Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya watembeaji kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar leo January 5, 2014 (Picha na Ikulu).
ZANZIBAR, Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania kuendelea kutoa maoni yao kuhusu aina ya Katiba wanayoitaka akisisitiza kuwa siyo dhambi kwa watu kutoa maoni yanayopingana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa tofauti na maneno yasiyokuwa ya kweli ambayo yamekuwa yanasambazwa na baadhi ya watu kuwa kazi ya Katiba imekamilika, bado Katiba mpya haijapatikana na wananchi wanaombwa kuendelea kutoa mapendekezo na maoni yao.
Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo kuhusu mchakato wa kusaka Katiba mpya nchini wakati alipokuwa anapokea Matembezi ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe iliyofanyika kwenye Viwanja vya Maisala, mjini Zanzibar, leo, Jumapili, Januari 5, 2014.
Akizungumza baada ya risala za vijana ambazo zimesisitiza msimamo wa CCM kuhusu aina ya Muungano ambao chama hicho kimeutetea tokea kuundwa kwake, Rais Kikwete amewaambia wananchi:
“Tunataka Katiba ya watu wote, siyo Katiba ya kikundi ama vikundi vya watu. Hivyo, toeni maoni na mapendekezo yenu bila hofu wala woga kuhusu aina ya Katiba ambayo mnaitaka. Ni haki yenu kutoa mawazo yenu bila hata kujali mtu mwingine anasema ama kufikiria nini. Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake na hata kutofautiana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba siyo dhambi.”
Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wanaweza kutoa maoni yao kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na kupitia kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambao wote watakuwa ni wajumbe wa Bunge la Katiba.
Jumatatu iliyopita, Desemba 30, mwaka jana, 2013, Tume ya Katiba iliyoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mstaafu, Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba ilimkabidhi Rais Kikwete Ripoti ya Tume hiyo ambayo ni pamoja na Rasimu ya pili ya mapendekezo ya Katiba mpya.
Ameongeza Rais Kikwete: “Kuna watu wameanza kupotosha wengine kwa kusema kuwa kazi ya Katiba imekamilika. La hasha. Tume imetoa mapendekezo ambayo yanatakiwa kujadiliwa na kuamuliwa ipasavyo na Bunge la Katiba. Bunge hilo lina mamlaka ya kuamua linavyoona inafaa kwa kifungu chochote cha mapendekezo ya Tume.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Itumieni vizuri fursa hii kutoa maoni yenu ili tupate Katiba inayotupatia Muungano imara na nchi ya kisemokrasia na inayozingatia na kuheshimu haki za binadamu. Tupate Katiba ambayo itaendelea kuifanya nchi yetu salama, tulivu na yenye kupata maendeleo shirikishi na kunufaisha wote.”
Katika hotuba yake, Rais Kikwete pia amewakumbusha vijana historia ya vyama vya ukombozi wa TANU na ASP, historia ya mahusiano kati ya vyama hivyo na watu wa Bara na Visiwani na chimbuko la Muungano wa Tanzania ambao ulizaliwa Aprili 26, 1964 na mchango wa Mapinduzi ya Zanzibar katika kuzaliwa kwa Muungano huo.
“Vile vile inatupasa tukumbuke kuwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ndiyo yalikuwa chachu ya Muungano wa nchi zetu mbili. Huweza kuzungumzia Muungano bila Mapinduzi. Kama Mapinduzi yasingefanyika Muungano usingekuwepo. Muungano ni mtoto wa Mapinduzi.”
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Tanzania Visiwani amerejea Dar es Salaam mchana wa leo.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2014
(556)
-
▼
January
(81)
- KINANA AKUTANA NA BODA BODA WA MKOA WA MBEYA
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA...
- MAKAMU MWENYEKITI CCM (BARA) NA KATIBU MKUU WAWASI...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAWAZIRI WA K...
- WAZIRI MKUCHIKA AELEZA SABABU ZA TANZANIA KUSHUKA ...
- KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANI...
- MABASI YA MWENDO KASI YAANZA MAJARIBIO JIJINI DAR
- NAPE ATEMBELEA SOKO LA SIDO MWANJELWA MJINI MBEYA...
- MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM YAPAMBAMOTO
- REGINALD MENGI AKUTNA NA KINANA LEO
- RAIS KIKWETE AAMRISHA JESHI KUSIMAMIA UTOAJI HUDUM...
- DK. SHEIN AMNADI RASMI MGO MBEA WA CCM JIMBO LA KI...
- MWANDISHI WA HABARI LEO KILIMANJARO, ARONLD SWAI, ...
- SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA...
- 96 WAMALIZA MAFUNZO KUPAMBANA NA MAJANGILI
- MTEMVU AKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, KATA YA...
- DK. BILAL KATIKA HARAMBEE KUCHANGISHA FEDHA ZA UJE...
- SEKONDARI YA LOYOLA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE
- VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOPO CHINI YA POVERTY FIGH...
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE...
