Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusianona Uratibu, Stephen Wasira, akisoma rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/20015, jijini Dar es Salaam |
Waziriwa Fedha Saada Mkuya akisoma Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/15 jijini Dar es Salaam. |
Waziri Mkuu akizungumza Baada ya kuwakilishwa kwa Rasimu ya Bajeti |
SERIKALI inampango wa kutoa vipaumbele kwa sekta ya gesi na Nishati katika bajeti ya mwaka mpya wafedha wa 2014/2015.
Akisoma Rasim yampango wa Maendeleo wa Taifa 2014/2015 Waziri waNchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu , Stephen Wasira (MB) alivitaja baadhi ya vipaumbele ikiwa ni sekta ya gesi asilia ambapo alitaja kuwa katika eneo la nishati kazi zilizofanyika katika mradi wa Bomba la Gesi (Mtwara –Dar es Salaam) ni kupokea mabomba yote yatakayo hitajika katika mradi huo.
Pia kuendelea kutandaza njia za mabomba ya gesi hadi Kilomita 498.5 sawa na asilimia 96 ya njia yote ya mabomba yenye urefu wa kilomita 212 katika mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi I (MW 150) kwa kutumia gesi asili.
Lengo lilikua ni kuanza kwa ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha Umeme ambapo hatua iliyofikiwa hadi Machi mwaka huu, ni kuagiza mitambo na vifaa mbalimbali, ambavyo ni Jenereta mbili za Gesi Asilia ambazo zimeshawasili na ujenzi wa mtambo umeanza.
Hata hivyo serikali imesema itaendelea kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya miradi ya umeme wa msongo wa 220 Kv Norh –West GridKvIringa –Shinyanga na Makambako-Songea.