Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AKAGUA UJENZI DARAJA LA MBUTU, IGUNGA MKOANI TABORA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maelezo kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akishuka, baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikagua sehemu ya ujenzi wa daraja hilo

 Nape akitoka baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitazama jiwe la msingi lililowekwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye ujenzi wa daraja hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply