Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ,Halmashauri ya wilaya ya Uyui imejenga nyumba nane kwa ajili ya watumishi wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uyui huku akipokea maelezo ya mradi wa ujenzi kutoka kwa Mhandisi wa Wilaya Ndugu Stephen Nyanda.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Tabora Ndugu Erasto Chilambo ,Shirika la Nyumba la Taifa linajenga nyumba 50 katika wilaya ya Uyui.
Mradi wa nyumba za makazi za bei nafuu ukiwa kwenye hatua nzuri, nyumba hizi zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa ambapo wananchi na watumishi wa serikali watauziwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka kibao cha kumbukumbu kuonyesha mti alioupanda kwenye shule ya sekondari Lolangulu piaKatibu Mkuu alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara kwenye sekondari hiyo iliyopo kata ya Ilolangulu wilayani Uyui mkoa wa Tabora.