) Ernest Mangu na Naibu IGP Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo jioni.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Saidi Mwema, katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, leo jioni.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Ernest Mangu, Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) Abdulrahman Kaniki. Picha na Ikulu

AMIRIJESHI MKUU, RAIS JAKAYA KIKWETE AMWAPISHA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijin... [Read More]

RAIS Mstaaf wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,akikata Utepe kuashiria kuifunga Makao Makuu ya Benki ya  PBZ Ismamic Bank ilioko katika jengo la Bima  Mpirani Zanzibar, kushoto Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee na Mkurugenzi  Mtendaji PBZ Bwa Juma Amour, ikiwa ni shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MZEE MWINYI AFUNGUA MAKAO MAKUU YA BPZ MJINI ZANZIBAR

RAIS Mstaaf wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,akikata Utepe kuashiria kuifunga Makao Makuu ya Benki ya  PBZ Ismamic Bank ilioko katika jen... [Read More]

NA BASHIR NKOROMO, DSM
Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imemkariri Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akisema kuwa Kamishna Mangu (pichani) anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

"Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi", tarifa hiyo imesema.

Taarifa hiyo imesema kuwa pia Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Taarifa hiyo imesema, Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI (IGP), ABDULRAHMAN KANIKI NAIBU IGP

NA BASHIR NKOROMO, DSM Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania, Rais Jakaya Kikwete Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua K... [Read More]



  •  Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume
  • Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi iliyofanya kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa ulipofika. Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya Tume kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba Nape alisema;
“CCM inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa waliyofanya, wamekamilisha kazi waliyotumwa salama na kwa wakati. Sasa tuwaachie wanaondelea na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye wananchi. Tunautakia kila lakheri mchakato huu, utumike kutuunganisha watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape
Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape anasema;
“Tumesikiliza hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali tatu, tumezisikia, tutazichukua,kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada ya tafakuri ya kutosha tutaamua ipasavyo” alisisitiza Nape.
Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.

CCM YAIPONGEZA TUME YA KATIBA

 Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza T... [Read More]


 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.
Jaji Warioba akikabidhi rasimu hiyo pia kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti  wa NCCR Mageuzi,  James Mbatia.
Rais Jakaya Kikwete, Dk. Shein, Dk. Bilal, Maalim Seif Sharif Mahad na viongozi wengine wakiwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

RAIS KIKWETE, DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA LEO

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, ... [Read More]

PATA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO

[Read More]

KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA GNSM CONTRACORS CO. LTD INAYOENDESHA NA GEOFREY MUNGAI YATOA MSAADA WA CHAKULA CHA MWAKA MPYA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

Mkurugenzi  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai kulia akikabidhi ms... [Read More]

SHUNYANGA, Tanzania
Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75)  amefariki dunia  baada ya kuugua kwa muda mrefu kifua kikuu.

Taarifa iliyopatikana kutoka mjini Shinyanga, imesema, diiwani huyo alifariki  jana mida ya saa 10 jioni katika hospitali ya mkoa  alikokuwa amelazwa   kwa muda wa siku mbili baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani  wakati akiendelea kutumia  dawa .

Kaimu Mwenyekiti wa  Halmashauri hiyo, Ngassa Sosthenes  amesema hayo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga  na kufafanua kwamba katika uhai wake diwani huyo  alisumbuliwa na maradhi ya ugonjwa huo wa kifua kikuu licha ya kwamba alikuwa akipata katika hospitali  mbalimbali.

Alisema, Desemba 26 mwaha huu, walipata taarifa ya kuzidiwa kwa diwani huyo wakaamua kumpeleka haraka katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na ndugu zake na madaktari kuendelea kumfanyia uchunguzi zaidi.

Amesema leo mwili  umetolewa  hospitali  na kuumpeleka kwenye kata yake  kwa ajili ya wananchi kwenda kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi kwenda kufanyika  mkoani Geita katika kata ya Mlele  walikozikwa pia wazazi wake.

Kwa mujibu wa Kaim Kwenyekiti huyo wa Halmashauri, Diwani huyo aliyezaliwa mwaka  1937, ameacha watoto saba wajane wawili na amekuwa diwani wa kata hiyo kwa awamu mbili mfululizo tangu mwaka 2005.

Msiba wa diwani huyo umekuja huku msiba mwingine wa Diwani wa  kata ya Nyida  ukiwa bado unaombolezwa na wananchi kufuatia diwani nao  Mshindikwa  Masele (40) kufariki dunia kutokana na ajali ya pikipiki yake aliyokuwa akiiendesha akitokea Isaka wilayani Kahama   Desemba  21, mwaka huu.

DIWANI MWINGINE WA CCM AFARIKI DUNIA SHINYANGA

SHUNYANGA, Tanzania Diwani wa CCM katika kata ya Mwakitolyo, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Kasanga Lumala (75)  amefariki dunia... [Read More]

MWENYEKITI wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam,  Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni mwalikwa kwenye Kichao cha kawaida cha Hamlashauri Kuu Kata ya Azimio jimboni humo, jana jioni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Esa Uswege.
=================
BASHIR NKOROMO, TEMEKE, Tanzania
Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Kibamba, Dar es Salaam, Ayoub Semvua, amesifu kuwa kasi ya utendaji kazi ya mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu ni kubwa na huenda inastahili kwendana na kasi ya utendaji wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.

"Nilipoitwa na rafiki zangu hawa wa Azimio, sikujua kama na wewe utakuwepo,  lakini nikawa nimenuia kuwa hata kama hutakuwepo nitakusifia kwa kazi kubwa unayofanya ya kimaendeleo katika kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo hili la Temeke... na sasa kuwa nimekukuta nitakusifu hapa hapa, wewe kasi yako ya utekelezaji wa ilani ya CCM inatisha, na kwa kasi hii unaweza kuwa unastahili kasi ya viongozi wetu  Ndugu Kinana, Mzee Mangula na Kijana wao Nape", alisema Semvua alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Azimio, ambacho alikuwa mgeni mwalikwa.

"Huyu Katibu wetu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula na kijana wao Nape, kasi yao ni kilometa 140 kwa saa. Kama kuna mtu aliyeingia katika uongozi wa CCM kwa lengo tofauti kasi hii lazima itamshinda na bora ajiondoe mwenyewe mapema",  Semvua aliongeza.

Semvua alisema, kutokana na utendaji bora na shirikishi wa Mtemvu, jimbo la Temeke limekuwa na sura tofauti kimaendeleo ikilingtanishwa na miaka 20 ikiongozwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa sasa wa TLP, Augustine Mtema ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

"Mfano mzuri wa maendeleo, niliyoshuhudia ambao kila mtu anauona ni barabara za lami zilivyotanda katika maeneo mbalimbali ndani ya Temeke, tangu nimetoka Kibamba nimeteleza kwa lami moja kwa moja bila kugusa udongo hadi naingia kwenye Ofisi hii ya CCM Azimio", alisema Semvua.

Semvua alisema, kutokana na kasi inayoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na viongozi wengine kama Mtemvu, CCM itashinda urais ba viti vingi vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2014.

Aliwataka wana-CCM kuachana na tabia ya kuwa na nongwa aliyoifananisha na ya kinywaji cha kahawa, ambayo baadhi wamekuwa wakidumu nayo kiasi cha kuchagua wapinzani wakidhani wameikomoa CCM kumbe wamejikomoa wenyewe.

"Pale wilaya ya Kinondoni tumepoteza viti viwili vya ubunge na vingi tu vya udiwani na mitaa, sababu kubwa ni nongwa tu. Wanasema, Wakasema aaa,  bora tuupe upinzani tuheshimiane. Sasa ukiwauliza pale Kawe na Ubungo kwamba mliwapa ubunge wapinzani sasa heshima gani mnapata? hawana jibu zaidi ya kuinama chini", alisema Semvua.

Akifungua kikao hicho, Mtemvu aliwataka wana-CCM na wananchi kwa jumla kuwapima viongozi kwa utendaji kazi zao na sio kwa uhodari wa porojo nyingi kwa sababu wananchi wanachohitaji ni maendeleo.

Alisema, katika kipindi chake cha Ubunge, Temeke imeweza kuwa na barabara karibu 15 zenye lami hadi pembezoni mwa mji huo na kwamba zile zisizokuwa na lami zimeboreshwa kwa kiwango kibwa kiasi cha kupitika nyakati zote.

