Na Mwandishi,New York
Siku chache baada ya Bw. Lakhdar Brahimi ,Mjumbe wa Maalum wa Katibu Mkuu na Muungano wa Nchi za Kiarabu kujiuzulu na usulushi wa mgogo wa Syria. Wananchi wa Syria wamepata pigo jingine, baada ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kushindwa kupitisha Azimio ambalo lingeipeleka Syria katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC).
Baraza Kuu la Usalama, lilikutana siku ya alhamisi ili kupigia kura rasimu ya Azimio hilo lilowasilishwa na Ufaransa, lakini likashindwa kupita baada ya Urusi na Uchina kupiga kura ya tururfu kupiga azimio hilo.
Wajumbe kumi na tatu kati ya 15 wanaounda Baraza hilo, walipiga kura ya kuunga mkono rasimu hiyo.
Kama Azimio hilo lingepita bila ya kupingwa, basi ICC ingepewa dhamana ya kuchunguza makosa yote ya jinai na uhalifu wa kivita kuanzia mwaka 2011 ulipoanza mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe ambapo zaidi ya watu 100.000 wamepoteza maisha huku mamilioni wakiwa ni wakimbizi.
Katibu Mkuu Ban ki Moon katika salamu zake zilizosomwa kwa niaba yake na Naibu Wake Bw. Jan Eliason, muda mfupi kabla ya kupinga kura, amesema, Baraza Kuu la Usalama na lile la haki za Binadamu yanawajibika kumaliza umwagaji damu na kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa wahanga wa machafuko hayo.
Akaongeza kuwa wananchi wa Syria wanayo haki ya msingi ya kupata haki. Umoja wa Mataifa na wananchama wake wanaowajibu wakuilinda haki hiyo. Kwa kuunga mkono mifumo ambayo itawawajibisha wahalifu wa makosa ya kivita. Na kusisitiza kwamba ni wazi kuwa hakuna upande wowote kati ya zinazopingana ambao hauna kosa.
Akasisitiza kuwa kama wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama wataendelea kuto kukubaliana kuhusu njia zinazoweza kuleta uwajibikaji juu ya uhalifu unaoendelea, hadhi ya chombo hicho muhimu na Umoja wa Mataifa kwa ujumla itaendelea kuathirika.
“ Tunapozungumzia uwajibikaji, lazima tufikirie si tu kwa pande zinazopingana, bali pia ni lazima tuwafikirie na wale ambao wanaendelea kuchochea mgogoro huu na kuendelea kwa madhara yanayotokana na wao kuendelea kutoa silaha kwa wale wanaotenda uhalifu” akasema Ban ki Moon.
Akawasihi wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama, kuweka pembeni tofauti zao na kufanya kazi pamoja ili kuumaliza mgogoro wa Syria pamoja na kutafuta suluhisho la kisiasa.
Kabla ya kuwasilisha wa Azimio hilo mbele ya Baraza Kuu la Usalama, kulikuwa na taarifa za kidiplomasia kuwa waandaji wa Azimio hilo walikuwa wakiziomba nchi ambazo si wajumbe wa Baraza Kuu kuunga mkono hali ambayo si ya kawaida.