Rais Bashar al Assad wa Syria amekanusha kuwa alihusika na shambulio kwa silaha za kemikali mjini Damascus mwezi uliopita.
Akihojiwa na televisheni ya Marekani, CBS, Bwana Assad alisema ikiwa serikali ya Rais Obama ina ushahidi kuwa alihusika, basi iutoe.
Rais Assad aliongeza kuwa washirika wa Syria watajibu shambulio lolote litalofanywa dhidi yake.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema Rais Assad amechagua wakati muwafaka kwa mahojiano hayo, kwa sababu punde baraza la congress litaanza kujadili azimio kuidhinisha Marekani kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.
Awali Jumapili mjini Paris Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema mawaziri wenzake wa Jumuia ya Kiarabu walikubali kuwa ikiwa Syria ilitumia silaha za kemikali, basi ilipindukia viwango vya kimataifa. BBC