SEMVUA: KASI YA MTEMVU INAENDANA NA YA KINANA, NAPE

MWENYEKITI wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam,  Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni m... [Read More]

RAIS KIKWETE AWAJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA MUHIMBILI Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa kat... [Read More]

 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Banki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya kuwasili. ((Picha na Freddy Maro)

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI KUCHEKIWA AFYA   Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete... [Read More]

JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU KWA RAIS KIKWETE, DK. SHEIN JUMATATU HII

JAJI WARIOBA DAR ES SALAAM, Tanzania Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid, imesema, Jumatatu ijayo y... [Read More]

TABOTA, Tanzania 
Watu wawili wamekamatwa na Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji ya babu yao.

Watuhumiwa hao ni Mwashi Mipawa (17) na Kashinje Mipawa(15)wote wakazi wa kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa.

Tukio hilo lilitokea Desemba 25 majira ya saa 7:30 jioni katika kijiji cha Ibole kata ya Igurubi wilayani hapa ambapo watuhumiwa hao ambao ni wajukuu walimpiga babu yao Makelemo Jagadi (55) na kusababisha kifo chache.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa amelewa pombe na alipofika nyumbani alianza kutukana hali ambayo ilipelekea kuanza kupigana na mke wake Milembe Mpela(50) na ndipo wajukuu zake walipoingilia ugomvi huo.

Aidha wakiwa katika ugomvi huo watuhumiwa hao walimpiga Babu yao Makeremo kwa kitu kizito kichwani kwenye paji la uso pamoja na kumvunja mkono wa kushoto na kusababisha kifo hicho.

Diwani wa kata ya Igurubi Bw.Edson Sadani alisema kuwa kufuatia ugomvi huo pia mke wa marehemu huyo aliumia na kusema kuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Peter Ouma alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

WAJUKUU WAMUUA BABU YAO KWA KIPIGO SIKU YA KRISMAS!!!!

TABOTA, Tanzania  Watu wawili wamekamatwa na Polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za mauaji ya babu yao. Watuhumiwa hao ni Mwash... [Read More]

MSIKILIZE LIVE, DAKTARI HUYU WA KUTIBU UMASIKINI

[Read More]

NA MWANDISHI WETU
VIONGOZI wa Jumuia ya Wazazi katika Kata za Temeke, Dar es Salaam, wametoa madai mazito kwa Mjumbe wao wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo Taifa, Nicholaus Msemo, kwamba 'ameingia mitini' tangu walipomchagua kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu wa Jumuia za CCM uliopita.

Wamedai kwamba tangu kuchaguliwa kwake hawajamuona kushiriki katika shughuli mbalimbali za Jumuia hiyo ikiwemo kufanya ziara walau za kuwashukuru wapigakura hao ambao ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam.

Malalamiko hayo juu ya Msemo kudaiwa kuingia mitini, yalitolewa mwanzoni mwa wiki hii, kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Angela Kizigha, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi mmoja, ulioko Mbagala Kuu, wilayani Temeke na kuhudhuriwa na viongozi ngazi za kata zote za wilaya hiyo ambao ni Wenyeviti, Makatibu na Makatibu wa  Elimu, Mazingura na Uchumi.

Mkutano huo uliitishwa na Kizigha kwa lengo la kuwashukuru viongozi hao, kwa kumchagua kuwa Mweneyekiti wao katika uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliofanyika Mwaka jana, ambapo katika shukurani hizo, aligawa sare za Jumuia hiyo kwa wajumbe wote 60 waliohudhuria na pia kutoa sh. milioni 1.2 kwa ajili ya kuanzisha Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) kwa viongozi hao.

"Mwenyekiti, kwanza sisi wenyeviti na viongozi wengine katika kata za Temeke, tunakupongeza kwa uamuzi wako wa kutenga mda kuja kutushukuru, lakini tunaomba pia utuambie aliko Ndugu Msemo. Huyu tangu tulipomchagua akapita tena kwa mbinde hatujawahi kumuona kabisa", alisema  Mweneyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Makangarawe Haruna Mtulya, wakati akizungumza kwa niaba ya wenzake katika mkutano huo.

