DAR ES SALAAM,
Zaidi ya wanachama 200 kutoka vyama vya upinzani kikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, katika Tawi la Kigogo Freshi Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam, wamevihama vyama vyao na kujiunga Chama Cha Mapinduzi-CCM.
Wanachama hao wamejiunga na CCM katika mkutano mkubwa wa hadhara ulioratibiwa na Chama Cha Mapinduzi, Tawi la Kigogo Freshi, Kata ya Pugu na kufanyika kwenye Uwanja wa Mpira Kigogo Freshi.
Katika mkutano huo wa hadhara, wanachama hao wapya ambao wengine wametoka CUF, wamekabidhiwa Kadi zao za CCM na Katibu wa CCM Kata ya Pugu SAID MGESA, kwa niaba ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa-NEC, kupitia Wilaya ya Ilala, RAMISH PATERI.
Mmoja kati ya wanachama wa Chadema aliyejiunga na CCM ni FIKIRI NYAMBIZA, ambaye amesema sababu kubwa zilizomfanya kukihama Chama chake na kujiunga na CCM, ni Chuki, Uroho wa Madaraka pamoja na misingi ya Ukabila inayoendelea kufanywa na viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema. SOURCE: UHURU FM