Google PlusRSS FeedEmail

WANANCHI WA KIJIJI CHA KIMOTORO WAKIMUOMBA KINANA AWASAIDIE KUTATUA TATIZO LAO

[Read More]



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kiteto mjini kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya na kuwaambia kuwa wilaya hito imekuwa na matatizo makubwa ya ardhi ambayo inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu sasa na si baadaye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vingi vya siasa vimekuwa kama wasanii wa kuigiza havina sera na vimekuwa vikiishi kutokana na matukio.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua Tshirt ya Chama kutoka kwa wakina Mama Wajasiriamali wanaouza nguo za CCM wilayani Kiteto.
Nguo za CCM zimekuwa zinauzwa katika kila kona nchini na kuvaliwa na watu wengi ambapo inakadiriwa CCM ina wanachama zaidi ya milioni sita nchi nzima na idadi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa Kimasai katika kijiji cha Kimotoro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanakijiji cha Irkiushbor wakati wa mapokezi mpakani mwa wilaya ya Simanjiro na Kiteto.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiruka juu kama Morani wa Kimasai alipotembelea kjiji cha Partimbo Eseki na kukagua miradi ya maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea shule ya msingi ya Laalakir .Shule hiyo ya msingi ni ya jamii ya wafugaji ambayo inafanya vizuri katika wilaya ya Kiteto.
Wanakijiji cha Kimotoro wilayani Simanjiro wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kumuomba awasaidie kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na hifadhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Partimbo Eseki baada ya kukagua miradi ya maji ambapo aliwataka wananchi hao kuitunza miradi hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wakina mama wa kijiji cha Partimbo kata ya Eseki .
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuwasaidia ng'ombe wa kijiji cha Partimbo kata ya Eseki wilayani Kiteto kunywa maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsaidia Mama wa Kimasai kumtwisha ndoo ya maji mara baada ya kuzindua huduma ya maji safi na salama, Kijiji cha Partimbo kata ya Eseki kina mradi wa maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo.

KINANA :MIGOGORO YA ARDHI KITETO ITATULIWE SASA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kiteto mjini kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya na kuwaambia kuwa wilaya h... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Kwaraa mjini Babati, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Kwaraa mjini Babati, leo
Kinana akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuhutubia mkutano wa hadhara leo

 Kinana akiwapungia mkono wananchi kwenye Uwanja wa Kwaraa, kuhutrubia mkutano wa hadhara . Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Bodaboda zikitoka Ofisi ya CCM wilaya ya Babati kuongoza msafara kwenda uwanjani. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYANI BABATI KWA MKUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA, KESHIO KUANZA KITETO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Kwaraa mjini Babati, leo  Katibu wa NEC, Itikadi na Uen... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya Maji mkazi wa Kijiji cha Himiti Kata ya Bonga, wilaya ya Babati mjini, Zena Rashid, bada ya kuzindua mradi wa maji wa kata hiyo leo akiwa katika katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya hiyo ya Babati mjini mkoani Manyara. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na anayeshangilia kushoto ni Mbunge wa Hanag, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezsshaji, Dk. Mary Nagu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya Maji mkazi wa Kijiji cha Himiti Kata ya Bonga, wilaya ya Babati mjini, Zena Rashid, bada ya kuzindua mradi wa maji wa kata hiyo leo akiwa katika katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya hiyo ya Babati mjini mkoani Manyara. Kushoto ni Mbunge wa Hanag, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezsshaji, Dk. Mary Nagu.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kushoto), akisalimia watumishi wa hospitali ya wilaya ya Babati, alipofika kwenye hospitali hiyo leo, akiwa katika ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi mkoani Manyara.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akipata maelezo kuhusu huduma za maabara katika hospitali hiyo ya wilaya ya Babati.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya Malangi kata ya Maisaka, Babati Mjini leo
 6. Nape akipanda mti Zahanati ya Malagi
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akikagua bweni alipotembelea shule ya sekondari ya Frederick Sumaye, Kata ya Singe, Babati mjini leo
 Kinana akikagua ujenzi wa ujenzi wa ukumbi kwenye shule hiyo leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa ngoma kuanza ziara ya siku moja katika wilaya ya Babati mjini leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

KINANA AINGIA BABATI MJINI LEO, KUUNGUMA UWANJA WA KWARAA JIONI HII

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya Maji mkazi wa Kijiji cha Himiti Kata ya Bonga, wilaya ya Babati mjini, Zena Rashi... [Read More]

NAPE ALIPOHUTUBIA MBULU (VIDEO)

[Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wamasai katika kijiji cha Ayamango (Gallapo) ambapo alikuwa na kazi ya kufungua shina la Wakereketwa Wajasiriamali na kuhutubia mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha bendera ya CCM baada ya kuzindua shina la Wakereketwa Wajasiriamali la Ayamango.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akipokea maneno ya usia baada ya kupewa heshima ya Mzee wa kabila la Wagoroa
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akipewa heshima ya kuwa kijana wa kabila la Wagoroa na Wazee wa kimila wa kijiji cha Ayamango.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ayamango ambapo aliwaambia CCM imesimama imara kwa sera na mipango bora .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ayamango na kuwaambia kazi kubwa ni kuimarisha chama ili kumuenzi Baba wa Taifa.Kinana pia alisema tatizo kubwa la migogoro ya ardhi wilayani Babati ni viongozi wa kijiji kuwa si waaminifu kwani wanauza ardhi hovyo bila kufuata taratibu wala kuwashirikisha wananchi wa kijiji husika.
 Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon akihutubia wakazi wa kijiji cha Ayamango
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi Computer kwa Mratibu wa Kituo Cha Mafunzo ya Ualimu Ndugu Andrea F Mzava ,Computer hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Mamire ambacho kitakuwa chuo cha kwanza cha Ualimu mkoani Manyara ambacho ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 470.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti nje ya majengo ya Chuo cha Ualimu Mamire ambacho kitakuwa chuo cha kwanza cha Ualimu mkoani Manyara ambacho ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 470, Chuo hiki kimejengwa kwa udhamini wa Shirikia lisilo la Kiserikali la So They Can pamoja na Nguvu za wananchi ambao wamechangia milioni 25
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wengine i wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Walimu wa Chuo cha Ualimu Mamire ambacho kitakuwa chuo cha kwanza cha Ualimu mkoani Manyara ambacho ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 470.

 Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Mamire likiwa kwenye hatua za mwisho kukamilika.

KINANA : VIONGOZI WA VIJIJI WAACHE KUUZA ARDHI BILA KUWASHIRIKISHA WANAKIJIJI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wamasai katika kijiji cha Ayamango (Gallapo) ambapo alikuwa na kazi ya kufungu... [Read More]


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika Kata ya Magara wilaya ya Babati Vijijini.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa chama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amezungukwa na wakazi wa Kata ya Magara wilayani Babati Vijijini waliojitokeza kwa wingi kuwapokea mara baada ya kuwasili wilayani hapo .
 Wananchi wa Kata ya Magara wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya Magara kabla ya kukagua mradi wa ujenzi  wa wodi ya kituo cha afya cha Mama na Mtoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya kituo cha afya cha mama na mtoto.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa chama.
 Wananchi wa Kijiji cha Magara wakionyesha bango la kuomba msaada wa kusaidiwa kujengwa kwa daraja katika mto Mangara.
 Mto Magara ambao wananchi wanaomba daraja lijengwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Magugu ambapo aliwapa usia vijana wenzake kwa kuwaambia Vijana wachape kazi na waachane na talalila za wanasiasa njaa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa  Magugu na kuwaambia viongozi wengi wa vijiji wamekuwa wakiingia mikataba bila kuwashirikisha wananchi hivyo kusababisha migogoro mikubwa ya ardhi na amewataka wananchi kuchagua viongozi makini,Katibu Mkuu wa CCM ameshtushwa na baadhi ya watu kumiliki sehemu kubwa ya ardhi na kuwakodishia wananchi kwa ajili ya kilimo cha mpunga.

KINANA AWASILI WILAYA YA BABATI VIJIJINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon mara baada ya kuwasili ... [Read More]

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali.Katibu Mkuu alisisitiza serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote waliojichukulia mali ya serikali bila utaratibu hasa nyumba za madaktari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakijiji cha Bashei ambao walimueleza kuwa wanalima sana kitunguu saumu lakini soko si zuri na kumuomba awasaidie kutafuta soko la kdumu, tatizo jingine ni ucheleweshaji wa kujenga bwawa la maji, Katika ziara hizi za Katibu Mkuu wananchi wamekuwa na imani kubwa na CCM kwa ushirikiano wanaoupata kwani majibu ya maswali yao yanakuwa ya kuridhisha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji ,pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.
Diwani wa Kata ya Eshkesh kutoka chama cha CUF Ndugu Naftal Z Kihandu akishukuru kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kuwasikiliza wananchi wa kata yake na kufungua njia kwa kuchangia mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Hydom na kuwaambia wapunguze muda na mambo ya siasa ,watumie muda mwingi kushikama na kujenga maendeleo yao.
 Wananchi wa Hydom wakinyoosha mikono yao kuunga mkono jitihada za CCM katika kuleta maendeleo nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya Chadema iliyorudishwa kwake na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Victoria Mshanga ambaye amjiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Hydom.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga picha ya wanakijiji cha Eshkesh pamoja na Richard Mwaikenda maarufu kama Kamanda wa Matukio,Wananchi wa Eshkesh wanashida ya maji na Zahanati ambapo maji yatapatikana karibuni kutokana na mipango ya halmashauri lakini zahanati pia itaanza kujengwa baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuhamasisha kwa kuanza kuwachangia mabati na Simenti na halmashauri na wanakijiji hao wataongezea nguvu kukamilisha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi na wanafunzi wa uuguzi wa Hospitali ya Hydom .Katibu Mkuu aliupongeza Uongozi pamoja na Watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati wa ujenzi wa daraja la Qorong'aida linalounganisha Kilimapunda na Kidarafa na linategemewa kugharimu zaidi ya bilioni moja.

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA MBULU KWA MAFANIKIO KUHUTUBIA BABATI LEO JIONI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo ... [Read More]