Google PlusRSS FeedEmail
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akifuturu pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.Amani Kaborou,Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Mohamed Nyawenga na Mbunge wa Manyovu Albert Obama.
 Baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na wakazi wa Kigoma mjini wakifuturu leo 31Julai 2013 katika ofisi za CCM wilaya ya Kigoma Mjini.
 Baadhi ya Mabalozi na wakazi wa Kigoma mjini wakipata futari
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache baada ya kufuturu na Mabalozi wa nyumba 10 ambapo alisisitiza Watanzania kutunza amani waliokuwa nayo.
 Sheikh Mustafa Halfan Kiumbe akisema maneno machache kabla ya kumkaribisha Sheikh Mkuu wa Kigoma
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akishiriki dua iliyoongozwa na Sheikh Hassan Idd Kiburwa leo baada ya kufuturu na mabalozi wa nyumba 10 wa Kigoma mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya mabalozi wa nyumba 10 kutoka Kigoma mjini ambao alifuturu nao pamoja.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji kutoka wilaya ya Kigoma mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufturu .

NAPE AFUTURU NA MABALOZI WA NYUMBA KUMI KIGOMA MJINI

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akifuturu pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.Amani Kaborou,Katibu wa CCM Mkoa wa ... [Read More]

NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada wa sheria ulioanzisha kodi mpya ya tozo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imesema uamuzi huo umedhihirisha kwamba serikali inawasikiliza na kuwajali wananchi wake.

Akiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari leo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amekaririwa akisema kwamba mjadala kuhusu muswada wa sheria ya kodi hiyo ya tozo hiyo utafanyika wakati wa mkutano wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Baada ya kupitishwa na bunge Juni mwaka huu, na utekelezwaji wake kuanza rasmi Julai mwaka huu, CCM ilikuwa miongoni mwa wadau waliopinga vikali kuanzishwa kwa kodi ya tozo hiyo, ikieleza kwamba ni mzigo na usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa simu ambao wengi matumizi yao ni ya kawaida.

Katika taarifa hiyo, CCM imesema kwa kuwa wabunge wengi ni wa chama hicho, watumie fursa hiyo kuhakikisha sheria ya tozo hiyo inaondolewa na wakati huohuo watumie uwezo wao wote kuhakikisha wanaishauri serikali vizuri kupata njia mbadala itakayotumika kuziba nafasi itakayokuwa imeachwa kwa kuondolewa tozo hiyo.

"Kimsingi hatua hii imetupa faraja na hivyo CCM inaipongeza Serikali kwa kuamua kusitisha sheria ya kodi ya tozo hiyo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu kwa kuwa ingesababisha usumbufu na adha isiyo ya lazima kwa wananchi", imesema CCM katika sehemu ya taarifa yake.

CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUREJESHA BUNGENI MUSWADA SHERIA YA KODI YA TOZO YA LAINI ZA SIMU

NA MWANDISHI WETU CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada wa ... [Read More]

WAZEE WA KIMILA WAMPONGEZA MBUNGE NYAMBARI NYANGWINE

NYAMBARI NYANGINE TARIME, Tanzania SAISA chafu zinazodaiwa kuanza kushika kasi katika majimbo ya Tarime na Rorya, zimewaibua wanasiasa wakon... [Read More]

  Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
 Kwa heshima kubwa Rais Jakaya Kikwete akivishwa uchifu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE ATAWAZWA OMUKUMA (CHIFU) WA MISSENYI, AHITIMISHA ZIARA YA KAGERA

    Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongoz... [Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali wa mkoa wa Kagera ambao waliongozana naye katika ziara yake ya siku sita mkoani humo. Rais Kikwete amewapongeza wanahabari hao na kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri ya kuufahamisha umma kila hatua ya ziara yake kwa ufasaha na weledi.
Wanahabari hao pia wamefurahi kuona kwamba Rais hakuja na jopo la wanahabari kutoka Dar es salaam kwa kuwaamini wao, hatua anbayo  wamesema imewapa faraja na furaha kubwa na  kujiamini zaidi.
PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA KYAKA-BUGENE, APONGEZA WANAHABARI WA KAGERA KWA KAZI NZURI

