Google PlusRSS FeedEmail

KINANA : NEEMA IMEWAJIA WAKAZI WA SHINYANGA

 Sehemu ya msafara wa Mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiingia Shinyanga Mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini .
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Meneja wa Kiwanda ya kutengeneza nguo na bidhaa zitokanazo na pamba ya Dahong Textile Co.Ltd Jing Lin,kushoto ni Balozi wa China nchini Lu Youqinq.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu uwekezaji kutoka China utakavyounufaisha mkoa wa Shinyanga alipotembelea kiwanda cha Dahong Textile leo tarehe 13 Septemba 2013.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Ally Lufunga  wakizungumzia fursa za mabadiliko ya viwanda walipotembelea cha Dahong textile ambacho kitaleta mabadiliko makubwa kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.
 Sehemu ya Kiwanda cha Dahong Textile kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi ,Kiwanda Hiki kitasaidia ajira kwa watanzania zaidi ya elfu kumi na pia kitasaidia kupandisha uchumi kwa wakulima wa pamba.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Xing Hua Investment ltd Tina Mugisha ambaye amesema kiwanda chake kitawezesha ajira nyingi na pia kuboresha bidhaa zitokanazo na mifugo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari maalum ya kubebea mizigo huku akipata maelezo kutoka kwa Balozi wa China nchini Lu Youqinq wakati alipotembelea kiwanda cha Dahong Textile mkoani Shinyanga.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawekezaji wa viwanda kutoka China mara baada ya kumaliza kuvitembelea viwanda hivyo,kushoto ni Balozi wa China nchini Lu Younqinq.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini Lu Youqinq wakiwapungia mkonno wajumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa,madiwani na mabalozi wa nyumba kumi kwenye uwanja wa Kambarage.
 Balozi wa China nchini Lu Youqinq akisalimia wajjumbe wa halmashauri kuu ya mkoa ,madiwani na mabalozi wa nyumba kumi katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga akipokea laptop kutoka kwa Balozi wa China Lu Youqinq.

 Balozi wa China nchini Lu Youqinq akimkabidhi laptop Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Charles Charles katikati ni Mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele.


This entry was posted in

Leave a Reply