Ndugu Kinana |
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kesho Jumanne, ataanza ziara ya siku nne mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na uhai wa Chama.
Taarifa ilizopata zimesema akiwa mkoani Shinyanga Kinana atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo sambamba na kutoa kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo pia atafanya vikao vya ndani ikiwa ni moja ya mikakati ya uimarishaji wa chama mkoani humo.
Katibu wa CCM mkoani Shinyanga, Adam Ngalawa amesema leo kwamba Kinana na msafara wake akiwemo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye, wanatarajiwa kupokelewa kesho saa 3 asubuhi katika kata ya Isaka wilayani Kahama wakitokea Nzega mkoani Tabora.
Ngalawa alisema baada ya kupokelewa kwa Katibu Mkuu akiwa katika kata ya Isaka atasaini kitabu cha wageni na kisha atapokea taarifa ya utekelezaji wa kazi za CCM za wilaya ya Kahama na mkoa kwa ujumla pamoja na taarifa ya serikali ya mkoa.
Akiwa katika kata hiyo Kinana atagawa kadi za CCM kwa wanachama wapya na kisha atawasalimia wananchi kabla ya kuelekea katika kata ya Mwendakulima ambako atakagua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha... Inaendelea>Bofya Hapa