Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema, posho ya dola 1.28 kwa siku wanayolipwa walinzi wa amani wanaohudumu katika Misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, hailingani na mazingira magumu na hatari ya utekelezaji wa mamlaka wanayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa.
Na kwa sababu hiyo ,na kwa zingatia hali halisi, Tanzania imesisiza kwamba, wakati umefika sasa wa kuangalia upya posho hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 20.
Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa mataifa, ametoa rai hiyo mwanzo mwa mkutano wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Ulinzi wa Amani maarufu kama C-34.
Kamati hii ambayo wajumbe wake ni kutoka nchi zinazochangia walinzi wa Amani katika misheni mbalimbali za kulinda amani, imeanza mkutano wake wa mwezi mmoja hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wajumbe watajadili mambo yote yanayohusu sera za ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Balozi Manongi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Kamati ilikuwa inaanza mkutano wake, wakati ambapo , operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za malipo duni.
“ Tunaposhindwa kukubaliana kujadili hoja ya kuongeza kiwango cha posho ya kila siku kwa walinzi wa amani, posho ambayo imebaki dola 1.28 kwa zaidi ya miaka 20, siyo tu kwamba tumewaangusha walinzi wa amani, bali pia tunawavunja moyo na kuwakatisha tamaa katika utekelezaji wa majukumu yao”. akasisitiza Balozi Manongi.
Akasema waeleza wajumbe licha ya malipo duni na mazingira magumu, walinzi hao wanajitolea uhai wao kwaajili ya watu wengine na kwamba,kutokana umuhimu wao , Umoja wa Mataifa umejikuta ukilazimika kuwapeleka katika Misheni ambazo ama hakuna amani ya kulinda au mahali ambako kuna vikundi vingi vyenye silaha vinavyokinzana.
“Hii ndiyo hali halisi inayozikabili Misheni zetu zote katika utekelezi wa mamlaka tunazokabidhiwa na Umoja wa Mataifa. Inasikitisha na kukatisha tamaa pale baadhi yetu tunaposisitiza kwamba Misheni mpya inayoundwa au kuongezewa mamlaka itekeleze mamlaka hayo kwa kuzingatia rasilimali zilizopo, ili hali tunafahamu wazi kwamba rasilimali zinazozungumzwa ama hazipo au hazikidhi hali halisi ya Misheni hizo”. Akabainisha Balozi Manongi.
Na kuongeza. “Ni vema tukaunganisha nguvu zetu kukabiliana na changamoto hizi na nyingine nyingi ili walinzi wa amani ambao wanategemewa sana waweze kusaidia katika ulinzi wa amani kwa raia wasiokuwa na hatia, lakini pia kujihakikishia usalama wao wenyewe.
Akaeleza kwamba ni matumaini ya Tanzania kuwa hoja ya kuongezwa kwa posho hiyo pamoja na nyongeza ya malipo ya vifaa itapewa umuhimu na kujadiliwa ipasavyo katika mkutano ujao wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Utawala na Bajeti ya Umoja wa Mataifa.
Pamoja na changamoto hizo, Muwakilishi huyo wa Tanzania, ameuhakikishia Umoja wa Mataifa kwamba, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwajibika kwa kushiriki katika operesheni za ulinzi wa Amani kwa mujibu wa Mamlaka inayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa.
“ Tumedhamiria na tunajivunia ushiriki wetu wa ulinzi wa Amani katika maeneo mbalimbali ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako tunashiriki kupitia Misheni ya Kulinda Amani katika DRC ( MONUSCO). Misheni ambayo ndani yake kuna Force Intervention Brigade ( FIB)”.
Vile vile akabainisha kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa, kuhusu Ulinzi, Usalama na Ushirikiano wa Ki- maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu.
Akizungumzia zaidi kuhusu Misheni ya MONUSCO na mchango wake katika usimamizi wa amani katika DRC.
Balozi Tuvako Manongi amesema, Tanzania inaamini kwamba utendaji kazi wa Misheni hiyo unasimama katika misingi ya Misheni Moja, Jeshi Moja, Nguvu Moja ya Mamlaka, kuwa ndiyo mweleko sahihi na wenye tija katika ngazi zote kiutendaji.
Misheni ya MONUSCO inaundwa na walinzi wa Amani kwa upande mmoja kutoka Pakistani, India na Bangladeshi pamoja na Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi kupitia FIB.
Aidha, Muwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, amezitaka Mamlaka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutumia mafanikio yaliyopatikana hivi karibuni, kuimarisha taasisi zake za kisiasa, kiulinzi , kiuchumi pamoja na kuongeza kasi ya majadiliano na maridhiano. Baadhi ya Waambata wa Kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao Katika Umoja wa Mataifa, wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Kulinda Amani. Katika Mkutano huu wajumbe ambazo ni kutoka nchi ambazo zinachangia walinzi wa amani watajadili sera zote zinazohusu ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2014
(556)
-
▼
February
(88)
- MWIGULU, MGOMBEA WA CCM KALENGA, WASHIRIKI MAZISHI...
- PRESIDENT KIKWETE RECEIVES A REPORT ON STATE OF AF...
- DC HANANG AKUTANISHA VIJANA 316 KUANZISHA SACCOS
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA ...
- MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM K...
- RAIS KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA KUHAKIKI TAKWIMU ZA...
- TAARIFA KUTOKA IDARA YA HALI YA HEWA
- RAIS KIKWETE AUNGANA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU KUTO...
- CCM YAPIGA KIPYENGA KALENGA; MWIGULU AMNADI MGOMBE...
