RORYA,Tanzania
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tai kupitia Chama hicho, Masirori Kyorang amefikishwa Katika Mahakama ya Mwanzo Shirati kujibu mashitaka ya ugoni.
Kwa mujibu wa kesi hiyo, Kyorang anadaiwa kushikwa ugoni na mke wa mlinzi wa Mbunge wa Jimbo la Rorya wakiwa gesti ya Triple Kabwana katika mji mdogo wa Shirati, suiku wa kuamkia jana.
Akisomewa Mashitaka hayo jana Julai 24, na Mwendesha Mashitaka wa Polisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Shirati Dock Nyatega , ambapo ilidaiwa kuwa mheshimiwa Masirori alikamatwa mida ya saa 3 usiku, katika chumbani akiwa na mke wa mlinzi huyo wa Mbunge wa Jimbo la Rorya aliyejulikana kwa jina Pendo Omolo.
Mtuhumiwa Masirori alikana Mashitaka yake na kupata Dhamana hadi kesi yake itakapotajwa tena Julai 29 , ambapo Mke huyo Pendo amekwenda Nyumbanio kwao hadi Shauri hilo litakapoanza kusikilizwa na kubaini Ukweli wake baada ya Ushahidi kutolewa Mahakamani alisikika akisema Hakimu Nyatega .
Habari hii imeandikwa na Samson Chacha, 0788312145, 0762219255