Google PlusRSS FeedEmail

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya  siku ya Jumamosi kutokana na muda. Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila mwaka.
Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila mara alisimama na kuwasalimia. 

Picha na Ikulu.

WANANCHI WAFURAHI KUMUONA RAIS KIKWETE AKIJUMUIKA NAO KWENYE MAONESHO YA SABASABA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya M... [Read More]

 Mbunge wa Chalinze, mkoa wa Pwani, Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, akijaribu kimoja kati ya vitanda 267, kabla ya kuvigawa kwa shule saba za jimboni Chalinze, katika hafla iliyofanyika jana, kwenye shule ya Sekondari Lugoba jimboni humo. Shule zilizopewa vitanda hivyo vikiwa na magodoro yake, idadi ya vitanda ilivyopata ikiwa kwenye mabano ni; Chalinze (50), Moreto (50), Mandera (25), Talawanda (24), Kiwangawa (50), Lugoba (38) na Kikaro (30). Kwa mujibu wa Ridhiwani mgawo huo ni wa awamu ya kwanza.
 Ridhiwani akimkabidhi vitanda  50 Mwalimu Emmanuel Kahabi kwa ajili ya shule ya Chalinze. Kushono ni Abubakari Mlawa wa Kampuni ya MM Steel iliyotoa vitanda hivyo
 Abdalla Sakasa wa Lugoba- akikabidhiwa vitanda vitanda 38
 Charles Mussa wa Talawanda- vitanda  24
 Justin Nguma wa Moreto  vitanda 50
 Omari Msami wa Kikaro-vitanda 30
 Rose Umila wa  Mandera Girls vitanda 25
 Saidi Ally wa Kiwangwa akipongezwa na wadau baada ya kupata vitanda 50.
 Ridhiwani akifurahi na wanafunzi wa shule ya Talawanda baada ya kukabidhi vitanda kwa mwalimu wa shyle hiyo (kulia)
 Mgawo awamu ya kwanza
 Ridhiwani akizungumza na wadau kueleza mikakati mbalimbali ya kukwamua maendeleo ya jimbo la Chalinze, ambapo alieleza kuwa miongoni mwa vipaumbele ni huduma za umeme ambapo italetwa Transfoma itakayowezesha jimbo hilo kupata umeme wa uhakika, afya na elimu
Wadau wakimsikiliza Ridhiwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog

RIDHIWANI AANZA KUSAIDIA WADAU, AKABIDHI VITANDA 167 KWA SHULE SABA JIMBONI MWAKE, AAHIDI KUMALIZIKA TATIZO LA UMEME CHALINZE

 Mbunge wa Chalinze, mkoa wa Pwani, Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, akijaribu kimoja kati ya vitanda 267, kabla ya kuvigawa kwa shule saba... [Read More]


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu kwa jina la FACEBOOK ya mwimbaji nguli wa muziki wa injili Rose Muhando, 

Msama alisema kuwa albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond-Jubilee jijini Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.

 Msama amesema kuwa baada ya albamu hiyo kuzinduliwa jijini Dar,Rose Muhando ataitambulisha tena albamu hiyoa kwa mashabiki wake Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Amesema kuwa kwa upande wa mkoa wa Mwanza,Rose Muhando ametoa kipau mbele kwa jiji hilo kuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa jijini Dar es Salaam.Msama amewataka mashabiki wa mwimbaji huyo nyota wa nyimbo za injili hapa nchini kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono.
Msama amesema kuwa Rose Muhando anaendelea kujipanga vyema kuhakikisha anawapa burudani ya nguvu,

Kwa mujibu wa Alex Msama amesema kuwa nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

FACEBOOK KUZINDULIWA JIJINI DAR AGOSTI 3,WAKAZI WA MWANZA WAJIANDAE AGOSTI 10 UWANJA WA CCM KIRUMBA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua a... [Read More]



1w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC) na Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, Wakati alipowasili katika banda la (NHC) na kukagua, Kupata maelezo mbalimbali ya shughuli za miradi inayotekelezwa na shirika hilo. Wakati alipotembelea maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam. Yanayofikia tamati kesho jijini Dar es salaam , Katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wa pili kutoka kulia ni Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa Mawasiliano NHC.
4w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika la Nyumba NHC kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dr. Abdalla Kigoda na Nalindwa Norbert mmoja wa maofisa wa Shirika la Nyumba NHC.
5w
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea banda lao ili kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
6w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa NHC , Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara (NHC) Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi , Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki na Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC).
7w
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara NHC Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi, Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC) na Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa (NHC) wakisubiri kuwasili kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete katika banda lao.
3w
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wakati alipotembelea banda hilo.

