Google PlusRSS FeedEmail

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA NZEGA NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA JIMBO LA BUKENE LEO KUFANYA ZIARA WILAYA YA UYUI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Jimbo la Bukene wilayani Nzega ambapo aliwaambia Katiba ni jambo zuri,Katiba ni muhimu kwa nchi lakini si mwarobaini wa matatizo ya wananchi.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Bukene kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi CCM ndio chama pekee kinachoongelea matatizo ya wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe,Fatma Mwassa akiwasalimia wakazi wa Bukene wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Bukene.

Mbunge wa Jimbo la Bukene Selemani Zedi akiwahutubia wananchi wake ambapo aliwaeleza kuwa jimbo hilo karibia litapunguza matatizo ya maji na umeme .Mbunge Zedi alisema miradi mitano ya maji inakamilika muda si mrefu na nguzo za umeme 200 zinahitajika Bukene kuondoa tatizo la Umeme.

Bi.Habiba Juma akirudisha Kadi,Bendera na Fulana ya CUF na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara ulofanyika Bukene .

Wanachama wapya wa CCM wakiinua kadi zao juu wakati wa kula kiapo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,zaidi ya wanachama wapya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.











This entry was posted in

Leave a Reply