Google PlusRSS FeedEmail

MWENYEKITI WA CCM MORO ANG'AKA OLE SENDEKA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Inocent Karogeries Akizungumza katika mkutano wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Morogoro RCC juu ya tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji mkoa wa Morogoro, leo, mjini Morogoro.

MOROGORO,Tanzania
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Inocent Karogeries amedai kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji, Mbunge wa Simanjiro, Ole Sendeka hana sifa kutumikia nafasi hiyo kwa sababu ni miongoni mwa wafugaji wakubwa hapa nchini. 

Kalogeriesametoa madai hayo huku akimlaumu Spika wa Bunge, Anna Makinda kwa kukubali Sendeka kuwekwa na Bunge katika nafasi hiyo. 

Alisema hayo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Morogoro RCC iliofanyika mjini Morogoro.

Alisema kuwa wabunge wanatambua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo na Mifugo ni mbunge wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Profesa Petter Msolwa ambaye ndiye alipaswa kuwa Mwenyekiti wa kamati teule ya kushugulikia migogoro hiyo ya wakulima na wafugaji.

‘’ Tumeshangaa kuona spika amemchagua Ole Sendeka kuwa Mwenyekiti wa kamati teule wakati yeye ni miongoni mwa wafugaji wakubwa hapa nchini’’ alisema

Alisema kuwa katika migogoro kama hiyo ili haki itendeke ni lazima apatikane mtu ambaye hafungamani na upande wowote ili aweze kutenda haki wakati wa maamuzi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kuwa kilichotokea katika utekelezaji wa kamati hiyo kwa mkoani wa Morogoro ni kwamba kamati hiyo haikushirikisha kiongozi hata mmoja wa chama wala wa Serikali na badala yake walikwenda wenyewe jambo ambalo linaashiria kutofanya kazi zake kikamilifu kwani wenyewe wanaojua vyanzo vya migogoro ya maeneo husika hawakushirikishwa.

‘’ Sisi kama viongozi wa Morogoro Kusini tulijipanga kushirikia vizuri katika ziara hiyo lakini chaajabu kamati hiyo ilipofika iliwakataa, mimi kama mbunge wa jimbo la Morogoro kusini nililazimisha nikaongozana nao lakini sikupewa hata nafasi ya kusema chochote badala yake ni kujitambulisha tu’’ Alisema

Alisema kuwa baadhi ya viongozi wakubwa hapa nchini wamekuwa wakimiliki mifugo na  kwamba ndio wanakwamisha zoezi la kuwaondoa wafugaji kwa kuandika ujumbe kwa watendaji ili waache mifugo yao.

Hata hivyo mbunge huyo alisema kuwa kama mkoa  kwa kutumia kamati hiyo teule wanahakika kuwa tatizo la migogoro ya ardhi haiwezi kutatuliwa na badala yake kuna kila sababu ya kuhakikisha wanaainisha mashamba makubwa ambayo ni mapori na kwenda kwa Rais ili ayafute.

‘’ Mimi nawambie watendaji kwa zoezi hili kwa kuwa mmegusa maeneo ya wakubwa hao tegemeeni mara baada ya taarifa ya tume hiyo kusoma hapo mwezi juni mwaka huu, tegemeeni kuhukumiwa  katika kazi zenu, lakini niwahakikishie kazi nzuri mmefanya sisi kama CCM tutahakikisha tunawatetea hadi mwsiho’, Alisema .
Mmoja wa watoa mada katika mkutano huo akiwasilisha bajeti ya mkoa wa Morogoro kwa mwaka 2014.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro Azizi Abood akisoma kitabu cha bajeti ya mkoa wa Morogoro katika kikao hicho.

 Viongozi wa wilaya ya Mvomero wakifutilia kwa makini mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hasani Masala akiongea katika mkutano huo .
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akizungumzia hoja ya wakulima kuonewa na wafugaji na kulaumu wabunge wa Morogoro walinyamaza kimya katika kikao cha bunge.

This entry was posted in

Leave a Reply