Google PlusRSS FeedEmail

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE SHINYANGA VIJIJINI LEO

 
01Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga, ambapo leo katibu Mkuu huyo ameendelea na ziara yake ya siku nne mkoani humo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuimarisha uhai wa chama hicho na utekelezaji wa Ilani ya ya Uchaguzi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -SHINYANGA. 1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum wakicheza na nyoka pamoja na wanakukundi cha utamaduni kutoka jimboni humo. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja akimlipa ujira wa shilingi elfu 10.000 Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye baada ya kumsaidia katika ujenzi wa Birika la kunweshea mifugo katika kata ya Didia, hata hivyo Kinana aliwapa fedha pia wajenzi wa birika hilo. 4Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Soko la Kata ya Didia lililojengwa katika kijiji cha Didia, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja. 5Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mbele ya soko hilo. 8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bw.Kiyungi Mohamde Kiyungi wakati alipokagua ujeni wa Hospitali ya Halmashauri hiyo inayojengwa katika kijiji cha Iselamagazi, wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja. 12Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akicheza na nyoka wakati aliposhiriki katika kucheza ngoma ya asili katika kijiji cha Didia. 14Hili ndilo soko la Didia 16Wapiga ngoma wa Kikundi cha ngoma cha Didia wakipiga ngoma wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa soko la Didia. 18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliomsimamisha katika kijiji cha Mwabenda ambao walikuwa na mabango yaliyokuwa yakielezea kero zao katika kijiji hicho ambazo zilikuwa ni Umeme na maji hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Ally Rufunga aliwaelezea mipango ya serikali kuhusu kijiji hicho katika kuhakikisha maji na umeme vinapatikana mapema katika kijiji hicho. 19Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Salawe katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtunza mmoja wa wasanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Salawe katika jimbo la Solwa mkoani Shinyanga. 22Wananchi wakiwa wamehudhuria kwa wingi katika mkutano huo wa hadhara. 23Mama na mwana wakahudhuria katika mkutano huo. 25Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 26MNEC Azza Hilal Hamad kutoka Viti Maalum mkoa wa Shinyanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijijini Salawe. 27Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwahutubia wapiga kura wake katika kijiji cha Salawe ambapo mkutano wa hadhara umefanyika leo. 28Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Salawe ambapo mkutano wa hadhara umefanyika leo.

This entry was posted in

Leave a Reply