Google PlusRSS FeedEmail

MTEMVU AKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, KATA YA TANDIKA, AAHIDI BARABARA ZILIZOSALIA KUPITIKA KWA VIWANGO BORA VIKIWEMO VYA LAMI

Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza, wakati wa kikao chake cha ndani na Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Tandika, Januari 26, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi. Baadhi ya walioketi meza kuu kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalumu Temeke, Mariam Mtemvu na Diwani wa Tandika, Zena Mgaya. Baadhi ya kero alizofuatilia ni pamoja na  hali ya barabara katika baadhi ya maeneo katika kata hiyo ambapo Mbunge huyo aliahidi kuwa Ofisi yake kwa kushirikiana na Chama itahakikisha barabara zilizo katika hali mbaya zinapitika kwa ubora unaostahili ikiwemo wa lami.
Diwani wa Kata ya Tandika Zena Mgaya (kushoto) atoa maelezo kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo. Wengine waliosimama ni madiwani na wenyeviti wa mitaa.
 DIWANI wa Viti Maalum, Temeke Dar es Salaam, Mariam Mtemvu akifafanua jambo, wakati wa kikao cha Mbumbe wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) na Halmashauri Kuu ya Kata ya Tandika kilichofanyika Ofisi ya CCM Kata hiyo, jana, kuzungumzia kero na hali ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo. Katikati ni Diwani wa Kata hiyo, Zena Mgaya
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Tandika wakiwa kwenye kikao hicho na Mtemvu.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

This entry was posted in

Leave a Reply