Google PlusRSS FeedEmail

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa kwa nguvu na madereva wa pikipiki za kubebea abiria maarufu kama Boda boda wakati wa kikao na Boda boda hao kilichofanyika ukumbi wa Mtenda ,Soweto Mbeya ikiwa moja ya sehemu za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na madereva wa Boda boda kwenye ukumbi wa Mtenda ,Soweto mkoani Mbeya.
 Sehemu ya Madereva Boda boda waliohudhuria kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana

 Sehemu ya Boda Boda zikiwa nje ya ukumbi wa Mtenda,Soweto mkoani Mbeya wakati kikao cha Madereva Boda Boda na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Madereva wa Boda Boda

KINANA AKUTANA NA BODA BODA WA MKOA WA MBEYA

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishangiliwa kwa nguvu na madereva wa pikipiki za kubebea abiria maarufu kama Boda boda wakat... [Read More]



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akimsindikiza na kuagana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Waziri huyo ameondoka jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, wakati alipokuwa akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, jana usiku kurejea nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA FINLAND BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, waka... [Read More]

 Makamu Mwenyekiti CCM(Bara) Ndugu Phillip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi wakati wa mapokezi kwenye ofisi za CCM Mkoa,Makamu Mwenyekiti amewasili mkoani Mbeya tayari kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi .
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phillip Mangula akisalimiana na Kanali Mstaafu Limbo Masanja mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya tayari kwa sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM zitakazofanyika tarehe 2 Februari kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka nje ya uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya akiongozana na Mwenyekiti wa wilaya ya Momba Ndugu Juma Yusufu Rashid na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dogo Idd Mabrouk nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumzwa na baadhi ya waandishi wa habari waliofika mkoani Mbeya kwa ajili ya kuapata habari na matukio mbali mbali yatakayojiri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM.
Bidhaa za CCM zikiwa kwenye soko sambamba na maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya kuzzaliwa kwa CCM zinazofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

MAKAMU MWENYEKITI CCM (BARA) NA KATIBU MKUU WAWASILI MBEYA TAYARI KWA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CCM

 Makamu Mwenyekiti CCM(Bara) Ndugu Phillip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi wakati wa mapokezi kw... [Read More]

 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR

 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapish... [Read More]


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati alipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAWAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, SAYANSI ELIMU IKULU DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Mi... [Read More]

Add caption
MOSHI, Tanzania
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshuhulikia Utawala Bora, Kaptein mstaafu, George Mkuchika amesema migogoro ya ardhi, mauaji ya maalbino na vikongwe, wanachi kujichukulia sheria mikononi, rushwa pamoja na ujangili zinadaiwa kuwa moja ya sababu zinazochangia kuporomoka kwa Tanzania katika viwango vya utawala bora duniani.

Mkuchika aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kikao ambacho ni cha kwanza kwa mwaka 2014 na maalum kwa ajili ya kujadili vipauumbele vya Bajeti ya Mkoa huo kwa mwaka 2014/2015.

Kaptein Mkuchika alisema kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa utawala bora nyuma ya Rwanda kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki nyuma ya Rwanda, 17 katika ukanda wa Afrika na 102  kati ya nchi 176  duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo Tanzania imeshuka kiwango katika ukanda wa Afrika katika kipindi cha miaka miwili.

Alisema katika taarifa hizo, Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 10 miaka miwili iliyopita na kuongeza kuwa kuporomoka huko kunatokana na kukithiri kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya albino na vikongwe, mapigano ya wakulima na wafugaji, Ujangili, ambapo zaidi ya watu kumi walikufa mkoani Manyara.

 “tukiangalia kiundani Matukio haya yamesababisha kwa kiasi kikubwa Tanzania kuporomoka katika viwango vya utawala bora, miaka miwili iliyopita, tulikuwa wa 10 katika bara la Afrika, Afrika mashariki tunashika nafasi ya 2, duniani tuko nafasi ya 102 kati ya nchi 176, kukithiri kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya albino na vikongwe, mapigano ya wakulima na wafugaji, Ujangili, zaidi ya watu kumi walikufa mkoani Manyara,” alisema Mkuchika.