KIKWETE AFURAHISHWA NA MIRADI YA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)

Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC) na Felix Maag... [Read More]



IMG_1291
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.
Na Mwandishi Wetu
WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kesho Jumatatu wanatarajiwa kuchezeshewa droo maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.
Katika droo hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali watakaojishindia zawadi hizo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer alieleza kuwa, droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja wote waliopata kutembelea banda hilo tokea siku ya kwanza na kujiorodhesha majina yao
Fatema alisema MeTL Group imeamua kutoa zawadi hizo kama shukrani na kujitangaza zaidi kwa wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa za MeTL Group.
“Kwa ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group, kama inavyojulikana, ‘The People’s Brand’, kwa droo hii wateja wetu watafurahia kwa zawadi hizo nono” alisema Fatema.
Katika droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki, zawadi za khanga, vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Aidha, MeTL Group imetambulisha rasmi vinywaji vyake vipya kwenye maonyesho hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye maonyesho hayo, MO Cola, MO Portello na MO Malt. Vingine ni MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).

JERRY SLAA KUKABIDHI ZAWADI KWA WATEJA WA BANDA LA MeTL SABASABA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa. Na Mwandishi Wetu WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 y... [Read More]


DSC_0086

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwasili kwenye banda la Makampuni ya MeTL GROUP na kulakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji (wa pili kushoto). Kulia ni Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali na Kushoto ni Afisa Mauzo wa MeTL GROUP, Yusuf Sadiq.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

DSC_0063

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na mkewe akiwasili katika banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0064

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer ( wa pili kulia) akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kwenye banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kulia ni Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.

DSC_0090

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Makampuni ya MeTL GROUP linalotoa huduma za bidhaa mbalimbali zikiwemo Soda, Unga, Mafuta ya kupikia, Sabuni za kufulia na Sabuni za kuogea na vingine vingi.

DSC_0070

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Makampuni ya MeTL Group huku Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akishuhudia tukio hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0097

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer (wa pili kulia) akimuelezea mchanganyiko uliotumika kutengenezea Soda zinazozalishwa na kiwanda cha AOne chini ya kampuni ya MeTL GROUP Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo jana kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0100

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akimwonyesha kinywaji kipya cha “MO Bomba” (Energy Drink)inayozalishwa na Aone kampuni mama ya vimiminika ya MeTL GROUP, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0118

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer (katikati) akitoa maelezo ya mali ghafi zinazotumika kutengenezea Mafuta ya kupikia yanayozalishwa na kiwanda cha East Coast Oils and Fats chini ya makampuni ya MeTL GROUP kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyetembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0124

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akikagua moja ya madumu ya mafuta yanayotengenezwa na kampuni ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar . Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer.

DSC_0143

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akimkabidhi zawadi ya Vitenge na Khanga vinavyozalishwa na kiwanda cha 21st CENTURY Textile Ltd chini ya Makampuni ya MeTL GROUP alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0146

Mdhibiti ubora idara ya sabuni za kampuni ya MeTL GROUP, Cuthbert Sangiwa Msuya akitoa maelezo ya utengezaji wa sabuni na vipodozi vya kampuni hiyo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) ( wa tatu kulia)alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer.

DSC_0004

Umati wa wakazi wa jiji la Dar wakimiminika kujipatia mahitaji maalum kwenye banda la makampuni ya METL kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar

DSC_0186

Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (wa pili kushoto) akimwonyesha bango la kampuni ya mama ya MeTL GROUP, STAR OIL Ltd wauzaji wa mafuta magari Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0033

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akipozi na mtoto aliyenunua kinywaji cha MO Malt kinachotengenezwa na kiwanda cha AOne chini ya kampuni ya MeTL GROUP.

DSC_0203

Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (Katikati) akitoa maelezo ya Baiskeli bora na imara za NABICO zinazotengenezwa na kampuni MeTL GROUP kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) aliyembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kulia ni Msimamizi wa mauzo kwenye la maonyesho ya sabasaba la MeTL GROUP, Jumanne Kisawaga.

DSC_0226

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer (kushoto) wakati akikagua Matrekta ya MeTL AGRO na zana bora za Kilimo zikiwemo Mbolea kwenye banda la makampuni ya MeTL GROUP hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Wa pili kulia ni Meneja Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.

DSC_0256

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo jana jijini Dar.

DSC_0232

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer akimsindikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid mara baada ya kutembelea banda la maonyesho ya Sabasaba la kampuni hiyo kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0265

Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi akiagana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea banda la kampuni hiyo.

DSC_0335

Mkurugenzi wa Masoko wa Makampuni ya MeTL “The People’s Brand”, Fatema Dewji- Jaffer akiwa (wa pili kushoto) kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa makampuni hayo ndani banda lao la maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0313

Mkazi wa jiji la Dar aliyekutwa na mpiga picha akiwa amejitwisha Carton ya Soda mpya za MO Portello zinazozalishwa na kamapuni ya MeTL Group kwenye duka la bidhaa banda mbalimbali ndani ya Banda la kampuni hiyo.

DSC_0345

Wafanyakazi wa wa Royal Soap Detergent Industries Zuhura Mwachuma na Aneth Masesa wakionyesha wateja bidhaa zao za sabuni ya unga waliofika kwenye banda la kampuni ya MeTL kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0323

Baadhi ya wafanyakazi wa makampuni ya MeTL wakipanga bidhaa mbalimbali kwenye duka lao lililopo ndani ya banda lao mbalimbali kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0041

Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko MeTL Group, Kelvin Msangi akipozi na mmoja wa wateja Bw. Bantanuka Burchardy baada ya kuwakabidhi zawadi ya T-shirt na Soda kama asante kwa kulwanunulia watoto wake Baiskeli mpya zilizopo kwenye banda la MeTL GROUP kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0021

Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko MeTL Group, Kelvin Msangi akimkabidhi zawadi Fransisca Bonifa mmoja wa wateja aliyenunua Viitenge kwenye banda la MeTL lililopo kwenye kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

DSC_0303

Mtaalamu wa kutembea juu kamba nchini Hassan Mkenjula a.k.a SPIDERMAN akitembea juu kamba huku akijiandaa kuvaa T-Shirt juu ya kamba hiyo huku umati wa watu ukishuhudia burudani hiyo…..Burudani hiyo ipo hapo siku zote za maonyesho ya Sabasaba mletee mtoto wako na familia waje kushuhudia burudani ya bure kabisa huku mkijipatia mahitaji mbalimbali kwenye banda la MeTL Group.

MAWAZIRI WATEMBELEA BANDA LA MeTL GROUP MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb) akiwasili kwenye banda la Makampuni ya MeTL GROUP na kulakiwa n... [Read More]



Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kila mwaka kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wakati alipotembelea na kukagua mabanda ya makampuni mbalimbali yanayoshiriki kwenye maonyesho hayo.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- DAR ES SALAAM 2 
 12 
Mshauri wa jeshi la Magereza Bw. Alferio akitoa maelezo kwa Rais jakaya Kikwete kuhusu kofia bora za kujikinga waendesha pikipiki wakati alipotembelea katika banda la Mafereza 15 
Rais jakaya Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje wakati alipotembelea katika banda hilo leo Mh. Rais Jakya Kikwete aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa. 3 
Rais jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasliano wa Umoja wa Mataifa (UN)wakati alipotembelea banda hilo leo na kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini. 4 
Rais jakaya Kikwete akizungumza na vijana waliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa katika mafunzo ya ujasiriamali wa tatu kutoka kulia nji Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasiliano wa umoja wa Mataifa (UN)
17 
Rais jakaya Kikwete akimsalimia mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati akitembelea katika mabanda mbalimbali kwenye viwanja vya Sabasaba leo.

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAONYESHO YA TANTRADE LEO

  Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kila mwaka kwenye viwanja... [Read More]