- Adai Vijana wamelelewa vyema na Muungano wa Serikali mbili na ndio Muungano pekee wanaouelewa.
- Asisitiza Umoja kati ya wana CCM na kuwaambia wakidumisha umoja watakuwa imara zaidi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akiwahutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya leo tarehe 1 Septemba 2013.
Waandishi kutoka vyombo mbali mbali wakichukua matukio kwenye Mkutano wa Umoja wa Vijana wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Komba Wapya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Sadifa Juma Khamis akihutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya.
Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakionekana kuvutiwa na hotuba za viongozi wa umoja wa Vijana.
Wapenzi wa CCM Zanzibar wakiwa wamekaa mpaka juu ya nyumba kusikiliza hotuba za viongozi wao kutoka umoja wa jumuiya ya vijana wa CCM.