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi,... [Read More]

CCM YAKOMALIA SERIKALI MBILI

CCM YAKOMALIA SERIKALI MBILI sehemu ya pili. [Read More]

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.
 Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15 zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).
 Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China).
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen  Clark Mtendaji Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na menejimenti ya shirika hilo.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa UN Women Bi. Lakshmi Puri (Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Ludovick S. L. Utouh mara baada ya kikao cha pamoja cha kilichofanyika makao makuu ya Ofisi, mjini New York Marekani.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tuvako Manongi (Watatu Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mara baada ya kikao kazi kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania, New York Marekani
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi (Katikati) na Bw. Justin Kisoka mmoja kati ya Maafisa Balozi wa Umoja wa Mataifa, nchini Marekani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Modest Mero (Watatu Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowatembelea, UN Plaza, New York Marekani. IMETAYARISHWA NA theNkoromo Blog

CAG WA TANZANIA KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA UMOJA WA MATAIFA, NEW YORK

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.... [Read More]

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira akiwa na Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacqueline Liana alipokagua maendeleo ya  katika shule moja akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza tarahe 24. 7. 2013
 Waziri na Mkuu wa wilaya, wakishuhudia mmoja wa wananfunzi wa shule hiyo alipokuwa akiandika ubaoni PICHA ZAIDI ZA ZIARA HIYO>> BOFYA HAPA

ZIARA YA WAZIRI WASSIRA WILAYANI MAGU YAFANA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira akiwa na Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacqueline Liana alipokagua maendeleo ya ... [Read More]

The EAC Brand 2013 survey team embarked on a week-long mission to Uganda on how citizens perceive the regional integration activities, programme and how much they understand of the Community. The survey will be undertaken in all Partner States between 16 July and 27 August. The first two teams set out for Uganda and Burundi. In the picture, the Brand Survey Team poses for a group picture with acting Uganda's Permanent Secretary Steven Niyonzima(with tie) and on his right is the EAC Brand Team leader, Sukhdev Chhatbar., after paying a courtesy call at the Uganda EAC Ministry in Kampala.

EAC BRAND SURVEY TEAM IN UGANDA

The EAC Brand 2013 survey team embarked on a week-long mission to Uganda on how citizens perceive the regional integration activities, progr... [Read More]

WANANCHI WA MAKETE WAKIONGEA MASUALA MUHIMU YA WILAYA YAO

[Read More]

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013. Aliyeshika utepe ni Jaji Mkuu, Othman Chande
 Rais Kikwete akiwa katika moja ya vyumba vya mahakama hiyo
 Rais Kikwete akifuatana na Jaji Mkuu wakati akikagua jengo la mahakama hiyo
 Jaji Mkuu Othman Chande akimpa maelezo Rais Kikwete wakati wakiwa kwenye jengo la mahakama hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa mahakama waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo la mahakama
Baadhi ya watu waliofika kwenye sherehe za uzinduzi wa jengo hilo. Picha na Ikulu

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013  Rais Jakaya Mrisho Kikw... [Read More]

RORYA,Tanzania
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tai kupitia Chama hicho, Masirori Kyorang  amefikishwa Katika Mahakama ya Mwanzo Shirati kujibu mashitaka ya ugoni.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, Kyorang anadaiwa kushikwa ugoni na mke wa mlinzi wa Mbunge wa Jimbo la Rorya wakiwa gesti ya Triple Kabwana katika mji mdogo wa  Shirati, suiku wa kuamkia jana.

Akisomewa Mashitaka hayo  jana Julai 24, na Mwendesha Mashitaka wa Polisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Shirati Dock Nyatega , ambapo ilidaiwa kuwa mheshimiwa Masirori alikamatwa  mida ya saa 3 usiku, katika chumbani akiwa na mke wa mlinzi huyo wa Mbunge wa Jimbo la Rorya aliyejulikana kwa jina Pendo Omolo.

