Google PlusRSS FeedEmail


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, akishiriki katika mazishi ya mmoja wa vijana watatu waliokufa baada ya kupata ajali ya gari katika Mlima Ukwasi, lilikuwa likienda Kijiji cha Tungamalenga kupeleka biashara ya maji. Mazishi hayo yalifanyika katika Kijiji cha Kidamali Kata ya Mzihi, Jimbo la Uchaguzi la Kalenga, Iringa Vijijini, jana.
 Mgombea wa CCM katika Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa akishiriki katika maziko ya mmoja wa vijana waliokufa kwenye ajali hiyo. Waliokufa kwenye ajali hiyo ni dereva Nyagile Luvanda,Sabasaba Kuzungola na Ansikali Chengula.CCM imetoa ubani kwa wafiwa sh. mil. 1 na kuahidi kuwasomesha watoto wa waifiwa.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia tiketi ya CCM, Gobfrey Mgimwa  (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya vijana wa Kijiji cha Kidamali alipokwenda kuwafariji wafiwa wa misiba hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (aliyevaa kombatii), akiwa na Mgombea Ubunge Kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (kulia kwake), na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu walipofika Kijiji cha Kidamali.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akisalimiana na baadhi ya vijana katika Kijiji cha Kidamali.
 Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu wakilia na  baada ya kuona magari yaliyobeba miili katika Kijiji cha Kidamali.
 Sehemu ya waombolezaji
 Jeneza lenye mwili wa mmoja wa vijana walikufa kwenye ajali hiyo ukiwasili eneo la maziko
 Mwili mwingine ukiwasili eneo la makaburi katika Kijiji cha Kidamali
 Sasa ni wakati wa maziko. Moja wa wana CCM akishiriki katika maziko hayo
 Nchemba na Mgimwa wakiwa katika maziko hayo
 Wanahabari wakiwa katika maziko hayo
 Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kidamali, walioshiriki mazishi ya vijana hao, wakisoma vipeperushi vilivyokuwa vikisambazwa na wafuasi wa Chadema wakati maziko ya vijana hao yakiendelea katika makaburi kwenye Kijiji cha Kidamali leo.


 Ulinzi wa askari ukiwa umeimarishwa wakati wa maziko ya vijana hao.
Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya vijana hao. Imetayarishwa na Kamanda Richard Mwaikenda

MWIGULU, MGOMBEA WA CCM KALENGA, WASHIRIKI MAZISHI YA WANANCHI WATATU WALIOKUFA KWA AJALI YA GARI JIMBO LA KALENGA, IRINGA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, akishiriki katika mazishi ya mmoja wa vijana watatu waliokufa baada ya kupata ajali ya gari k... [Read More]

The Boston University Director of the African Presidential Centre Ambassador Charles Stith(left) hands over to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete a 2013 Report on African Leaders and State of Africa at State House Dar es Salaam. Feb 28, 2014. Professor Stith who is also a former US ambassador to Tanzania is an expert on Political and Economic Development of the Sub-Saharan Africa.(photo by Freddy Maro)

PRESIDENT KIKWETE RECEIVES A REPORT ON STATE OF AFRICA FROM AMBASSADOR CHARLES STITH

The Boston University Director of the African Presidential Centre Ambassador Charles Stith(left) hands over to President Dr.Jakaya Mrisho Ki... [Read More]


HANANG, Tanzania
MKUU wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme amewakutanisha vijana 316 wa wilaya hiyo na kuunda SACCOS yao, katika kutelekeza sera ya CCM ya kuwakomboa vijana kichumi na kuondokana na umaskini na pia kuwaondoa vijana kutojihisisha na shughuli ambazo hazina tija kwao na taifa.

Saccos hiyo ambayo tayari imesajiliwa kwa jina la Hanang Vijana  inawanachama wapatao 269 katika wenye ikundi vitano vya ufugaji kuku wa kienyeji, ufyatuaji wa matofali kisasa kwa teknolojia ya hydroform, bodaboda,  ufugaji nyuki na kilimo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema leo kwamba, Saccos hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni wilayani Hanang na

Waziri wa Habari, Vijana, Utamadu7ni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara waziri wa habari, vijana.

"Vijana wa wilaya hii wamefurahia muungano huu kwani wamesema ni kwa mara ya kwanza tangu wilaya imeundwa kwa mkuu wa wilaya kuwaunganisha vijana bila kujali itikadi zao wala dini wa jinsia", alisema Mkuu huyo wa nwilaya

Alisema vijanahao wameishukuru sana serikali kwa mpango huo wa kwaunganisha na wameahidi kushiriki kikamilifu katika shushuli za kiuchumi na kushirikiana na serikali.

Mkuu huyo alisema Saccos hiyo inaundwa na vija wote kuanzia wenye elimu ya Chuo Kikuu mpaka darasa la saba na

ambao hawakwenda shule na kauli mbiu yao ni: "Juhudi za vijana ni ukombozi wa taifa- Hanang amani na maendeleo".