- TANZANIAN YOUTH, DOREEN NONI AT THE WORLD ECONOMIC...
- NAPE: MAWAZIRI TULIWANYOOSHEA VIDOLE ILI HATUA MAD...
- MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE SAIDI BWANAMDOGO KUM...
- AJALI ILIYOUA WANAFUNZI WANE NA KUJERUHI 47 WAKIKI...
- BRAVO YAPELEKE VIJANA WENGINE WANNE KUFANYAKAZI DUBAI
- MBUNGE WA CHALINZI SAIDI BWANAMDOGO AMEFARIKI DUNI...
- MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA MZEE YUSUFU MAK...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAPYA
- MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU APATA CHAKULA CHA JI...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI MTEULE...
- MAMIA WAMZIKA DEUSDEDIT MTAMBALIKE
- RAIS KIKWETE ATANGAZA MABADILIKO YA BARAZA LAKE L...
- KAMPUNI YA WORLD BUZ YAELEZA NJIA MBADALA KUPUNGUZ...
- NAPE AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA MAGOMENI B...
- MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA ...
- RAIS KIKWETE ATEUA MATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA MI...
- PINDA AKAGUA MAREKEBISHO YA UKUMBI WA BUNGE KWA AJ...
- DEREVA WA BODABODA AUAWA KINYAMA TARIME-RORYA
- KALENDA YA VIKAO VYA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MWAKA ...
- KIONGOZI WA JUMUIA YA KIROHO YA BOHRA DUNIANI AFAR...
- TAARIFA YA CAG YAMNG'OA MEYA MANISPAA YA BUKOBA, A...
- NEW YORK YAJADILI UFANISI WA SHERIA ZINAZODHIBITI ...
- MTEMVU AKABIDHI MADAWATI KWA SHULE ZOTE ZA MSINGI ...
- WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA MAAFA YA MAUAJI YA WAKU...
- MBUNGE WA CHALINZE ALAZWA ICU MUHIMBILI
- RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MW...
- WAKULIMA WATESEKA NA WAUZAJI DAWA BANDIA ZA KILIMO
- WABAMBWA NA MISOKOTO 5,000 ARUSHA
- RAIS JAKAYA KIKWETE WAJULIA HALI MZEE MSUYA NA WAZ...
- KAMATI KUU YAMTEUA MAHMOUD THABIT KOMBO KUWA MGOMB...
- NJAMA ZA KUNDI LA WAASI LA M23 KUJIPANGA UPYA ZAFI...
- CHADEMA YATABIRIWA KUINGIA UCHAGUZI MKUU 2015 IKIW...
- KCC YA UGANDA YATWAA KOMBE LA MAPINDUZI BADA YA KU...
- KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MJINI ZANZIBA...
- CHADEMA, CUF WAKIMBIWA DAR
- UN RESIDENT COORDINATOR BIDS FAREWELL TO ZANZIBAR
- BALOZI WA TANZANIA MAREKANI AMTEMBELEA DEWJI
- MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YAFANA ZANZIBAR
- MTEMVU ATEMBELEA WAPIGAKURA WAKE KATA YA KILAKALA,...
- SALMIN AMOUR NA AMANI KARUME WATUNUKIWA NISHANI NA...
- RAIS KIKWETE AWAANDALIA MABALOZI SHEREHE YA KUUKAR...
- PROF ELIESANTE AMALIZA ZIARA MKOA WA PWANI
- SENSA: TEMBO WAPUNGUA KWA ASILIMIA 66 TANZANIA
- MWENYEKITI WA CCM MORO ANG'AKA OLE SENDEKA KUWA MW...
- UZINDUZI WA TAASISI YA MWAHARAKATI BIBI BINTI SAAD
- KAMATI MAALUM YA CCM YAKUTANA MJINI ZANZIBAR
- BENKI KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA KUMBUKUMBU Y...
- ZITTO AIBWAGA CHADEMA MBELE YA TUNDU LISU MAHAKAMA...
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA MAZISHI YA DK. MGIMWA, ...
- NDEJEMBI ASEMA SERIKALI MBILI NDIYO NGUZO PEKEE IM...
- SAKATA LA ZITTO KABWE NA UONGOZI WA CHADEMA LEO MA...
- JK: SIYO DHAMBI KUTOFAUTIANA NA MAPENDEKEZO YA TUM...
- RAIS KIKWETE NA MAKAMU WAKE WAONGOZA KUAGA MWILI W...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBO...
- MANGULA AZIDI KUWAWAKIA WANA-CCM WANAOJINADI KABLA...
- DC KANGOYE AWAFUNDA VIJANA KULETA MAGEUZI MAKUBWA ...
- ZITTO AMBWAGA TUNDULISU MAHAKAMA KUU, NI KATIKA OM...
- MWILI WA DK. MGIMWA KUWASILI DAR ES SALAAM, KESHOK...
- VIDEO YA SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI Y...
- WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA, RAIS...
-
▼
January
(81)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.