Google PlusRSS FeedEmail

JERRY SLAA KUKABIDHI ZAWADI KWA WATEJA WA BANDA LA MeTL SABASABA



IMG_1291
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.
Na Mwandishi Wetu
WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kesho Jumatatu wanatarajiwa kuchezeshewa droo maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.
Katika droo hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali watakaojishindia zawadi hizo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer alieleza kuwa, droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja wote waliopata kutembelea banda hilo tokea siku ya kwanza na kujiorodhesha majina yao
Fatema alisema MeTL Group imeamua kutoa zawadi hizo kama shukrani na kujitangaza zaidi kwa wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa za MeTL Group.
“Kwa ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group, kama inavyojulikana, ‘The People’s Brand’, kwa droo hii wateja wetu watafurahia kwa zawadi hizo nono” alisema Fatema.
Katika droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki, zawadi za khanga, vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Aidha, MeTL Group imetambulisha rasmi vinywaji vyake vipya kwenye maonyesho hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye maonyesho hayo, MO Cola, MO Portello na MO Malt. Vingine ni MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).

This entry was posted in

Leave a Reply