DC HANANG AKUTANISHA VIJANA 316 KUANZISHA SACCOS

HANANG, Tanzania MKUU wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme amewakutanisha vijana 316 wa wilaya hiyo na kuunda SACCOS yao, katika kutelekeza ... [Read More]

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, IKULU DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es s... [Read More]

 Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
  Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
  Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga.
 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.

MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA

 Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, I... [Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe  kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya  Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA MAWASILIANO

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring Sy... [Read More]

TAARIFA KUTOKA IDARA YA HALI YA HEWA

TAARIFA YA HALI YA HEWA [Read More]


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadick.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine  kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho  kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu  kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo February 27, 2014. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AUNGANA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA BALOZI KAZAURA

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kik... [Read More]

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, alipozindua rasmi kampeni za CCM jioni hii katika mapnei za CCM zilizofanyika Uwanja wa Ifunda, Iringa Vijijini.(Picha na Bashir Nkoromo)

Mwigulu:Slaa ana mapepo

Na Mwandishi Wetu, Kalenga, Iringa

NAIBU Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mwigulu Nchemba amesema kichwa cha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Willibrod Slaa kina mapepo zaidi ya saba.

Amesema Dk.Slaa baada kuacha kumtumikia Mungu mawazo na mtazawamo wake amekuwa ni mtu wa kuzusha uongo.

Mwigulu alitoa kauli hiyo jana kijiji cha Ifunda katika Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa wakati akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa chama hicho.

CCM imemsimamisha mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa jimbo la Kalenga Dk.William Mgimwa, Godfrey Mgimwa kugombea nafasi ubunge kujaza nafasi iliyoachwa wazi.

Alisema kuwa Biblia inasema kuea mtumishi wa Mungu atakayerudi nyuma atakuwa na mara sabini, na hicho ndicho kinachotokea kwa Dk.Slaa.

"Ndio maana hivi sasa ana miaka 70 lakini anamchumba, mate yake yamejaa uongo.Amezoea kusema uongo na kufanya maandamano.

"Kazi ya Dk.Slaa ni kusema uongo kila siku.Na tabia yake ya kufanya maandamano imefika mahali hata akilala usiku anamka na kuanza kuzunguka kitanda maana anafanya maandamano hadi nyumbani kwake,"alisema.

Aliongeza kuwa leo hii akitakiwa kutaja jina la mtu mmoja nchini ambaye hamuheshimu basi atataja jina la Dk.Slaa na hiyo inatokana na tabia yake  ya kusema uongo na kutukana kwenye majukwaa.

Hata hivyo, alisema kuwa Dk.Slaa anahangaika kwasababu kila mwisho wa mwezi analipwa sh.milioni saba , hivyo kinachomfanya kuzungumza ni kufanikisha maslahi yake na wenye uchunguzi na wananchi ni Serikali ya CCM.

Wakati huo huo,Mwigulu alisema kuwa  wenye kutaka nyongeza ya posho katika Bunge la Katiba wanajisumbua huku akisisitiza anayeona haitoshi aondoke.

Alisema yeye akiwa Naibu Waziri wa Fedha, hawezi kukubali kuona posho inaongezwa na huku akisisitiza atakuwa makini kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali.

Alisema kabla ya kuwa Naibu Waziri amekuwa akikerwa na tabia ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali na ndio maana aliamua kukemea hata kitendo cha  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kumshinikiza mbunge wa viti maalumu wa chama chake aende Dubai kwa kazi maalumu,"alisema Mwigulu.


Amesema kuwa Dk.Slaa anahangaika kwasababu kila mwisho wa mwezi analipwa sh.milioni saba , hivyo kinachomfanya kuzungumza ni kufanikisha maslahi yake na wenye uchunguzi na wananchi ni Serikali ya CCM.

Mwigulu alitoa kauli hiyo jana kijiji cha Ifunda katika Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa wakati akizindua kampeni za uchaguzi mdogo wa chama hicho.

Alisema kuwa CCM ndio yenye Ilani inayotekelezwa ambayo wananchi waliingia mkataba na chama hicho na kinachoendelea sasa ni utekelezaji wake.

"Tunahitaji maendeleo ya wananchi, tunazungumzia mambo ya msingi kwa ajili ya maisha ya wananchi wa Kalenga.Huyu Slaa anahangaika kwasababu anahitaji kulipwa mwisho wa mwezi.


"Huwa nashangaa watu wanaoshabikia Chadema, maana hawana wanachofanya zaidi ni kutengeneza makesi kila siku.Fuatilia wabunge wanaume tabu na wanawake nao tabu

Hata hivyo alisema uchaguzi huo si wa kupambanisha sera maana ni uchaguzi mdogo na kwamba uchaguzi mkuu mwaka 2010, tayari Watanzania waliingia mkataba na CCM.

Alisema kuwa ilani ya inayotekelezwa sasa ni ya CCM na upinzani hauna wanachotekeleza na hata kusimamia mgombea wao ni ushamba wa siasa.

