Google PlusRSS FeedEmail
 KATIBU Mkuu mstaafu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Sixtus Mapunda, faili wakati wa makabidhiano ya Ofisi, waliyofanya leo, Makao Makuu ya UVCCM, mjini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni, Naibu Katibu Mkuu UVCCM (Bara), Mfaume Ally Kizigo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Seki Kasuga..
 Sixtus Mapunda akipitia nyaraka kwenye faili alilokabidhiwa na Shigela wakati wa makabidhiano ya ofisi leo. Kushoto ni Kizigo
 Makamu Mwenyekiti UVCCM, Taifa, Mboni Mhita (kushoto) akisalimiana na Shigela baada ya kuwasili kwenye mapokezi hayo.
Mboni Mhita akimsalimia pia, Mkumbe wa Kamati Kuu ya Utekelezaji UVCCM Taufa,Seki Kasuga wakati wa makabidhiano hayo. Imetayarishwa na BASHIR NKOROMO

SHIGELA NA SIXTUS WAFANYA MAKABIDHIANO RASMI YA OFISI LEO

 KATIBU Mkuu mstaafu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Sixtus Mapunda, fai... [Read More]



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
 
Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.
 
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
 
Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.
 
Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.
 
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
 
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
05/09/2013

 

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA KUFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA SHINYANGA,MARA NA SIMIYU

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, S... [Read More]

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Saloaam, leo.
 Balozi wa Sudan hapa nchini Dk. Yassir Mohamed Ali (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kitabu kuhusu nchi hiyto, wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
Kinana akimshukuru Balozi kwa kumpa kitabu hicho. Imetayarushwa na theNkoromo Blog

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA SUDAN

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, ... [Read More]



Ilikuwa dakika, saa, mwezi na sasa ni miaka 10 kamili tangu alyekuwa Baba wa Marehemu John Stephano Shilatu, Mzee STEPHANO SHIGEMELO SHILATU wa Kisesa Mwanza atutoke ghafla duniani mnamo tarehe 04/09/2003 kutokana na mradhi yaliyokuwa yanakusumbua.

Unakumbukwa na wanao, wajukuu, vitukuu, ndugu, jamaa na marafiki zako ambao hawataa wausahau ucheshi, upendo, na huruma zako kwa kila mtu.

Tunazidi kumuomba Mwenyezi Mungu akupumzishe mahali pema peponi.
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE! AMEN!!

KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 YA NDG. STEPHEN S. SHILATU

Ilikuwa dakika, saa, mwezi na sasa ni miaka 10 kamili tangu alyekuwa Baba wa Marehemu John Stephano Shilatu, Mzee STEPHANO SHIGEMELO SHIL... [Read More]

 Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda (wapili kushoto) akiwasalimia baadhi ya watumishi wa makao makuu ya Jumuia hiyo, jijini Dar es Salaam, alipowasili kuripoti rasmi ofisini kwake, kwenye jengo la makao makuu hayo ya UVCCM, lililopo kwenye makutano ya Barabara ya Morogoro na Lumumba. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Mfaume Ally Kizigo ambaye Baraza Kuu la UVCCM lililofanyika Zanzibar juzi, lilimuithinisha kuendelea na nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia zaidi ya miaka minne sasa.
 "HAPA NDIYO OFISINI KWAKO MKUU" Kizigo akisema, wakati wakiwa ofisini kwa Sixtus, makamo makuu ya UVCCM, Dar es Salaam.
Sixtus na Kizigo wakipeana mikakati ya kazi, baada ya mapokezi ya viongozi hao makao makuu ya UVCCM Dar es Salaam, leo. Imetayarishwa na: theNkoromo Blog

SIXTUS ARIPOTI RASMI LEO MAKAO MAKUU YA UVCCM, DAR

 Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda (wapili kushoto) akiwasalimia baadhi ya watumishi wa makao makuu ya Jumui... [Read More]

  • Adai Vijana wamelelewa vyema na Muungano wa Serikali mbili na ndio Muungano pekee wanaouelewa.
  • Asisitiza  Umoja kati ya wana CCM na kuwaambia wakidumisha umoja watakuwa imara zaidi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (Zanzibar) Ndugu Shaka Hamdu Shaka akihutubia wananchi wa Zanzibar na kuwaahidi kuwa sasa wajiandae kwa mikutano ya mara kwa mara yenye tija ya kuimarisha chama na kudumisha Muungano.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akiwahutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya leo tarehe 1 Septemba 2013.
 Waandishi kutoka vyombo mbali mbali wakichukua matukio kwenye Mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Komba Wapya Zanzibar.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Sadifa Juma Khamis akihutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya.
 Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakionekana kuvutiwa na hotuba za viongozi wa umoja wa Vijana.
 Wapenzi wa CCM Zanzibar wakiwa wamekaa mpaka juu ya nyumba kusikiliza hotuba za viongozi wao kutoka umoja wa jumuiya ya vijana wa CCM.

SIXTUS MAPUNDA: VIJANA WANAUELEWA ZAIDI MUUNGANO WA SERIKALI MBILI

Adai Vijana wamelelewa vyema na Muungano wa Serikali mbili na ndio Muungano pekee wanaouelewa. Asisitiza  Umoja kati ya wana CCM na kuwaambi... [Read More]

Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Martin Shigela akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Mboni Muhita kabla ya kuanza kwa kikao cha wajumbe wa baraza la Umoja wa Vijana katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


Mtela Mwampamba akiwasili kwenye uwanja wa CCM Afisi Kuu za CCM Zanzibar tayari kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Vijana Taifa.

Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa  Antony Mavunde akisaliminiana na Mjumbe wa Baraza kutoka Jumuiya ya Wazazi William Malecela nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Vijana Taifa.
Wajumbe wa Baraza la Vijana wakicheza ngoma ya Boso yenye asili ya Kusini Pemba, kabla ya kuanza kikao cha Baraza Kuu la Vijana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Balozi Seif Idd akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar ambapo Makamu wa Pili wa Rais ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi.
Viongozi Wakuu wa CCM wakiomba Dua mbele ya kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Vijana la CCM Taifa.


January Makamba akizungumza na Wajumbe wa Baraza laVijana wa CCM kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Emmanuel Nchimbi akitoa salaam kwa wajumbe wa Baraza kuu la Vijana Taifa kabla kuanza kwa kikao cha Baraza Kuu la Vijana wa CCM
Mjumbe wa Kamati Kuu Mohamed Seif Khatibu akiwasalimu wajumbe wa Kikao Cha Baraza Kuu la Vijana la Taifa kwenye ukumbi wa mikutano CCM Zanzibar.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Sadifa Juma Hamisi akisoma risala kabla ya kumkaribisha Balozi Seif Idd kufungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana.


Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Idd akitoa hotuba ya kufungua kikao cha Baraza Kuu la CCM Vijana leo 1/9/2013 katika ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.



Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda akizungumza kwa mara ya kwanza na wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM .

 Meza Kuu ikiwa na Katibu Mkuu mpya aliyechaguliwa Sixtus Mapunda wakati wa kikao cha Baraza la Vijana kilichofanyika Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza kuu la CCM wakiserebuka baada ya kuidhinisha kuwa Sixtus Mapunda ndiye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkubatia Katibu Mkuu wa umoja wa vijana aliyemaliza muda wake Ndugu Martin Shigela,kulia niKatibu Mkuu mpya wa UVCCM akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai .

SIXTUS MAPUNDA APITISHWA KWA KISHINDO UVCCM

Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Martin Shigela akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Mboni Muhita kabla ya kuanza kwa... [Read More]