TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba balozi mdogo wa Libya nchini Tanzania , Bwana Ismail Nwairat amejiua ofisini kwake.
Taarifa za awali zinasema Balozi huyo alijifungia ofsini kwake na kujipiga risasi kifuani.
Hata hivyo haijalezwa nini chanzo cha tukio hilo na taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi na mamlaka zinazohusika.
Mtandao huu unafuatilia kwa umakini taarifa hizi na pindi zitakapotbitishwa utajuzwa kwa kina.