Kuhusu swala la Rushwa, Mkuchika alisema tatizo hilo haliwezi kumalizwa endapo wananchi wenyewe hawatabadili tabia yao kwani uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya Rushwa ndogo hutokana na Wananchi wenyewe.

Alisema katika swala la Rushwa, kamati za ushauri za mikoa na mabaraza ya Halmashauri zina nafasi kubwa kufanikisha vita na mapambano dhidi ya vitendo hivyo kutokana na kuhusika kwao katika maamuzi mengi yanayohusu maendeleo ya mikoa na Halmashauri zao.

“kweli kwa kiasi kikubwa kamati ya ushauri ya mkoa, mabaraza ya madiwani zina nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la rushwa katika Halmashauri na mikoa yao, endapo watu hawa watabadilika hasa katika maamuzi wanayoyachukua katika shughuli na vikao vyao,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama aliwataka watendaji katika halmashauri zote za wilaya hiyo kutekeleza agizo la kutenga mgao wa asilimia 15 kwa ajili ya makundi maalum ambayo ni asilimia 5 kwa ajili ya vijana asilimia 5 ya wanawake na asilimia5 kwa ajili ya vita dhidi ya mapambano ya  Ukimwi ambapo alisema mkoa haitasita kuichukulia hatua Halmashauri itakayoshindwa kutekjeleza agizo hilo.

“kila halmashauri inatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya makundi maalumu ambapo , asilimia 5 kwa vijana, tano kwa wanawake na asilimia 5 kwa ajili ya mapambano dhidi ya vita ya Ukimwi, na halmashauri itakayoshindwa kutekeleza itachukuliwa hatua kali,” alisema.

WAZIRI MKUCHIKA AELEZA SABABU ZA TANZANIA KUSHUKA VIWANGO VYA UTAWALA BORA DUNIANI

Add caption MOSHI, Tanzania WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshuhulikia Utawala Bora, Kaptein mstaafu, George Mkuchika amesema migogoro ya ... [Read More]

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.



   Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.

Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya. Katibu wa NEC ... [Read More]


 Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.

MABASI YA MWENDO KASI YAANZA MAJARIBIO JIJINI DAR

 Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatiz... [Read More]


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya.
Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya mara baada ya mpira kumalizika.













NAPE ATEMBELEA SOKO LA SIDO MWANJELWA MJINI MBEYA KIMYA KIMYA

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nap... [Read More]

 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ikiwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambayo kitaifa mwaka huu inafanyika mkoani Mbeya.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Maganga Sengelema akimuonyesha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sehemu ya kuweka jukwaa la waandishi wa habari kwenye uwanja wa Sokoine ambapo sherehe za miaka 37 ya CCM zitasheherekewa kitaifa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa maandalizi ya awali katika uwanja wa Sokoine ambao unategemewa kufanyika kwa sherehe za mika 37 ya CCM tarehe 2 mwezi wa februari mwaka huu,mgeni wa heshima anategemewa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kurekebisha uwanja wa Sokoine ili uweze kutumika vizuri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM .

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM YAPAMBAMOTO

  Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Luteni Mstaafu Maganga Sengelema akifafanua jambo mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye uwan... [Read More]

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi (kushoto), Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.Picha na Bashir Nkoromo

REGINALD MENGI AKUTNA NA KINANA LEO

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi (kushoto), Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya ... [Read More]

RAIS KIKWETE AAMRISHA JESHI KUSIMAMIA UTOAJI HUDUMA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MOROGORO

RAIS KIKWETE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameliam... [Read More]


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi  Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
R ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo.



 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa  CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo, katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar

DK. SHEIN AMNADI RASMI MGO MBEA WA CCM JIMBO LA KIEMBESAMAKI, MAHMOUD THABIT KOMBO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu... [Read More]

MWANDISHI WA HABARI LEO KILIMANJARO, ARONLD SWAI, MWENYEKITI MPYA UVCCM WILAYA YA HAI

Arnold Swai (wa kwanza kushoto)wakati wa upigaji kura, zoezi lilofanyika juzi, wilayani Hai kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti Mjumbe wa... [Read More]