Google PlusRSS FeedEmail

KINANA: VIJANA WASHIRIKISHWE KWENYE MIRADI YA UJENZI YA HALMASHAURI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kaliua kwenye viwanja vya Maliasili ambapo aliwaambia wananchi wao kazi ya CCM ni kutenda na wapinzani kazi yao ni kusema.Katibu Mkuu waliwataka viongozi wa halmashauri kuwashirikisha vijana katika miradi ya ujenzi kwani watakuwa wamepunguza gharama na pia kuwapatia vijana ajira.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akiwasalimia wananchi wa Kaliua na kuwaambia kuwa kuna muhimu ya kutambua sheria za vyama vya ushirika na vyama vya msingi kwani vyama hivyo ni vyama vya hiari kujiunga na si lazima.
 Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi Profesa Juma Kapuya akihutubia wananchi wa jimbo lake na kuwaambia kuwa kamwe hatochoka kuwasemea pale inapomlazimu kusema,amewahakikishia wananchi wake kupata umeme pamoja na minara ya mawasiliano.
 Huu ndio ujumbe ulioandikwa kwenye tshirt mbali mbali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi za CCM Wilaya ya Kaliua.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa pongezi kwa wana CCM wa wilaya mpya ya Kaliua kwa juhudi zao za kujenga ofisi ya CCM katika wilaya hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari ya Ugunga pamoja na Mbunge wa Urambo Magharibi Profesa Juma Kapuya
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka milango katika jengo la Utawala katika shule ya Sekondari Ugunga,Katibu Mkuu aliwapongeza uongozi wa halmashauri kwa uamuzi wa kuatumia mafundi vijana wa kawaida kwani inapunguza sana gharama za ujenzi lakini pia inatoa ajira za kutosha kwa vijana wa maeneo husika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa pongezi kwa viongozi wa halmashauri kwa kujenga soko la Kaliua kwa gharama nafuu .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana na Mbunge wa Urambo Magharibi Profesa Juma Kapuya kufyatua matofali kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Usindi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akinunua ndizi kwenye soko la kijiji cha Kazaroho wilayani Kaliua,Tabora.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara wa soko la kijiji cha Kazaeo wlayani Kaliua,Tabora.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye soko la Kijiji cha Kazaroho akiongozana na Diwani wa kata ya Kaliua Ndugu Haruna Kasele.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiukata muwa kwa goti mara baada ya kuununua .Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wailani ya uchaguzi wa CCM 2010 katika kijiji cha Kazaroho kata ya Kaliua,wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

This entry was posted in

Leave a Reply