Google PlusRSS FeedEmail
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan,  wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Syria nchini Tanzania, Abdulmonem Annan, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 3, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA
Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 03, 2014
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Julai 03, 2014 amekutana na Waheshimiwa Mabalozi wa nchi za Oman na Syria wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Mheshimiwa Makamu wa Rais amekutana na Mabalozi hao ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Awali alikuwa ni Balozi wa Oman, Mheshimiwa Saoud Ali Mohammed Al-Ruqaish aliyefika kukutana na Mheshimiwa Makamu na kufafanua kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman unazidi kuimarika na kwamba wawekezaji kutoka Oman wamekuwa wakija kwa wingi kuwekeza Tanzania tofauti na siku za nyuma huku pia Tanzania ikionesha kufungua milango yake kwa uwekezaji mkubwa wa kati nchini Tanzania.
Kwa upande wa Balozi wa Syria Mheshimiwa Abdulmonem Annan yeye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa Syria iko katika kipindi kigumu na kwamba nchi hiyo kwa sasa inatafuta kila linalowezekana kurejesha amani. Balozi huyo alifafanua kuwa nchi yake inahitaji msaada wa nchi za Kimataifa ili kusaidia kuweka pande zote zinazokinzana mezani kwa lengo la kufikia maazimio yatakayoifanya nchi hiyo isiparanganyike.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi za Syria kuwa, Tanzania inatamani sana kuona hali ya utulivu inarejea Syria na kwamba nchi hiyo inaendelea kujenga uchumi uliobomoka tayari. Pia alisema kuwa msimamo wa Tanzania unabakia katika kutaka pande zinazohusika katika mgogoro huo zinafuikia suluhu kwa amani ili wananchi wengi wasipoteze maisha.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam


MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MABALOZI WA OMAN NA SYRIA

  Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saoud Ali Moh... [Read More]

Meneja wa Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo , akifurahia tuzo ya udhamini kwa upande wa vinjwaji katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa baada kuipokea kutoka kwa  Makamu wa Pili wa  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi, Seif Alli Idd Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalla Kigoda.

TBL YATWAA TUZO YA UDHAMINI MAONESHO YA SABASABA DAR

Meneja wa Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo , akifurahia tuzo ya udhamini kwa upande wa vinjwaji katika Maones... [Read More]



DSC_0004
Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0008
Utajiuliza kwani LG wapo ndani ya Banda la MeTL Group kwenye maonyesho ya Sabasaba kwa sababu MeTL Group wamekuwa Mawakala waliothibitishwa Tanzania nzima (Authorized Dealers) kuuza vifaa vya LG nchini. USISAHAU KUJINADIKISHA KWA AJILI YA DROO YA BAHATI NASIBU ITAKAYOCHEZESHWA TAREHE 7 MWEZI HUU NDANI YA BANDA LETU...!
DSC_0120
Kampuni ya MeTL Group inahusika pia na masuala ya Vitenge, Khanga, Mashuka na n.k Njoo upendeze mwanamke na vitenge bora na imara kutoka MeTL Group.....Sikukuu ya Eid ilee na maandalizi yawe mapema kabisa...!
DSC_0125
Wakazi wa jiji la Dar wakivinjari ndani ya Banda la Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL Group) kujipatia mahitaji mbalimbali za bidhaa bora kabisa kwa bei nafuu msimu huu wa Sabasaba.
DSC_0151
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiangalia na kupata maelezo ya bidhaa mbalimbali kama TV, Music System, Simu za mkononi za nyingine nyingi kutoka kampuni ya LG ambapo MeTL Group ndio Authorized Dealers pekee nchini Tanzania.
DSC_0124
Muonekano wa ndani wa Banda letu la MeTL Group ukiwa umenakshiwa kwa mabango pamoja na TV za LG zinazoonyesha matangazo mbalimbali ya bidhaa zetu.
DSC_0136
Mmoja wa wateja akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wetu waliobobea wa vipozi kwenye banda letu la MeTL Group.
DSC_0117
Watu wanatakaje kupendeza.....!! bado wewe tu hujajipatia kitenge chako na Khanga....kwa bei nafuu kabisa katika msimu wa Sabasaba.
DSC_0360
Baadhi ya ushers wanaotohuduma kwa wateja ndani ya banda la MeTL GROUP wakipozi kwenye Big Screen ya LG inayoonyesha tangazo la bidhaa mpya ya "MO BEAUTY SOAP" ambapo Balozi wake ni mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.

