MBEYA, TANZANIA.
KATIBU wa CHADEMA, wilaya ya Mbeya vijijini, James Mpalaza, amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya sh.73,000.
Habari ambazo Daily Nkoromo Blog imezipata, kutoka Mbeya zimesema, Mpalaza ambaye pia ni Katibu wa Baraza la kata ya Nsalala anatuhumiwa kutenda kosa hilo la kupokea rushwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata hiyo, Lookred Ndile, kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Baraza hilo aliyetajwa kwa jina la Mama Rajabu.
Akithibitisha kukamatwa kwa Katibu huyo wa CHADEMA wilaya, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya, Daniel Mtuka, alisema mtuhumiwa huyo alinaswa na maofisa wa Idara hiyo leo saa 6:00 mchana.
Mtuka alisema kigogo huyo wa CHADEMA, alikamatwa katika ukumbi unaotumika kushauri na kutoa hukumu za kesi zinazofikishwa kwenye Baraza la Kata ya Nsalala, iliyopo wilaya ya Mbeya vijijini.
Kwa mujibu wa Mtuka, TAKUKURU walipokea taarifa kutoka kwa Ndile kuwa viongozi hao wawili wamemuomba rushwa ya shilingi 73,000 ili waweze kumpa nakara ya kesi yake aliyokuwa ameshindwa pamoja na muenendo mzima wa kesi hiyo.
Akifafanua zaidi, Mtuka alisema Ndile alikuwa ameshtakiwa na Monica Degule wakigombania mpaka uliopo kati ya nyumba zao na shauri hil lililopsikilizwa katika Baraza hilo la kata Monica alishinda.
"Baada ya hukumu kutolewa Ndile hakuridhika nayo na hivyo kuandika barua ya kuomba hukumu na muenendo wa kesi ili aweze kwenda ngazi za juu zaidi ambapo alitakiwa kulipa gharama ya shilingi 10,000.
Mtuka aliongeza lakini alipoenda na kiasi hicho ambacho ndiyo kinatakiwa kisheria, watuhumiwa hao wawili walimueleza Ndile kuwa anatakiwa kupeleka shilingi 73,000 ili apatiwe vitu hivyo alivyokuwa anavihitaji.
Alisema ndipo Ndile alipoenda kutoa taarifa TAKUKURU ambapo alipewa kiasi hicho cha fedha na maofisa wa Idara hiyo waliweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili akiwemo Katibu wa CHADEMA wilaya ya Mbeya vijijini.
Naye Ndile akizungumza na Uhuru alisema alihukumiwa kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja, kulipa gharama za Baraza na akishindwa kutekeleza hayo atatakiwa kufyatua matofali 1000 na pia kumlipa Monica gharama zote alizotumia katika kesi hiyo.
"Nilipewa muda wa siku 40 kukata rufani ya kesi yangu na hivyo nikalazimika kuandika barua ya kuomba nakara ya hukumu na mwenendo mzima wa kesi, ambapo awali nilitakiwa kulipia sh.10,000 lakini nilipoenda na kiasi hicho niligeuziwa kibao na kutakiwa kulipa sh.73,000 ndipo nikaenda kutoa taarifa TAKUKURU" alisema Ndile.
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
-
▼
2012
(476)
-
▼
December
(50)
- HOTUBA YA MWAKA MPYA YA RAIS JAKAYA KIKWETE
- RAIS KIKWETE APONGEZWA KWA MAFANIKIO YA SENSA YA W...
- RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI PADRI AMBRO...
- RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIY...
- MKUTANO WA EWURA NA JUKWAA LA WAHARIRI WAFANYIKA DAR
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZULU KABURI LA HAYATI I...
- CCM: 2013 KUWA MWAKA WA KUCHAPAKAZI TU
- RAIS KIKWETE APONGEZWA NA WASANII WAKONGWE KWA KUW...
- MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHALIB BILAL,ASAINI K...
- RAIS KIKWETE AKABIDHIWA HATI YA BIMA YAKE YA MAISH...
- RAIS KIKWETE AKUTANA NA MMILIKI NA VIONGOZI WA KLA...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MRA...
- RAIS ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA TABOR...
- RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA UGANDA, AKUTANA N...
- HATIMAYE ‘AROBAINI’ YA CHADEMA YATIMIA
- Top National Parks in Africa
- WORLD BANK PRESS RELEASE WIND EAST AFRICA SINGIDA ...
- WATALII WA NDANI WAKITALII NCHI YAO
- IKULU YAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE BORA, YAPOKEA MAK...
- KUTANA NA NUSRA MAGULUKO (28) MWANAMKE JASIRI ANAY...
- ...
- DKT. BILAL AHIMIZA MAELEWANO BAINA YA WAFUASI WA D...
- RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUN...
- VIJANA JAZZ YAIBUKA UPYA, YAMSHUKURU RAIS KIKWETE ...
- SAFARI YA LAKE LAND KUHAMASISHA UTALII KUANZA KESHO
- MHADHIRI OUT AKABIDHI KWA KINANA VITABU VYA KITAAL...
- RAIS WA ZANZIBAR DR ALI M. SHEIN AKUTANA NA UONGOZ...
- KUFUATIA KAULI ZA MAALIM SEIF; CCM ZANZIBAR YATOA ...
- RAIS KIKWETE APOKEA MAJENGO MAPYA MATATU YA HUDUMA...
- KINANA NA SEKRETARIETI YAKE WAKUTANA NA MAKATIBU W...
- MATUKIO MBALI MBALI YA SHEREHE ZA MIAKA 51 YA UHURU
- SIKU 14 ZA KUIONA TANZANIA, MTANZANIA TEMBELEA TAN...
- MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA JENGO JIPYA LA O...
- PRESIDENT KIKWETE HOSTS DINNER FOR GAVI FORUM MEET...
- MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA WATANZANIA 3 K...
- RAIS AZINDUA DAHARIA ZA SHULE YA WASICHANA YA NACH...
- MWENYEKITI WA CCM, NDUGU JAKAYA KIKWETE AKABIDHI K...
- KINANA ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU MSAIDI...
- KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MBARONI...
- NAPE AMPONGEZA DK. SLAA KWA KUKIRI KUWA NA KADI YA...
- MUHAMED SEIF KHATIB AKABIDHIWA RASMI OFISI, LUMUMBA
- WAPINZANI WAANZA KUPAGAWA.....
- MAKALA MAALUM
- ZIARA YA JK NACHINGWEA
- NAPE: VIGOGO CHADEMA WANA KADI ZA CCM
- NDUGU, RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MAHAKAMA YA...
- NAPE AFAFANUA "MKAKATI WA KUHUISHA CHAMA" STAR TV.
- MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) WILAYA YA...
- MAAZIDHISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, MKOANI LINDI
-
▼
December
(50)
LOVE LINKS
Powered by Blogger.