Mtuhumiwa Masirori alikana Mashitaka yake na kupata Dhamana hadi kesi yake itakapotajwa tena Julai  29 , ambapo Mke huyo Pendo amekwenda Nyumbanio kwao hadi Shauri hilo litakapoanza kusikilizwa na kubaini Ukweli wake baada ya Ushahidi kutolewa Mahakamani alisikika akisema Hakimu Nyatega .
 Habari hii imeandikwa na Samson Chacha, 0788312145, 0762219255

DIWANI WA CHADEMA ATINGA MAHAKANIKUJIBU SHITAKA LA UGONI

RORYA,Tanzania Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tai kup... [Read More]

WASHINGTON, DC, Julai 22, 2013 – Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.

Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni  202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.
Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika,
Ripoti  hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia  47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku..

“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika.
“Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”

Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia.
Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..

Mpango wa kuleta mabadiliko

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::

· Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.
· Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .
· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa  usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.
·
Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .

Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji



BENKI YA DUNIA YAIPA CHANGAMOTO AFRIKA KUBORESHA MATUMIZI YA ARDHI KUONDOA UMASIKINI

WASHINGTON, DC, Julai 22, 2013  – Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza... [Read More]

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha. Picha na OMR

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi 'Physical Sciences' (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza, baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013. Picha na OMR
 Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI, CHANGAMOTO ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA MIJI BARANI AFRIKA, JIJINI ARUSHA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi  wa Mkutano wa Kimataifa k... [Read More]

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kushoto) akishiriki swala ya Magharibi na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wa Mkoani Arusha, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza baadhi ya wananchi wa mkoani Arusha kuchukua futari, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiagana na wageni wao baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR




MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WANANCHI MKOANI ARUSHA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kushoto) akishiriki  swala ya Magharibi na b... [Read More]

Makhtar Diop is the World Bank Group’s Vice President for Africa 

How Africa Can Transform Land Tenure, Revolutionize Agriculture, and End Poverty
                                                     A Ten Step Plan for Change
WASHINGTON, DC, July 22, 2013 – Sub-Saharan Africa is home to nearly half of the world’s usable, uncultivated land but so far the continent has not been able to develop these unused tracts, estimated at more than 202 million hectares, to dramatically reduce poverty and boost growth, jobs, and shared prosperity.  

According to a new World Bank report, “Securing Africa’s Land for Shared Prosperity,” released today, African countries and their communities could effectively end ‘land grabs,’ grow significantly more food across the region, and transform their development prospects if they can modernize the complex governance procedures that govern land ownership and management over the next decade. Africa has the highest poverty rate in the world with 47.5 percent of the population living below US $1.25 a day.

“Despite abundant land and mineral wealth, Africa remains poor,” says Makhtar Diop, World Bank Vice President for Africa. “Improving land governance is vital for achieving rapid economic growth and translating it into significantly less poverty and more opportunity for Africans, including women who make up 70 percent of Africa’s farmers yet are locked out of land ownership due to customary laws. The status quo is unacceptable and must change so that all Africans can benefit from their land.”

The report notes that more than 90 percent of Africa’s rural land is undocumented, making it highly vulnerable to land grabbing and expropriation with poor compensation. However based on encouraging evidence from country pilots in African countries such as Ghana, Malawi, Mozambique, Tanzania, and Uganda, Securing Africa’s Land for Shared Prosperity suggests an action plan that could help revolutionize agricultural production, end land grabbing, and eradicate extreme poverty in Africa. 

An action plan for change 

The report suggests that Africa could finally realize the vast development promise of its land over the course of the next decade by: 

· Championing reforms and investments to document all communal lands and prime lands that are individually owned 
· Regularizing tenure rights of squatters on public land in urban slums that are home to 60 percent of urban dwellers in Africa. 
· Tackling the weak governance and corruption endemic to the land governance system in many African countries which often favor the status quo and harm the interests of poor people.
· Generating the political will of African governments to mobilize behind these land reforms and attract the political and financial buy-in of the international development community.

The new report says it would cost African countries and their development partners, including the private sector, US $4.5 billion spread over 10 years to scale up these policy reforms and investments.



