KINANA ATOA SOMO PEMBA
Awataka wananchi kutokubali kuyumbishwa Awaambia wananchi wa Pemba ,Muungano wa serikali mbili ni rahisi kuusimamia na kuzitatua changamoto ... [Read More]
KINANA AWASILI PEMBA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili kwenye uwan... [Read More]
Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha za nyukilia basi ziwe na haki ya kutumia nyukilia kwa matumizi salama, na pia kupewa misaada ya kiufudi na uwezeshwaji katika eneo hilo.
Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati alipokuwa akitoa maoni ya Tanzania katika mkutano wa Kamati ya Maandalizi kwaajili ya mkutano utakaofanyia tathmini utekelezaji wa Mkataba wa kuzuia usambazaji holela wa silaha za nyukilia ( NPT).
Tanzania inashiriki kikamilifu katika Mkutano huo wa maandalizi ambao ni wa wiki mbili na unafanyika Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Wanaoshiriki mkutano huu ni nchi wanachama wa NPT pamoja na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Dhumuni la mkutano huu wa maandalizi, ni kuaanda dondoo na mapendekezo yatakayojadiliwa katika mkutano wa tathmini kuhusu NPT. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwakani (2015).
Mwakilishi huyo wa Tanzania, amebainisha kwamba, hakuna asiyetambua madhara ya silaha za nyukilia kutokana matukioa kadhaa mbayo yametokea huko nyuma yakiwamo ya Hiroshima.
Akasema, inasikitisha kwamba yale mataifa ambayo yana malimbikizo ya silaha hizo, yameendelea kushikilia misimamo yao na hata kufikia mahali pa kutetea uhalali wa kuwa na silaha hizo.
Tanzania ikaeleza kwamba, silaha za nyukilia si tisho kubwa kwa nchi za Afrika, kwani tishio kubwa na ambalo linachangia katika uvunjifu wa Amani na upotevu wa maisha ya watu ni silaha ndogo ndogo na nyepesi na siyo silaha za nyukilia.
Balozi Mwinyi amewahoji washiriki wa mkutano huo, kwamba ni dunia ya aina gani tunayotaka kuwarithisha watoto wetu kwa kuendelea kukumbatia silaha hizo za maangamizi.
Akabainisha kwamba Tanzania inaamini katika Mkataba huo wa NPT kwa kile alichosema utekelezaji wake utaifanya dunia kuwa mahali salama. Na kwamba licha ya kuridhia mkataba huo, Tanzania pia ni mwanachama wa mikataba mingine ya kikanda inayohusu uthibiti wa silaha za nyukilia. Hotuba Kamili ya Balozi Mwinyi>BOFYA HAPA
TANZANIA YATAKA MATUMIZI SALAMA YA NYUKILIA YASIZUIWE
Na Mwandishi Maalum, New York Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha za nyukilia basi ziwe ... [Read More]
MWENDELEZO WA PASAKA;MWANAMUZIKI REBECCA MALOPE KUTUMBUIZA APRIL 4 JIJINI MWANZA
MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajiwa kutua kwenye jiji la Mwanza a.k.a ROCKY CITY April 4,ikiwa ni... [Read More]
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusianona Uratibu, Stephen Wasira, akisoma rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/20015, jijini Dar es Salaam |
| Waziriwa Fedha Saada Mkuya akisoma Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/15 jijini Dar es Salaam. |
| Waziri Mkuu akizungumza Baada ya kuwakilishwa kwa Rasimu ya Bajeti |
SERIKALI inampango wa kutoa vipaumbele kwa sekta ya gesi na Nishati katika bajeti ya mwaka mpya wafedha wa 2014/2015.
Akisoma Rasim yampango wa Maendeleo wa Taifa 2014/2015 Waziri waNchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu , Stephen Wasira (MB) alivitaja baadhi ya vipaumbele ikiwa ni sekta ya gesi asilia ambapo alitaja kuwa katika eneo la nishati kazi zilizofanyika katika mradi wa Bomba la Gesi (Mtwara –Dar es Salaam) ni kupokea mabomba yote yatakayo hitajika katika mradi huo.
Pia kuendelea kutandaza njia za mabomba ya gesi hadi Kilomita 498.5 sawa na asilimia 96 ya njia yote ya mabomba yenye urefu wa kilomita 212 katika mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi I (MW 150) kwa kutumia gesi asili.
Lengo lilikua ni kuanza kwa ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme ambapo hatua iliyofikiwa hadi Machi mwaka huu, ni kuagiza mitambo na vifaa mbalimbali, ambavyo ni Jenereta mbili za Gesi Asilia ambazo zimeshawasili na ujenzi wa mtambo umeanza.
Hata hivyo serikali imesema itaendelea kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya miradi ya umeme wa msongo wa 220 Kv Norh –West GridKvIringa –Shinyanga na Makambako-Songea.
GESI KUPEWA KIPAUMBELE BAJETI YA 2014/15
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusianona Uratibu, Stephen Wasira, akisoma rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/20015, jijini Dar es Salaam Waziri... [Read More]
SHEREHE ZA MEI MOSI MWANZA ZAFANA
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakipita ya mgeni wa heshima Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evarist Welle Ndikilo wakati wa maadhimi... [Read More]
































