Google PlusRSS FeedEmail

MTEMVU AKABIDHI MADAWATI KWA SHULE ZOTE ZA MSINGI JIMBONI MWAKE

 MBUNGE wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, akizungumza wakati Mfuko wa Jimbo hilo ulipokabidhi madawati 500 kwa ajili ya shule za msingi za Kata 13 katika jimbo hilo.
      Madawati hayo yenye thamani ya Sh. milioni 67.5, ameyakabidhi kwa madiwani wa kata hizo, katika hafla iliyofanyika leo, Januari 17, 2014, katika karakara ya Chuo cha VETA, Chang'ombe. Aliyekaa pembezoni mwake ni Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Keko Magurumbasi, Aziz Ally ambaye anasoma darasa la saba katika shule hiyo ambayo pia imepatiwa madawati.
 Ofisa Elimu wa Manispaa wa Temeke, Dar es Salaam, Hononina Mumba akitoa shukrani zake wakati wa makabidhiano ya madawati hayo ambayo inakisiwa kila shule itapata madawati 45.
 Mtemvu akimtazama Azizi wa Shule ya Mnsingi Keko Magurumbasi, wakati akiandika jina lake, huku amekaa naye kwenye dawati wakati wa hafla ya kukabidhi madawati hayo leo.
 Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi Keko Magurumbasi, Azizi Ally, akitoa shukrani kwa naba ya wanafunzi wenzake kwa msaada wa madawati yaliyotolewa na mbunge Mtemvu (kulia)
 Baadhi ya madawati yaliyotolewa na Mtemvu.
Mtemvu (wanne kulia) akiwa na madiwani wa Kata za Temeke, baada ya kukabidhi madawati leo.

This entry was posted in

Leave a Reply