Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AMALIZA ZIARA SIKONGE KWA KUHUZUNISHWA NA VILIO VYA DHULMA WANAZOFANYIWA WAKULIMA WA TUMBAKU

Kaim Mganga Mkuu Sikonge,  Laurent Lushekya, akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye kituo cha afya cha  Kitunda kilichopo km 170 kutoka  Sikonge mjini, alipofika kukagua kituo hicho cha afya leo Mei 15, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Tabora
Mganga Mfgawidhi wa Kituo cha Afya cha Kitunda, wilayani Sikonge, Dk Sylivanus Kabatula akitoa maelezo wa Ndugu Kinana kuhusu ucheleweshwaji wa ujenzi wa jengo la upasuaji unaofanywa na mkandarasi Humprey katika kituo hicho cha afya, hivyo kuwakosesha wananchi huduma za matibabu
 Kinana akikagua kituo cha afya Kitunda, sikonge
Kinana akikagua ofisi za Kituo hicho cha afya
Kinana akiingia kukagua jengo la maabara shule ya sekondari  Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akikagua ndani ya jengo la maabara shule ya sekondari  Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimsikiliza mbunge wa Sikonge Saidi Nkumba (kulia) wakati akimweleza baadhi ya kero ambazo wapigakura wa jimbo hilo wangependa zitatuliwe katika suala la huduma za afya. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mganga Mfawadhi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Kitunda.
 Kinana akisomewa taarifa ya ujenzi wa jengo la maabara shule ya sekondari  Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akipata maelezo kuhusu ujenzi wa tanki la maji la maabara shule ya sekondari  Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge, leo
Kinana akikagua nyumba mpya ya mwalimu shule ya sekondari  Kiwele, Kata ya Kitunda, Sikonge
Kinana akisoma vijiji vitavyopata umeme wilayani Sikonge mwaka huu wa fedha.
 Katibu Mkuu  wa CCM, Kinana akihutubia katika mkutano huo leo Mei 15, 2014, ambapo akijibu Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya Kitunda, alielezea kusikishwa kwake na kitendo cha vyama vya ushirika kudaiwa kuwadhulumu bila huruma wakulima wa tumbaku wa Kata hiyo, huku akionyesha kushangazwa kwake na hatua ya  waziri mwenye dhamana na kilimo, Chakula na Ushirika kutotembelea wakulima kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Mapema baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuuliza maswali au kutoa maoni kuhusu kero  walidaikuwa zaidi y  asilimia 64 ya wakulima hawajapewa malipo yao ya mauzo ya tumbaku ya mwaka jana na vyama vya ushirika katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani Tabora. Pia wakulima hao walisema kuwa wanadaiwa zaidi ya sh. bilioni 112 za mauzo hewa ya  pembembejeo.
 Mkulima wa tumbaku katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jinsi viongozi wa vyama vya ushirika walivyosaini mkataba hewa wa pembejeo zenye thamani ya s dola za kimarekani 150.
 Mwakilishi wa wakulima wa tumbaku katika Chama cha Ushirika  cha Tumbaku Mkoa wa Tabora ( WETCO), Lameck Mnyama, akielezea  jinsi viongozi wa ushirika huo wanavyowanyonya wakulima wa zao hilo, wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kitunda uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM ambapo alidai hadi sasa wanaudai ushirika dola za kimarekani 76.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano huo, ambapo aliwataka wananchi kuendelea kuiambiwa CCM matatizo na kero zao kwa kuwa ndiyo chama chenye ridhaa yao ya kuwasimamia haki zao na siyo vyama vingine vya siasa "Kazi yetu CCM ni kuendelea  kuisimamia Serikali ili wananchi wapate haki zao, kwani walioomba kura kwenu ni CCM, hivyo tukikaa kimya  tutalaumiwa , najua kwa ziara hii hapa Kitunda itafanya mambo yabadilike, hiyo ndiyo salmu yetu kwenu, asanteni" alisema  Nape alipokuwa anahutubia katika mkutano huo wa Kata ya Kitunda,
 Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akielezea kwa masikitiko jinsi wakulima wa zao la tumbaku wanavyodhulimiwa mabilioni na viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Sikonge na Mkoa wa Tabora.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo wa Kinana katika Kata ya Kitunda. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply