Google PlusRSS FeedEmail

MKUTANO WA UVCCM, ULIOFANYIKA LEO MOROGORO WAFANA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma akihutubia aktika mkutano wa UVCCM uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mkwajuni, Kata ya Kichangani mkoani Morogoro leo Machi 3, 2013, ikiwa ni mwisho wa ziara yake na viongozi wa kitaifa wa Jumuia hiyo mkoani humo, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na UVCCM
Mbunge wa Morogoro, Abdulazizi Mohammed Abood akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM, baada ya kupandishwa jukwaani na Sadifa (wapili kushoto) wakati wa mkutano huo.
 Sadifa akikabidhi kadi ya Umoja wa CCM, kwa mwanachama mpya wakati wa mkutano huo. Jumla ya wanachama 1700 walipewa kadi.
Sadifa na baadhi ya viongozi wakishirikina na wanachama kula kiapo cha CCM baada ya wanachama wapya wa UVCCM kupewa kadi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akihutubia kwenye mkutano huo
 Mmoja wa vijana machachari aliyehama hivi karibuni kutoka Chadema, Mtela Mwampamba akihutubia kwenye mkutano huo.
"Vijana, Chadema wanawazingua tu, wanawahamasisha kufanya maandamano ili wawapige picha za kwenda kuonyesha  nchi za nje kwa marafiki zao ili wapewe mamilioni ya fedha kwa manufaa yao", anasema Mwampamba kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya UVCCM Kaka Mpokwa.
Vijana wakiwa wamembeba Mwampamba baada ya kuinogewa na hotuba yake kwenye mkutano huo
Kama Mwampamba, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, Juliana Shonza, ambaye amehamia CCM hivi karibuni, akibebwa na vijana wa UVCCM, baada ya 'kuimwagia razi' Chadema jukwaani kwenye mkutano huo.
"Hawa walijaribu kuwapiga mawe ili msifike kwenye mkutano huu, lakini tazama mlivyofurika! Sasa ninasema, Uwezo wa kuwapiga tunao na nia ya kuwapiga tunayo..Tutawapiga, lakini sisi hatutawapiga kwa mawe ila kwa sera zetu makini" akasema Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati akihutubia kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Morogoro, Abdulaziz Mohamed Abood akiongoza msafara wa pikipiki kwenda kwenye mkutano huo
 Vijana wakiserebuka kwa nyimbo za hamasa kwenye mkutano huo
 "Raaaaaaa UVCCM" Vijana hawa wa CCM wakati wa shamrashamra kwenye mkutano huo
Kujimwaya mwaya hakukukoma hadi mwisho wa mkutano. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO WA Nkoromo Blog na CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply