Google PlusRSS FeedEmail

MTEMVU ATEMBELEA WAPIGAKURA WAKE KATA YA KILAKALA, TEMEKE,

 Vijana wa eneo la Kilakala, jimbo la Temeke Dar es Salaam, wakiwa wamelizonga gari la mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtemvu, ili asikilize kero zao walipokuwa katika ziara ya kusikiliza kero za wapigakura wake, na utekelezaji wa ilani ya CCM, katika jimbo lake leo
 Mariam Ramadhani akimkabidhi risala Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, kabla ya mbunge huyo kuzindua shina la Wajasiriamali wa UVCCM, Mtaa wa Mazegela, Kata ya Kilakala jimboni humo leo
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akifungua shina hilo
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akisalimia wazee wa Kilakala kabla ya kuzungumza nao katika kata hiyo leo
 Diwani wa Viti Maalum, Mariam Abbas Mtemvu, akisalimia wazee alipofika na mumewe kwenye kuzungunza na Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Kilakala leo
 Ofisa Mtendaji Kata ya Kilakala, Temeke, Peter Makoye akisoma taarifa ta utekelezaji wa maendeleo katika kata hiyo, wakati Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alipozungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Kilakala jimboni humo.
Mtemvu akizungumza na Halmashauri ya CCM ya Kata hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kata hiyo, Amir Salum na wengine kutoka kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Temeke Amina Mtemvu na Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Temeke, Masumo.

This entry was posted in

Leave a Reply