NDUGU KINANA |
DAR ES SALAAM, Tanzania
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahiman Kinana anawatakia Wakristo na watanzania wote kwa ujumla sikukuu njema ya Pasaka.
Ndugu Kinana amesema "Ni vema watanzania kwa pamoja kusherehekea sikukuu hii ya Pasaka kwa unyenyekevu na utulivu.
Ndugu Kinana amewaasa pia Watanzania kuitumia sikukuu hii kutafakari kwa kina na kumwomba Mungu aendelee kuijalia nchi yetu ya Tanzania ili iendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
CCM inaamini kuwa wajibu wa kuilinda Amani, upendo na umoja ni ya kila mwananchi na kwamba la msingi ni kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake.