Google PlusRSS FeedEmail

IKULU YAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE BORA, YAPOKEA MAKOMBE YA SHIMIWI NA KUPONGEZA WANAMICHEZO WAKE

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimpa zawadi Bw. Miraji Ahmed Saleh kwa kuibua mfanyakazi bora na pia mfanyakazi hodari wa  Ofisi ya Rais Ikulu. Bw Saleh ni  Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika 
Idara ya Huduma  za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kuwazawadia iliyofanyika  Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya 
maka huu mjini Dodoma katika  hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika  Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwaka huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara  56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal,  Kuvuta kamba wanawake na wanaume  na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake)  na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Ikulu  katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika  Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam


This entry was posted in

Leave a Reply