Google PlusRSS FeedEmail

CCM YATINGISHA SINGIDA MJINI, MAMIA WAHUDHURIA MKUTANO WA HADHARA VIWANJA VYA PEOPLES

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii, lwenye Viwanja vya Peoples mjini Singida, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo wa Singida.
 Mamia ya wananchi wakishangilia katika mkutano wa CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Peoples mjini Singida
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapungua mkono wananchi alipowasili kwenye Viwanja vya Peoples kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Singida, leo. Pamoja naye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara ) Mwigulu Nchemba na katibu wa NEC itukadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto)
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishuka kwenye Bajaji aliyosafiri nayo katika msafara maalum kutoka Ofisi ya CCM mkoa wa Singida kwenda kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida leo. Nyuma yake ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnayue ambaye pia amesafiri kwa bajaji kwenye msafara huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliokuwa kando ya barabara alipokaribia kuingia kwa babjaji kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida kwenye mkutano huo wa hadhara, Nyuma yake ni Nape akiwa pia kwenye bajaji
  Msafara wa bajaji
Mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji akiwa kwenye bodaboda (kulia) wakati wa msafara kwenda kwenye mkutano huo. (Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

This entry was posted in

Leave a Reply