Google PlusRSS FeedEmail

RAIS KIKWETE NA MAKAMU WAKE WAONGOZA KUAGA MWILI WA DK. MGIMWA DAR, WAZIRI MKUU APOKEA MWILI IRINGA

 Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kwenda mkoani Iringa kwa maziko.
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dk. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kwenda.
 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nayerere akitoa heshima za mwisho
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
 Spika wa Bunge Anna Makinda akitoa heshima za mwisho
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Mgimwa mjini Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk. Mgimwa.
 Wananchi mbalimbali waliofika kutoa heshima za mwishi kwa mwili wa Dk Mgimwa leo
 Viongozi kutoka baadhi ya vyama vya siasa, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mabatia na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Dk. Mgimwa.
 Waombolezaji kwenye kuaga mwili wa Dk, Mgimwa
Waombolezaji wakiwa Karimjee kuaga mwili wa Dk Mgimwa
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jane Kakingo Mgimwa, mjane wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya mwili wa marehemu kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli Iringa  Desemba 5, 2014 kwa ajili ya mazishi  yanayotarajiwa kufanyika kijijini Magunga Desemba  6, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati mwili wa  aliyekuwa  Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati ulipowasili kwenye uwanja wa ndege  wa Nduli Iringa Desemba 5,2014 kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika  Desemba 6, 2014 kijijini  Magunga. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

This entry was posted in

Leave a Reply