- MASELE AWAWEZESHA WAKINA MAMA LISHE SHINYANGA
- NAPE : CCM IMEJENGWA KWA MISINGI IMARA
- TANZANIA YASISITIZA NYONGEZA YA POSHO KWA WALINZI...
- MTEMVU ACHANGIA VIKOBA TEMEKE
- MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA ...
- WAZIRI NYALANDU AWANG'OA VIGOGO IDARA YA WANYAMAPORI
- WAMILIKI WA MAENEO YA BIASHARA WAOMBWA KUTOA KIPAU...
- WANAFUNZI WA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII WATEMBELEA ...
- AFTER PARTY YA LADY IN RED ILIVYOFANA
- RAIS JAKAYA KIKWETE AMLILIA BALOZI FULGENCE KAZAUR...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ...
- SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM MAREKANI KUFANYIKA LEO ...
- MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATOKA
- SALMA MOSHA: BALOZI ZINA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA NNE...
- ZIARA YA MZEE MANGULA CHINA
- MEMBE: SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KUSIMAMIA MASUA...
- PSPF YAWAPIGA MSASA WANAHABARI DAR, WENGI WAVUTIWA...
- TAHADHARI YA MVUA
- NAPE: NDOTO ZANGU KABLA YA KUWA MWANASIASA NILITAM...
- MSAADA TOKA UINGEREZA KWA MAMA WA MAPACHA WANNE WA...
- VIDEO YA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI NAPE NNAUYE A...
- WADAU WAOMBWA KUDHAMINI MAONYESHO YA KAZI ZA VIJAN...
- CCM YATOA ADHABU YA ONYO KALI KWA WANAOJITANGAZA K...
- CCM KUBAKI NA MUUNDO WA SERIKALI MBILI
- KINANA ASUKIWA MIKAKATI YA KUMHUJUMU KISIASA
- HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA YAENDELEA LEO
- MEMBE AHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI
- JK AWAPA RUNGU CCM, AWATAKA KUACHA UNYONGE DHIDI Y...
- JAKAYA AZINDUA SERA YA MTANDAO WA VIKUNDI VYA MAAD...
- SABMILLER AFRICA/TBL ZAISADIA ACE AFRICA KUBORESHA...
- RAIS KIKWETE ALIPOREJE NYUMBANI JANA AKITOKEA LONDON
- KONGAMANO LA UWEKEZAJI KANDA YA ZIWA LAENDELEA LEO...
- TIC YASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI N...
- RWANDA AIR YATOA SEMINA KWA MAWAKALA WA MASHIRIKA ...
- KAMATI YA MAADILI YAMHOJI WASSIRA MJINI DODOMA
- JANUARY MAKAMBA AHOJIWA KAMATI YA MAADILI
- WATATU WAHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UHA...
- JIMBO LA TEMEKE CCM LAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI, ...
- RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI AIFAGILIA TAA...
- WAANDISHI WA HABARI WA REDIO ZA JAMII WAASWA KUZIN...
- TBL YAKABIDHI WODI YA WAZAZI NA MIUNDOMBINU YA MAJ...
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA TAFA...
- TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA
- CCM YATEUA MGOMBEA WAKE UCHGAUZI MDOGO JIMBO LA K...
- TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA UCHAGUZ...
- KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA CHINI YA MWENYEKITI WAK...
- MAANDALIZI BUNGE LA KATIBA
- CCM YATOA SHUKRANI KWA WANANCHI KUIMWAGA CHADEMA K...
- MADABIDA KIZIMBANI AKIDAIWA KUSAMBAZA DAWA BANDIA ...
- RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE PAT...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MJUMBE WA EU, NA SHIRIKA L...
- KONGAMANO LA 9 LA CTO LA MABADILIKO YA MFUMO WA U...
- CCM KIDEDEA, YAIACHA MBALI CHADEMA UCHAGUZI MDOGO ...
- MTEMVU AZUNGUMZA NA HALMASHAURI KUU YA CCM KATA YA...
- YANGA YAINYUKA KOMORIZINE SPORTS SABA BILA
- TAARIFA RASMI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MA...
- TASWIRA YA MKUTANO WA NANE WA MWISHO KUHUSU MAENDE...
- NAPE:KUZUIA WATU KUPIGA KURA NI KUIHUJUMU DEMOKRASIA
- NAPE ALAANI VITENDO VYA KINYAMA VINAVYOFANYWA NA U...
- KIKAO MAALUMU CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA VYENYE...
- ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN NCHINI INDIA
- JUMA NKAMIA; KUTOKA UTANGAZAJI HADI NAIBU WAZIRI
- MAOFISA HABARI NA MAWASILIANO WATOA MSAADA KWA WAZ...
- MWAKILISHI MPYA WA KIEMBESAMAKI AAPISHWA
- RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE APOKEA HUNDI YA SHILING...
- USIKU WA WASANII NA WAANDISHI WA HABARI WAFANA
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKUU WA JESHI...
- TANZANIA MJUMBE WA BODI TENDAJI UNDP, UNFPA NA UNOPS
- KINANA AZURU NYUMBANI KWA MAREHEMU MGIMWA, IRINGA
- RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJENGO YA BUNGE DODOMA
- MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AGUSWA NA UTENDAJI WA KINANA, ...
- MATEMBEZI YA MSHIKAMAO KUADHIMISHA MIAKA 37 YA CCM...
- MWENYEKITI WA CCM TAIFA AWASILI MKOANI MBEYA TAYAR...
- MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YAFIKIA HATUA ZA...
- CCM YAZIDI KUJIIMARISHA MBEYA MJINI
- MAANDALIZI SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM YAIVA MBEYA
-
▼
February
(88)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.