Google PlusRSS FeedEmail
Waziri wa Kazi na Ajira Bi.Gaudentia Kabaka akitoa tamko la Serikali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usitishwaji wa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya mawakala binafsi wa huduma za ajira wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa idara ya habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
*****************************
TAMKO LENYEWE HILI HAPA
1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko  toka kwa wadau mbalimbali kuhusu taratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999  (Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002). Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na  ushauri elekezi kwa watafuta kazi,  kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.  Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba  utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na  na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 (Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008).

4. Uchunguzi huu umebaini  athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:
· Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;
· Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume  na  kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;
· Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;
· Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;
· Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.

5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri  wafanyakazi wanaowatafutia kazi.  Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha  wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda  kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.

6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995 na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.

7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya  usajili wa Uwakala kwa KAMISHNA WA KAZI  kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.

8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala  waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.

IMETOLEWA NA
GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)
WAZIRI WA KAZI NA AJIRA
27/01/2014

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA

Waziri wa Kazi na Ajira Bi.Gaudentia Kabaka akitoa tamko la Serikali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usitishwaji wa utaratib... [Read More]

Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA)  wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA  ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
 
 Askari wa hifadhi ya  mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu.
 Picha na Katavi yetu Blog

*********************
Na   Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog.
Mpanda Katavi
 Jumla ya  Askari 96 wa  Shirika  la Hifadhi la Taifa  la Wanyama Pori  (TANAPA) wametimu    mafunzo  ya miezi   mitatu  katika  chuo     kipya   cha wanyama   pori   cha Mlele  kilichopo   Mkoa  wa Katavi  na kutoa  kiapo cha uti  mbele ya Mkurugenzi mkuu  wa TANAPA Allan Kijazi

Askari hao  wa TANAPA walimaliza  mafunzo  hayo  hapo juzi  kwenye chuo  hicho   cha  wanyama Pori  cha Mlele  akiwa ni  mafunzo ya  kwanza  hapa  nchini  kwa TANAPA  kutoa  mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori kupatiwa mafunzo hayo  kabla ya kuanza  kazi

Katika  Risala yao ya  wahitimu wa mafunzo hayo  ya kulinda maliasili  iliyosomwa  na Bruno  Mbunda  walieleza kuwa wamejifundisha  mbinu mbalimbali za kulinda   rasilimali za Taifa  kwa Vitendo   na nadharia

Waliyataja baadhi ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata  waharifu  kumpekua  mharifu  na kutotumia  nguvu  sana  katika kukamata  mharifu    pamoja  na  pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha

Walieleza  katika kipindi hicho cha  mafunzo    wahitimi   hao walifanikiwa kukamata  waharifu  hamsini  wakati  wakifanya  doria  katika maeneo mbambali ya Mbuga ya  Katavi  na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa  Lwafi

Wahitimu hao walieleza kuwa  mafunzo hayo yaliwashirikisha  Askari  99  lakini  watatu kati yao wameshindwa  kuhitimu  zikiwemo  sababu  mbambali  kama  utoro na utovu  wa nidhamu   hari ambayo ilfanya wahitimu  waliomaliza kubaki  96 ambapo kati yao mwanamke  ni mmoja  na wanaume ni  95

Kwa upande wake mkuu wamapori ya akiba  ya  Rukwa Lwafi  Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano  na  ubovu wa miundo  mbinu ya barabaa  na  upungufu  wa  magari pamoja  idadi ndogo ya washiriki  wa mafunzo kwa wanawake na ufinyu  wa bajeti

Nae  Mkurugenzi  wa Hifadhi  na Ikolojia  Martini  Loibook  alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata yanaumuhimu  sana  hasa kutokana na changamoto  zinazoikabili nchi  yetu  inayokabiliwa na wimbi la ujangili

Pia Mkurugenzi wa  utumishi   na utawalla   wa TANAPA  Witnes Shoo  aliwataka wahitimu hao  kufanya kazi  kwa uaminifu  kwa kujituma  na  wawe na didamu  na  wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi

Mkurugenzi Mkuu   wa TANAPA  Allan Kijazi  aliwaasa wahitimu hao  wahakikishe wanafanya kazi  zao kwa uaminifu mkubwa  hasa  katika shughuli zao  katika kupambana kukomesha ujangili 
Aliwataka kutojihusisha  na masuala ya ujangiri na badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo ndani ya nchi na nje ya nchi

Alisema wapo baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote yule au watu

96 WAMALIZA MAFUNZO KUPAMBANA NA MAJANGILI

Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoan... [Read More]

Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza, wakati wa kikao chake cha ndani na Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Tandika, Januari 26, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi. Baadhi ya walioketi meza kuu kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalumu Temeke, Mariam Mtemvu na Diwani wa Tandika, Zena Mgaya. Baadhi ya kero alizofuatilia ni pamoja na  hali ya barabara katika baadhi ya maeneo katika kata hiyo ambapo Mbunge huyo aliahidi kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Chama itahakikisha barabara zilizo katika hali mbaya zinapitika kwa ubora unaostahili ikiwemo wa lami.
Diwani wa Kata ya Tandika Zena Mgaya (kushoto) atoa maelezo kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo. Wengine waliosimama ni madiwani na wenyeviti wa mitaa.
 DIWANI wa Viti Maalum, Temeke Dar es Salaam, Mariam Mtemvu akifafanua jambo, wakati wa kikao cha Mbumbe wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) na Halmashauri Kuu ya Kata ya Tandika kilichofanyika Ofisi ya CCM Kata hiyo, jana, kuzungumzia kero na hali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo. Katikati ni Diwani wa Kata hiyo, Zena Mgaya
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Tandika wakiwa kwenye kikao hicho na Mtemvu.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MTEMVU AKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, KATA YA TANDIKA, AAHIDI BARABARA ZILIZOSALIA KUPITIKA KWA VIWANGO BORA VIKIWEMO VYA LAMI

Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza, wakati wa kikao chake cha ndani na Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Tandika, Januar... [Read More]

DK. BILAL KATIKA HARAMBEE KUCHANGISHA FEDHA ZA UJENZI WA UKUMBI WA MIKUTANO WA KANISA LA MT. PETER, OYSTERBAY

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wakati wa Ibada maalum ya Hara... [Read More]


Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.

SHULE ya Sekondari ya Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi shuleni. Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto ya utandawazi. Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho wanahudhuria masomo yao.
Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia . 
Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia 
Baadhi ya wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili suleni hapo walizawadiwa katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri  akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi hao. 
Baadhi ya wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili suleni hapo walizawadiwa katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi haoMgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri  akilishwa keki na mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayo. 
Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akilishwa keki na mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayoMgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri (kulia) akilishwa keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kwenye hafla hiyo. 
Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri (kulia) akilishwa keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kwenye hafla hiyo.Wanafunzi wa Kidato cha Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji fedha kwenye hafla hiyo. 
Wanafunzi wa Kidato cha Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji fedha kwenye hafla hiyoChuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayo. Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayo.Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.

SEKONDARI YA LOYOLA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE

Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Baadhi ya wageni w... [Read More]

*NI GARI SITA AINA YA SUZUKI CARRY,  *BAJAJ KUMI, *PIKIPIKI 19 AINA YA BOXER, *PIKIPIKI YA MZIGO AINA YA TOYO, *VIFAA VYA UMEME VYA USEREMALA, *MBAO, *VIFAA VYA STATIORIES NA VIFAA VYA SHOOTING CAMERA
Vifaa vikiwa tayari kukabidhiwa kwa vikundi hivyo vya Vicoba chini ya PFT
 Baadhi ya sare zilizovaliwa na wadau zilikuwa na ujumbe huu
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwezeshaji na Uwekezaji. Dk. Mary Nagu (kushoto) akiwasili ukumbini huku akiwa na Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, kwa ajili ya kuvigawia vifaa mbalimbali  vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimtambulisha kwa waziri Nangu, Mwezeshaji wa VICOBA walioko chini ya PFTJohannes Linde wakati waziri Nagu alipowasili ukumbini.
 Wanavikundi wakilipuka kwa shamrashamra wakati wa mapokezi ya waziri Nagu ukumbini
 Cherekochereko na mabango
 Kina mama wa Vicoba wakifurahi
 Mama Mtemvu na Mwanae wakiwa kwenye hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakiwa wamekaa baada ya mapokezi
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza kwenye hafla hiyo
 Msanii Snura Mushi maarufu kwa jila na Majanga, akikonga nyoyo za wanavicoba wakati wa hafla hiyo
 Snura Majanga akionyesha umahiri wake mbele ya wana-Vicoba
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkabidhi Waziri Nagu hati maalum ya shukrani kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na mchango alioutoa wa sh. milioni 50 kwa PFT. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo na Jamii Jinsia na Watoto Pindi Chana.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abbas Mtemvu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi gari kwa moja wa viongozi wa PFT.
Masiriamali ambaye ni mwanachama wa moja ya vikundi cya Vicoba vilivyopo chini ya PFT akiwa kazini wakati wa hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakichangamkia fomu za NSSF za Matibabu
 Wanakikundi cha Vicoba wakiwa kwenye gari lao baada ya kukabidhiwa
 Mweneyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wakati wa hafla hiyo
Mtembu akiwa na Kina Juma Nature na Snura Majanga ambao walitumbuiza kwenye hafla hiyo. KUPATA MAELEZO KAMILI KUHUSU HAFLA HIYO NA PFT>BOFYAGA HAPA

VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOPO CHINI YA POVERTY FIGHTING TANZANIA (PFT) INAYOSIMAMIWA NA MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU VYAKABIDHIWA VIFAA VYA MILIONI 192.3

*NI GARI SITA AINA YA SUZUKI CARRY,  *BAJAJ KUMI, *PIKIPIKI 19 AINA YA BOXER, *PIKIPIKI YA MZIGO AINA YA TOYO, *VIFAA VYA UMEME VYA USEREMAL... [Read More]

  Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo. Picha na OMR

  Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono. Picha na OMR
 Rais Kikwete akitoa pole kwa waombolezaji
 Waombolezaji wakiomba dua wakati wa mazishi hayo
Waombolezaji kina mama wakiwa msibani

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE LEO

  Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dun... [Read More]