Walidai kwamba mbali na kutojitokeza kuwashuku, tangu walipomchagua, Msemo amekuwa akiwapiga chenga, badala ya kuwa nao karibu kwa lengo la kuwapa ushirikiana katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wanachama na wananchi wa kawaida ambazo zimekuwa zikijitokeza katika kata zao.

Akijibu, Angela ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashairiki, alisema, anatambua kwamba katika Jumuia hiyo wapo baadhi ya viongozi ambao baada ya kuchaguliwa wamejiona kwamba wameshamaliza kazi, na hivyo hawajishughulishi tena, katika kufuatilia kero za wanachama na wananchi kwa jumla, na kibaya zaidi wengine hawahudhurii hata kikao vya kikatiba.

"Sitawajibu kuhusu hili la Msemo kwa kuwa siyo ajenda iliyonileta, hapa nimekuja kuwashukuru na kutatua baadhi ya kero nilizoahidi kwamba tutasaidiana kuzifanyia kazi kama kuanzisha Saccos na kugawa sare maalum za Jumuia yetu, hili nimefanya, lakini kwa kweli tunao viongozi wa aina hii na baadhi yao tunakusudia kuwaandikia barua za kujieleza kwa nini wasivuliwe uongozi kama hawataki kuutumikia", alisema Angela.

Habari zilizopatikana, zimeeleza kwamba, Kikao cha Baraza  Kuu la Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, kilichofanyika juzi, kimeazimia kumwandikia barua Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mustafa Yakub kutokana na kudaiwa kutoshiriki kikamilivu katika shughuli za jumuia ikiwemo kukwepa vikao rasmi.

Akizungumza kwa simu, Msemo akikana tuhuma dhidi yake, akidai kwamba amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali ikiwemo kufadhili mikutano ya Jumuia hiyo, huku akisisitiza kwamba, kuwashukuru wapigakura siyo lazima ni jambo la kufanywa kwa hiari.

"Hayo ni majungu na fitina za kisiasa tu, mimi nimekuwa nikishiriki shughuli nyingi sana,japokuwa nimewahi kukosekana baadhi ya vikao, lakini sasa kukosekana kikao kimoja tu ndiyo ionekane sishirikiani kabisa na wenzangu? Na kuhusu hili la kuwashukuru wapigakura, hili siyo lazima ni la hiari", alisema Msemo.

Baada ya habari hii kuchapwa leo katika gazeti la UHURU, Mlalamikiwa Ndugu Msemo ameelezea kutoridhishwa na madai hayo dhidi yake. Kwa kuwa kwenye gazeti hapati zaidi fursa ya kutoa maoni yake kwa marefu na mapana, Tumeichapa stori hiyo hapa kumpa fursa hiyo ili tumsikilie.  Mbali na Msemo, wengine pia mnakaribishwa kutoa maoni kuhusu stori hii.


Mtayarishaji Mkuu
CCM Blog
0712 48008

KIONGOZI ADAIWA KUINGIA MITINI TEMEKE, ASAKWA NA WAPIGAKURA WAKE

NA MWANDISHI WETU VIONGOZI wa Jumuia ya Wazazi katika Kata za Temeke, Dar es Salaam, wametoa madai mazito kwa Mjumbe wao wa Baraza Kuu la Ju... [Read More]

 Rais Jakaya Kikwete akikaribisha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moo, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Desemba 24, 2013. Badaye walikuwa na mazungumza kuhusu masuala mbalimbali ya Kimataifa hususan amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine Duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon. Rais Kikwete yupo jijini  New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake. (picha na Freddy Maro)
 Wakizungumza
 Rais Kikwete akimshukuru Ki-Moon baada ya mazungumzo yao
 Ki-Moon akimvuta pembeni Rais Kikwete kisha..
Akamwambia jambo kabla ya kuagana

RAIS KIKWETE AENDELEA VEMA NA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE MAREKANI, AKUTANA NA BAN KI-MOON

 Rais Jakaya Kikwete akikaribisha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moo, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Mare... [Read More]

X-MASS NJEMA KWA WOTE

[Read More]

Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akitazama pikipiki mbili kati ya 44 zilizotolewa msaada kwake na  Ubalozi wa China  nchini pamoja na Kampuni ya  Futang ya China katika  makabidhiano yaliyofanyika  kijijini kwake, Kibaoni wilayani Mlele Desemba  24, 2013. Wapili kulia ni  Balozi wa China nchini, Dr. Lu Youqing. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PINDA APOKEA MSAADA WA PIKIPIKI 44

Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akitazama pikipiki mbili kati ya 44 zilizotolewa msaada kwake na  Ubalozi wa China  nchini pamoja na Kampuni ... [Read More]

 Na Oscar Assenga,Korogwe.
JESHI la Polisi mkoani  hapa kwa kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma za kuhusika na kuweka mabomu  yaliyokuwa yameandaliwa tayari kwa kulipuka kwenye nyumba mbili tofauti za ibada.

Pamoja na mabomu hao watuhumiwa hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi wanatuhumiwa kuhusika na kukutwa na vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko ya mabomu hayo pamoja na silaha za jadi ambazo pia zilikuwa zimefichwa katika nyumba hizo za ibada huku katika Kijiji cha Maili kumi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.


Vifaa vingine ni mapanga,visu,Mifuko ya Sandarusi ,manati,vifuniko 12 vya maji,kofia nne na vitambaa vya kufunga kichwani pamoja na Tende walizokuwa wakitumia kama chakula.

Akizungumza  katika mahojiano na Tanga Raha Blog, ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Constantine Massawe alisema kuwa watu hao walikamatwa Disemba 17 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku huko wilayani Korogwe.

Kamanda Massawe alisema kuwa Askari Polisi wakiwa kaika kizuizi cha Maili 10 wilaya ya Korogwe waliwatilia shaka vijana watatu wa kiume waliokuwa wamebeba vifurishi na walipotaka wasimame walikimbilia msituni na ndipo mmoja alipokamatwa na Askari hao.

“sasa baada ya kukamatwa huyu mmoja na ndipo alipopekuliwa na kukutwa na vifaa hivyo kwenye begi lake na ndipo msako wa kuwatafuta hawa wengine ulipoanza”,alisema Kamanda huyo.

Hata hivyo alisema kuwa  alisema kuwa katika msako huo ambao ulifanywa na Polisi kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Maili kumi ndipo walipobaini kuwepo kwa vifaa vingine katika nyumba mbili tofauti za ibada zilizopo Kijijini hapo.

Alisema watuhumiwa hao baada ya mwenzao kukamatwa walikimbia kujificha kwenye nyumba hizo za ibada ndipo wakazi wa maeneo hayo walipowatilia mashaka na kutoa taarifa kwa Polisi.

“Baada ya kukimbizwa wakaona mahali salama kwao ni kwenye nyumba za ibada lakini wananchi wa eneo lile waliwatilia shaka na kuamua kutoa taarifa ndipo yalipokutwa hayo mabomu ambayo yalikuwa yameshaandaliwa kulipuka kwani kulikuwa na petrol na tambi ndani ya chupa hizo na zile gololi hutumika kama silaha zinapolipuka”,alifafanua Kamanda Massawe.

Hata hivyo kwa mujibu wa Kamanda huyo ni kwamba baada ya mahojiano ya Polisi na watuhumiwa hao walibaini kuwa ni miongoni mwa wale waliokimbi katika oparesheni ya kuwasaka wahalifu iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu huko wilayani Kilindi.

“Hawa ni miongoni mwa wale waliosababisha machafuko wilayani Kilindi ambapo Mgambo aliuawa sasa wengine walikimbia na inaonekana nao hawa wapo katika mtandao huo”,alisema.

Kamanda Massawe alitoa wito  kwa wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa taarifa mara moja kwa Polisi mara wanapobaini kuwepo kwa watu ambao wanawatilia mashaka kwenye maeneo yao.

WATENGENEZAJI SABA WA MAMBOMU YA KIVITA WASHIKWA KATIKA NYUMBA YA IBADA

  Na Oscar Assenga,Korogwe. JESHI la Polisi mkoani  hapa kwa kushirikiana na wakazi wa Kijiji cha Maili kumi wilayani Korogwe wamefanikiwa k... [Read More]