Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Aben Mgode akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto 5000 pamoja na baadhi ya magunia 16 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokamatwa kutokana na misako mbalimbali iliyofanyika mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi, Polisi Arusha
Watu saba wakiwemo wanawake wawili wamekamatwa na misokoto 5,000 ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilo 47.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Mti mmoja lililopo wilaya ya Monduli.
Mafanikio hayo yalitokana na msako shtukizi uliofanywa na jeshi la polisi Mkoani hapa kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni baada ya kufanya upekuzi katika magari mbalimbali na kupata madawa hayo ambayo yalikuwa yanasafirishwa na watuhumiwa hao kupitia magari ya abiria yaliyokuwa yakielekea Manyara, Singida, Dodoma na Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas watuhumiwa hao walikuwa wanayahifadhi madawa hayo kwenye mifuko ya “plastic” ili yasitoe harufu na kisha kuweka kwenye mabegi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Godwina Munisi (31) Mkazi wa Sombetini , Mwajuma Kingu (48) Mkazi wa Mbauda, Fidelis Joseph (48) Mkazi wa Ngarenaro, Selemani Ally (34) Mkazi wa Olmatejoo, Omari Ally (25) Mkazi wa Babati Mkoani Manyara Kasimu Ayubu (39) Mkazi wa Tarakea Rombo Mkoani Kilimanjaro na Yasini Talian (40) Mkazi wa Ngarenaro.
Kamanda Sabas alisema kwamba watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Wakati huo huo katika msako unaoendelea wilayani Longido, jumla ya magunia 16 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yamepatikana katika eneo la kijiji cha Leboo baada ya askari Polisi kufanya msako na kufanikiwa kupata magunia hayo 16 yaliyokuwa yanasafirishwa .
Kamanda Sabas alisema kwamba, askari hao walikuwa wanafanya msako usiku na mara baada ya watuhumiwa hao kugundua kuwa wanafuatiliwa walitelekeza magunia hayo 16 na kukimbia.
Inasemekana kwamba watuhumiwa hao walikuwa wanatumia wanyama aina ya Punda kusafirishia madawa hayo ambapo magunia yalikuwa yamefungwa mawili mawili.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoani hapa bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao ili wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2014
(556)
-
▼
January
(81)
- KINANA AKUTANA NA BODA BODA WA MKOA WA MBEYA
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA WAZIRI MKUU WA...
- MAKAMU MWENYEKITI CCM (BARA) NA KATIBU MKUU WAWASI...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAWAZIRI WA K...
- WAZIRI MKUCHIKA AELEZA SABABU ZA TANZANIA KUSHUKA ...
- KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANI...
- MABASI YA MWENDO KASI YAANZA MAJARIBIO JIJINI DAR
- NAPE ATEMBELEA SOKO LA SIDO MWANJELWA MJINI MBEYA...
- MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM YAPAMBAMOTO
- REGINALD MENGI AKUTNA NA KINANA LEO
- RAIS KIKWETE AAMRISHA JESHI KUSIMAMIA UTOAJI HUDUM...
- DK. SHEIN AMNADI RASMI MGO MBEA WA CCM JIMBO LA KI...
- MWANDISHI WA HABARI LEO KILIMANJARO, ARONLD SWAI, ...
- SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA...
- 96 WAMALIZA MAFUNZO KUPAMBANA NA MAJANGILI
- MTEMVU AKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM, KATA YA...
- DK. BILAL KATIKA HARAMBEE KUCHANGISHA FEDHA ZA UJE...
- SEKONDARI YA LOYOLA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA KIKE
- VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOPO CHINI YA POVERTY FIGH...
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE...
- TANZANIAN YOUTH, DOREEN NONI AT THE WORLD ECONOMIC...
- NAPE: MAWAZIRI TULIWANYOOSHEA VIDOLE ILI HATUA MAD...
- MAZISHI YA MBUNGE WA CHALINZE SAIDI BWANAMDOGO KUM...
- AJALI ILIYOUA WANAFUNZI WANE NA KUJERUHI 47 WAKIKI...
- BRAVO YAPELEKE VIJANA WENGINE WANNE KUFANYAKAZI DUBAI
- MBUNGE WA CHALINZI SAIDI BWANAMDOGO AMEFARIKI DUNI...
- MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA MZEE YUSUFU MAK...
- RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAPYA
- MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU APATA CHAKULA CHA JI...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI MTEULE...
- MAMIA WAMZIKA DEUSDEDIT MTAMBALIKE
- RAIS KIKWETE ATANGAZA MABADILIKO YA BARAZA LAKE L...
- KAMPUNI YA WORLD BUZ YAELEZA NJIA MBADALA KUPUNGUZ...
- NAPE AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA MAGOMENI B...
- MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA ...
- RAIS KIKWETE ATEUA MATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA MI...
- PINDA AKAGUA MAREKEBISHO YA UKUMBI WA BUNGE KWA AJ...
- DEREVA WA BODABODA AUAWA KINYAMA TARIME-RORYA
- KALENDA YA VIKAO VYA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MWAKA ...
- KIONGOZI WA JUMUIA YA KIROHO YA BOHRA DUNIANI AFAR...
- TAARIFA YA CAG YAMNG'OA MEYA MANISPAA YA BUKOBA, A...
- NEW YORK YAJADILI UFANISI WA SHERIA ZINAZODHIBITI ...
- MTEMVU AKABIDHI MADAWATI KWA SHULE ZOTE ZA MSINGI ...
- WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA MAAFA YA MAUAJI YA WAKU...
- MBUNGE WA CHALINZE ALAZWA ICU MUHIMBILI
- RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUUAGA MW...
- WAKULIMA WATESEKA NA WAUZAJI DAWA BANDIA ZA KILIMO
- WABAMBWA NA MISOKOTO 5,000 ARUSHA
- RAIS JAKAYA KIKWETE WAJULIA HALI MZEE MSUYA NA WAZ...
- KAMATI KUU YAMTEUA MAHMOUD THABIT KOMBO KUWA MGOMB...
- NJAMA ZA KUNDI LA WAASI LA M23 KUJIPANGA UPYA ZAFI...
- CHADEMA YATABIRIWA KUINGIA UCHAGUZI MKUU 2015 IKIW...
- KCC YA UGANDA YATWAA KOMBE LA MAPINDUZI BADA YA KU...
- KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MJINI ZANZIBA...
- CHADEMA, CUF WAKIMBIWA DAR
- UN RESIDENT COORDINATOR BIDS FAREWELL TO ZANZIBAR
- BALOZI WA TANZANIA MAREKANI AMTEMBELEA DEWJI
- MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YAFANA ZANZIBAR
- MTEMVU ATEMBELEA WAPIGAKURA WAKE KATA YA KILAKALA,...
- SALMIN AMOUR NA AMANI KARUME WATUNUKIWA NISHANI NA...
- RAIS KIKWETE AWAANDALIA MABALOZI SHEREHE YA KUUKAR...
- PROF ELIESANTE AMALIZA ZIARA MKOA WA PWANI
- SENSA: TEMBO WAPUNGUA KWA ASILIMIA 66 TANZANIA
- MWENYEKITI WA CCM MORO ANG'AKA OLE SENDEKA KUWA MW...
- UZINDUZI WA TAASISI YA MWAHARAKATI BIBI BINTI SAAD
- KAMATI MAALUM YA CCM YAKUTANA MJINI ZANZIBAR
- BENKI KUU YA TANZANIA YATOA SARAFU YA KUMBUKUMBU Y...
- ZITTO AIBWAGA CHADEMA MBELE YA TUNDU LISU MAHAKAMA...
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA MAZISHI YA DK. MGIMWA, ...
- NDEJEMBI ASEMA SERIKALI MBILI NDIYO NGUZO PEKEE IM...
- SAKATA LA ZITTO KABWE NA UONGOZI WA CHADEMA LEO MA...
- JK: SIYO DHAMBI KUTOFAUTIANA NA MAPENDEKEZO YA TUM...
- RAIS KIKWETE NA MAKAMU WAKE WAONGOZA KUAGA MWILI W...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBO...
- MANGULA AZIDI KUWAWAKIA WANA-CCM WANAOJINADI KABLA...
- DC KANGOYE AWAFUNDA VIJANA KULETA MAGEUZI MAKUBWA ...
- ZITTO AMBWAGA TUNDULISU MAHAKAMA KUU, NI KATIKA OM...
- MWILI WA DK. MGIMWA KUWASILI DAR ES SALAAM, KESHOK...
- VIDEO YA SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI Y...
- WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA, RAIS...
-
▼
January
(81)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.