"Kinachoendelea sasa ni kutekeleza maendeleo kupitia ilani ya CCM ambayo wanayoimiliki ni wa CCM.Hivyo hakuna sababu ya kupoteza muda,"alisema.

Alisema, umefika wakati kwa wananchi kumtuma kijana Godfrey Mgimwa ili akafanye kazi ya kuleta maendeleo yao na si kuchagua mbunge kwa sababu tu ya kuchagua.

Hata hivyo, alisema wananchi wanahitaji barabara, maji, umeme afya bora na huduma nyingine za msingi na mwenye kufanya kazi hiyo ni Serikali ya CCM, hivyo Mgimwa atasaidia katika kufanikisha hilo.

Aliongeza kazi ya upinzani ni kuomba jamii ipate matatizo ili wao wapate nafasi ya kusema .Haiwezekani kuwa na wanasiasa ambao kazi yao ni kuombea matatizo kila siku.

Mwigulu aliwaomba, wananchi kuacha ushabiki katika mambo ya maendeleo, hivyo hawatakiwi kufanya kosa kwa kumchagua mtu ambaye anatoka nje ya CCM.

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa Dk.Pindi Chana alisema kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na si maandamano.

Alisema anashangazwa na Chadema wanashindwa kutatua matatizo ya wananchi na badala yake wanazunguka hewani kwa helkopta wakati wananchi wapo chini.


Akizungumza katika mkutano huo, Chifu wa kabila la Wahehe,Abdul Mkwawa alisema kuwa kamwe hawezi kuwa Chadema na wanaozusha kuwa amemkaribisha Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Willibrod Slaa katika Jimbo la Kalenga wanajisumbua.

Alisema kuwa yeye ni kada wa CCM na ataendelea kuwa chama hicho na kwamba damu yake ni CCM.

"Siwezi kuwa Chadema wamezusha hadi kwenye mitandao eti nimemkaribisha Slaa Kalenga na wanadai mimi ni Chadema.Si kweli kwanza huyo Slaa wa kazi gani huku kwetu,"alisema.


Katibu CCM Wilaya

Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Hassan Mtaturu alisema kuwa wafuasi na wanachama wa Chadema wameanza kufanya vurugu lakini alionya kuwa hatawakuwa tayari kuvumilia.

Alisema kuwa watadhibiti na katika hilo hawatakuwa na huruma maana hawapo tayari kuonewa.

Alisema tayari wamepata majina ya vijana wa watu wa Chadema ambao wamebainika kufanya hujuma dhidi ya CCM ambao waliamua kuweka vibao vyenye misumari ili magari yaliyokuwa na wanachama wao yaharibikie.

Alitaja majina ya vijana waliotega misumari hiyo Issa Nyamahanga , Martin Nyangi na Rashid Dau wote wa Kijiji cha Wasa.

"Tumeanza uchunguzi , hivyo majina hayo tutakabidhi polisi ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa hatua.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Nsambatavangu alisema kuwa Chadema si chama ambacho kinastahili kupewa nafasi kwani kazi yake ni kuvuruga amani ya nchi.

Alisema kuwa kazi yao imekuwa kumtukana Rais , Serikali na CCM huku muda mwingi wakitumia kuhamasisha vurugu na maandamano.

Alisema wananchi wa Kalenga wasifanye makosa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kwa kuchagua mtu ambaye atakuwa ni wa vurugu kila kukicha na badala yake wachague CCM kwa maendeleo.

CCM YAPIGA KIPYENGA KALENGA; MWIGULU AMNADI MGOMBEA WA CCM ADAI DK. SLAA ANA MAPEPO ZAIDI YA SABA KICHWANI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, alipozindua r... [Read More]


 Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe wa Shinyanga mjini ambapo aliwasaidia kufungua SACCOS na kuwaongezea mtaji wa biashara yao.
 Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia jambo wakati wa hotuba ya Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
 Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakishangilia baada ya kuwezeshwa pesa kwenye mitaji ya biashara yao Mbunge wao Ndugu Stephen Masele,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.
Wakina Mama Lishe ambao wengi ni Wajane na Yatima wa Shinyanga mjini wakipeana mikono na  Mbunge wao Ndugu Stephen Masele baada ya kuwawezesha kuwa na SACCOSS pia kuwasaidia mtaji wa zaidi ya shilingi milioni nane,kwenye ukumbi wa NSSF CCM mkoa wa Shinyanga uliofanyika jana tarehe 26 Februari 2014.

MASELE AWAWEZESHA WAKINA MAMA LISHE SHINYANGA

 Mbunge wa Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Ndugu Stephen Masele akizungumza kwenye mkutano na wakina Mama na Baba Lishe... [Read More]

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini.
 Wakazi wa Shinyanga mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26 Februari 2014 kujiunga na CCM.
 Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
Sebastian Peter maarufu kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjni Shinyanga.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu  Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjni tarehe 26 Februari 2014.

NAPE : CCM IMEJENGWA KWA MISINGI IMARA

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi w... [Read More]