NA BASHIR NKOROMO
SERIKALI inapata mapato ya takribani Sh. milioni 3.5 kwa siku kutokana na usafiri wa treni katika jiji la Dares Salaam.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) Dk.Zacharia Mganilwa wakati akimkabidhi tuzo Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha sekta ya reli nchini kwa niaba ya kampuni ya Mwandi Tanzania kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Aidha Dk. Mganilwa tuzo pia imetolewa kutokana na Waziri Mwakyembe ameweza kufufua na kuweka kwenye fikra Reli ya Musoma ya kwenda Arusha na Reli Tanga.
Akizungumza katika makadhiano hayo,Dk.Mganilwa amesema kuwa tuzo hiyo ilizingatia vigezo vyote muhimu vya kumpata mshindi kwa kuzingatia mchango wa muhusika katika sekta ya hiyo ,mtazamo wa wananchi kwa mtu husika na msimamo binafsi wa mtu husika kwenye uboreshaji huo.
“Ninyi ni mashuhuda wa mapinduzi ya usafiri wa treni za abiria jijini Dar es Salaam unaowanufaisha zaidi ya abiria 14,000 kila siku na ikumbukwe kwamba wazo la kuanzishwa usafiri huo lilikuwepo lakini Mheshimiwa Waziri ndiye aliyekuja kufanya ndoto hiyo kuwa uhalisia”alisema Dkt.Mganilwa.
Tuzo hiyo imepatikana baada ya kushindanishwa kwa majina matatu ya watu ambao wana mchango mkubwa kwenye maendeleo na mapinduzi ya reli Tanzania kwa kurejea kila mmoja katika kipindi chake cha na kile alichokifanya.
Aidha ameiomba Serikali kupitia wizara ya hiyo kuanzisha mfuko wa miundo mbinu kwa fedha zitakazo kuwa zinapatikana katika usafirshaji ili kuweza kuendelea kuboresha suala hilo na kukuza uchumi wa nchi yetu pamoja na kuleta maendeleo.
Naye Waziri Mwakyembe ameishukuru kampuni hiyo kwa kuuona mchango wake katika jamii na kuweza kumpatia tuzo, ambayo ni motisha itakayo muongezea juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo kupitia sekta ya hiyo.
“Kwa niaba ya TRL, RHACO na wafanyakazi wote wa wizara ya Uchukuzi napenda kuishukuru kampuni ya Mwandi Tanzania kwa kuuona mchango wangu katika sekta ya usafiri wa treni bado tunaendelea kuweka mipango madhubuti kuboresha usafiri wa treni nchini na Afrika Mashariki kiujumla”alisema Dkt.Mwakyembe.
Watu wengine walioshiriki katika ushindani wa tuzo hiyo, Injia Festo Mwanyika na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Reli Tanzania na Linford Mboma kutoka Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).