Google PlusRSS FeedEmail

MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA HANANG AJIKAANGA MBELE YA KINANA NA NAPE MKUTNANONI

 .Kinana na Nape wakimhoji vizuri Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba aeleze alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani analipwa.

Hatua hiyo ya kumhoji ilifikiwa baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto kuwa viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba iliserikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo

This entry was posted in

Leave a Reply