DSC_0238
Mmoja wa kikundi cha uhamasishaji kwenye banda la MeTL Group akikata kiu yake na kinywa chenye ladha tamu kabisa ambacho kitaingia sokoni hivi karibuni "MO Portello" kinachouzwa ndani ya banda hilo.
DSC_0240
Aaaah kinywaji safi kabisa...sasa nimekata kiu yangu...!! Unakaribishwa na wewe pia kukijaribu kinauzwa kwa bei nzuri kabisa ya offer katika msimu huu wa Sabasaba.
DSC_0242
Mimi napenda "MO Portello" wewe je....??
DSC_0292
AGRO MeTL wauzaji wa Mbolea na Matrekta ya kisasa ambayo ni imara na bora kwa mazingira yetu ya Tanzania yapo kwenye banda letu...Kilimo kwanza ndio mpango mzima...!!
DSC_0109
Mambo ya Katani yanahusika pia ndani ya banda la MeTL Group kwenye viwanja vya Sabasaba.
DSC_0131
Mambo ya Ugali, Maandazi na bidhaa mbalimbali za nafaka zinapatikana pia bila kusahau MO SEMBE..Unga safi kabisa wa kupikia.
DSC_0142
Mambo ya usafi pia yanahusika jamani eeeeh...Sabuni za kufulia za unga zenye kuondoa madoa sugu na uchafu wa aina zote zinapatikana pia wewe tu na pochi lako.
DSC_0224
Watoto wakipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa vinywaji vya MeTL Group kwenye banda letu ndani ya maonyesho ya Sabasaba.
DSC_0236
Watoto wakipata Ukodak baada ya kuyakubali maji safi ya kunywa kwa gharama nafuu kabisa yanayotengenezwa na MeTL Group.
DSC_0253
Kata kiu yako kwa kujichagulia kinywaji ukipendacho hapa ndani ya banda la MeTL GROUP.
DSC_0345
Mmoja wa wateja akiangalia tangazo la bidhaa mpya ya MO BEAUTY SOAP ambapo Balozi wa sabuni hiyo ni mrembo aliyewahi kushitaji la Miss Tanzania namba mbili JOKATE MWEGELO.
DSC_0332
DSC_0113
Mfanyakazi wa MeTL Group akitoa maelezo ya ubora wa maji safi ya kunywa yenye viwango vya kimataifa. Unakaribishwa sana kuuliza maswali mbalimbali ndani ya banda letu.
DSC_0264
Kikundi cha NOMA SANA Group kikitoa burudani nje ya banda la MeTL Group kuwatumbuiza wakazi wa jiji wanaotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini.Kwa picha zaidi ingia hapa

MAMBO YAMEIVA NDANI YA BANDA LA MeTL GROUP KWENYE MAONYESHO YA SABASABA!

Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam ... [Read More]


Mkurugenzi-wa-Idara-ya-Habari-Maelezo-Asa-Mwambene-kulia-akiwa-na-Mkurugenzi-Msaidizi-wa-Idara-hiyo-Vicent-Tiganya-640x360 
Msemaji wa Serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku katika chumba cha ofisi za ubalozi huo.
Mwambene alisema kuwa mpaka sasa haijafahamika kifo cha balozi huyo kimetokana na nini, ila wafanyakazi wa karibu katika ubalozi huo wamesema kuwa walisikia mlio wa risasi chumbani kwake, na walipojaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa na wakatumia nguvu ya kuvunja mlango huo na kufanikiwa kumkuta balozi yupo katika hali ya mbaya.
Aidha walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia.
Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.

SERIKALI YATHIBITISHA KIFO CHA BALOZI WA LIBYA

  Msemaji wa Serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kuji... [Read More]


DSC_0208 DSC_0209
DSC_0218
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya banda lao na nyuso za bashasha baada ya kunyakua tuzo ya Machapisho kwa Umma (Mass Media na Publicity) kwa mara ya tatu mfululizo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kutoka kushoto ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi, Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Programme Officer wa Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji (IOM), Charles Mkude na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
DSC_0226
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa wameshikilia tuzo pamoja na cheti walichotunikiwa jana wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyopewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi.
DSC_0162
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama (wa tatu kushoto) akizungumza na mzazi aliyeambatana na watoto wake kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwa ajili ya kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. Kushoto ni Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana " Kazi Njenje" na anayefuatia ni Programme Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi.
DSC_0174
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa mzazi aliyeambatana na watoto kwenye banda la Umoja wa Mataifa kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa hapa nchini kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
DSC_0195
Amos Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana "Kazi Njenje" akieleza kwa mmoja wa wadau namna anavyofanya kazi zake za uchoraji ambapo UN imempa nafasi ya kuonyesha kuonyesha kazi zake za sanaa ya uchoraji kwenye banda hilo kwa ajili yakujitafutia soko na kuendeleza maisha yake.
DSC_0232
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wageni waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.

UN YAZIDI KUNG'AA MAONYESHO YA SABASABA, YATWAA TUZO YA "MACHAPISHO KWA UMMA"

Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya banda lao na nyuso za bashasha baada ya kunyakua tuzo ... [Read More]



Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.

 Rais wa Burundi akisalimiana na mke wa Makamu wa Rais wa Tanzania.

 Vijana wa halaiki wakipamba maadhimisho hayo

 Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwenye maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.  (Picha na OMR)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza walipokutana kwenye Uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi wakati wa maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika Julai 1-2014.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mwa Tanzania Mhe. Dkt Moahammed Gharib Bilal, Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza wakipokea maandamano ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika Julai 1-2014 katika uwanja wa Prince Louis Rwegasore jijini Bujumbura Burundi.
 Julai 01, 2014 Bujumbura

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Jumanne, Julai Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za kilele cha miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.


Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia kulikuwa na Makamu wa Rais wa Somalia, Waziri Mkuu wa Chad na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika. Sherehe hizo zilianza kwa Rais Pierre Nkurunzinza kuweka silaha katika eneo  maalum la Uhuru na kufuatiwa na maadhimisho yaliyoshirikisha wananchi mbalimbali katika uwanja wa Rwagasore.


Akizungumza baada ya kutoa tuzo mbalimbali za heshima, Rais Nkurunzinza aliwashukuru wageni wote waliofika katika sherehe hizo na akabainisha kuwa Tanzania ni rafiki wa Burundi hivyo anafurahishwa sana kuona ikiwa imewakilishwa na uongozi wa ngazi za juu katika sherehe hizo.


Burundi ambayo inategemea sana bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na hasa uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo linaiunganisha na Tanzania, inaadhimisha miaka 52 ya uhuru huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali kiuchumi sambamba na kisiasa kufuatia kuwa na miongo kadhaa ya mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.


Kwa sasa Burundi licha ya kukua kimaendeleo pia inaongezeka idadi ambapo inakadiriwa kuwa na watu milioni 6. 

Uhusiano baina ya Tanzania na Burundi unabaki kuwa wa damu ambapo pia redio za nchi hii hutangaza vipindi kadhaa kwa kutimia Kiswahili sambamba na nyimbo za muziki za wasanii wa Tanzania hupata nafasi kubwa katika redio za Burundi.

Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai Mosi, 2014 Bujumbura: Burundi

DK BILAL AUHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU WA BURUNDI

Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza akikagua gwaride rasmi kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 52 wa Uhuru wa Nchi hiyo yaliyofanyika Julai... [Read More]

BREAKING NEWZZZ!: BALOZI MDOGO WA LIBYA NCHINI TANZANIA AJIUA

TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba balozi mdogo wa Libya nchini Tanzania , Bwana Ismail Nwairat amejiua ofisini kwake. Taarifa... [Read More]