MKUU wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme amewakutanisha vijana 316 wa wilaya hiyo na kuunda SACCOS yao, katika kutelekeza sera ya CCM ya kuwakomboa vijana kichumi na kuondokana na umaskini na pia kuwaondoa vijana kutojihisisha na shughuli ambazo hazina tija kwao na taifa.
Saccos hiyo ambayo tayari imesajiliwa kwa jina la Hanang Vijana inawanachama wapatao 269 katika wenye ikundi vitano vya ufugaji kuku wa kienyeji, ufyatuaji wa matofali kisasa kwa teknolojia ya hydroform, bodaboda, ufugaji nyuki na kilimo.
Mkuu huyo wa wilaya amesema leo kwamba, Saccos hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni wilayani Hanang na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamadu7ni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara waziri wa habari, vijana.
"Vijana wa wilaya hii wamefurahia muungano huu kwani wamesema ni kwa mara ya kwanza tangu wilaya imeundwa kwa mkuu wa wilaya kuwaunganisha vijana bila kujali itikadi zao wala dini wa jinsia", alisema Mkuu huyo wa nwilaya
Alisema vijanahao wameishukuru sana serikali kwa mpango huo wa kwaunganisha na wameahidi kushiriki kikamilifu katika shushuli za kiuchumi na kushirikiana na serikali.
Mkuu huyo alisema Saccos hiyo inaundwa na vija wote kuanzia wenye elimu ya Chuo Kikuu mpaka darasa la saba na
ambao hawakwenda shule na kauli mbiu yao ni: "Juhudi za vijana ni ukombozi wa taifa- Hanang amani na maendeleo".
Kwa kweli vijana wa Hanang tunamshukuru sana mkuu wetu wa wilaya na serikali kwa ujumla kwa juhudi zake katika kutokomeza umasikikini, wengi wetu tulikuwa hatuna ajira rasmi wala kipato cha uhakika, SACCOS hii inatupa matumaini ya kujikomboa kutoka katika umasikini na kuijenga Hananh yetu. Hongera Mhe. Mndeme.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.