Vijana wa UVCCM toka bara na visiwani wakitembea kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi makao makuu ya UVCCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kuhamasisha Serikali mbili.(Picha zote na Zainul Mzige).
*AWATAKA VIJANA KWENDA KWA WANANCHI KUWAELIMISHA UMUHIMU WA SERIKALI MBILI
*ASEMA KEO ZA MUUNGANO ZINAZUNGUMZIKA
Na Damas Makangale, MOblog
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi amewataka vijana wa CCM kwenda kwa wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na serikali mbili katika kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na wanamatembezi wa UVCCM kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar leo mchana katika makao makuu UVCCM jijini Dar es Salaam , Ndugu Ndejembi amesema serikali ndio nguzo kuu ya kudumisha muungano kati ya bara na visiwani.
“Tunataka vijana waelewe kwamba serikali mbili ndio njia kuu ya kudumisha muungano wetu kwa kuwa waasisi wa muungano Mzee Karume na Baba wa taifa Nyerere walio mbali katika kuchanganya mchanga wan chi hizi mbili na ndio njia bora katika kudumisha upendo, undugu na amani katika nchi yetu,” amesema Ndugu Ndejembi.
Mjumbe huyo wa NEC taifa alilisitiza kwamba mapendekezo ya tume ya mabadiliko ya katiba ya serikali tatu itawagawa watanzania kati ya bara na visiwani na ni serikali mbili ndio itawaleta karibu watanzania.
Ndejembi aliongeza kuwa serikali tatu siyo suluhisho la kero mbalimbali za muungano bali matatizo ya sasa ndani ya muungano yanaweza kushughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa maslahi mapana ya taifa.
Mjumbe huyo wa NEC alisisitiza kwamba rasimu ya katiba ya pili iliyowasilishwa hivi karibuni na Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba katika kipengele cha maadili na miiko ya uongozi, CCM haina matatizo kwa maadili ya viongozi kuwekwa katika katiba kwa maslahi ya taifa.
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mkoa bara na visiwani mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi aliyesoma risala ya wanamatembezi amesema takribani vijana 600 walishiriki matembezi hayo ambayo kati yao 35 walitoka katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.
“tunaunga mkono, kupongeza na kuenzi mapinduzi ya mwaka 1964, kwani mapinduzi hayo ni alama ya ukombozi wa wanyonge waliokandamizwa, kuonewa na kudhulumiwa haki na utu wao,” amesema Yaredi
Amesema kuwa vijana wanatambua kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 ndio chachu ya muungano na kwamba vijana ndio tunu ya taifa na watalinda muungano kwa nguvu zao zote.
Wanamatembezi wakiwa wamebeba picha za Waasisi wa Muungano na Viongozi wa sasa wa bara na visiwani.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea maandamano hayo.
Pichani juu na chini ni MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha za waasisi wa Taifa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha ya Dkt. Ali Mohamed Shein Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mikoani bara na visiwani wakiwa na bendera za Chama na Taifa.
Sehemu ya vijana wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC), Deo Ndejembi, wakati akitoa hotuba fupi baada ya kupokea matembezi hayo ya vijana.
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi, akisoma risala ya vijana kwa Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi kuhusu msimamo wa vijana wa serikali mbili katika kulinda muungano wa Bara na Visiwani.
Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi, akimpongeza Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi kwa risala nzuri.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akizungumza na wanamatembezi kutoka UVCCM bara na visiwani kuhusu umuhimu wa Vijana kutoa Elimu na kuhamasisha umuhimu wa Serikali mbili kama njia bora ya kulinda Muungano wa Tanzania.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi akisalimiana na baadhi ya vijana walishiriki matembezi ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar waliowasili leo kutoka visiwani Zanzibar.
Hilda Oddy, Katibu kata ya Ubungo, Uhamasishaji (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wengine wa UVCCM.