“Improving the performance and productivity of Africa’s agricultural sector is vital for broad-based growth, more jobs, investment, and substantially less poverty,” says Jamal Saghir, World Bank Director for Sustainable Development in Africa. “Land governance is a proven pathway to achieving transformational change and impact that will help secure Africa’s future for the benefit of all its families.” 

Opportunities for change have never been better 

Surging food commodity prices and foreign direct investment have increased the potential return on investing in effective land administration through higher agricultural yields and better market access and prices. Most African countries already have the basic land laws in place that recognize customary land rights and gender equality which are essential to reinforce needed reforms. 

In addition, new satellite and information technologies can greatly reduce the cost of land administration. A growing number of African countries are now using these technologies to reduce the costs of surveying and mapping land and computerizing their land registries to improve efficiency and reduce corruption.  
Some 26 African countries have established at least one continuously operating reference station (CORS) and about 50 CORS are contributing data to the African geodetic reference system, which, once completed, will provide a uniform coordinate reference system across the continent.  

Challenges remain

With only 10 percent of Africa’s rural land registered, inefficient land administration means that it takes twice as long and costs twice as much to transfer land compared to industrialized countries, and weak governance is the leading cause for corruption in the land sector. 

The report warns that “…unless communal and individual land rights are registered and land governance is improved, the recent surge in foreign direct investment in Africa will not generate shared and sustained growth, as disruptions will likely arise from the dispossession of local communities, and investors’ deals will face severe uncertainty or collapse, as witnessed in Madagascar in 2009.”   

The report notes successful examples of how African governments have undertaken tough reforms, enacted laws and implemented progressive land policies that have benefited poor communities. Highlighting the need for greater capacity, the report finds that Ghana, Kenya and Uganda each have fewer than 10 professional land surveyors per one million people, compared to 197 in Malaysia and 150 in Sri Lanka.  Of Kenya’s 206 registered land surveyors, only 85 were found to be practicing.  The report points to the futility of building capacity without making complementary investments in land administration. 

“Land governance issues need to be front and center in Africa to maintain and better its surging growth and achieve its development promise,” says Frank Byamugisha, author of the report and Lead Land Specialist in the World Bank’s Africa Region. “Our findings provide a useful, policy-oriented roadmap for African countries and communities to secure their own land for building shared prosperity.”

As of 2002, at least 20 countries in Sub-Saharan Africa had recognized customary land rights and gender equality, a number that has nearly doubled. The African Union Commission has developed a land policy framework backed by a five year strategic plan for implementation to 2016.  

How the World Bank Group helps to improve land governance 

As this report points out, Africa is home to the largest amount of land that can be brought under the plow and securing access to land is critical for millions of its people. Investing in improved land governance then offers a win-win opportunity for governments, investors and the landless.

The World Bank Group supports and endorses the Voluntary Guidelines on the Responsible Governance of Tenure of Land, Fisheries and Forests in the Context of National Food Security (“the VGs”). These guidelines are a major international instrument to inform specific policy reforms, including our own procedures and guidance to clients. The World Bank Group is already working with countries to implement the VGs, with a special focus on Africa.  

The World Bank Group and its partners have also developed the Land Governance Assessment Framework (LGAF) as a diagnostic tool to assess the status of land governance at the country level. LGAF assessments have been carried out—or are underway—in 18 countries, 10 of them in Africa. The World Bank Group now support 24  projects on land administration amounting to US $928 million – likely the largest number of interventions on the governance of land tenure of any international development agency.  

HOW AFRICA CAN TRANSFORM LAND TENURE, REVOLUTIONIZE AGRICULTURE, AND END POVERTY

Makhtar Diop is the World Bank Group’s Vice President for Africa  How Africa Can Transform Land Tenure, Revolutionize Agriculture, and End P... [Read More]

  Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar. Picha na OMR


 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakiwafariji wafiwa baada ya kutoka heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar. Picha na OMR

 Mkuu wa Majeshi David Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.

 Rais Jakaya, akizungumza wakati wa zoezi hilo.

  Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Picha na OMR

 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam. Picha na OMR

Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.

ASKARI WALIOKUFA DARFUR WAAGWA LEO DAR, RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUAGA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO

   Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi  la Ulinzi la Wananchi ... [Read More]