Google PlusRSS FeedEmail

WAPINZANI WAANZA KUPAGAWA.....

Baada ya kuumbuliwa na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye kuwa vigogo wa  Chadema  wana kadi za CCM na bado wanazilipia, Dk.Slaa amekiri kuwa na kadi ya CCM na anaitunza na kuienzi kadi hiyo katika makumbusho yake kwa ajili ya historia ya wajukuu wake kwa kuwa ni mali yake.
....JE WALE WANAORUDISHA KADI KWENYE MIKUTANO YAO HAWAHITAJI KUMBUKUMBU?
Navyoelewa mie kitu kizuri ndio kinawekwa kwa ajili ya kumbukumbu nina amini Dk.Slaa ameweka kumbukumbu kwa wajukuu zake kuonyesha uzuri na ubora wa chama bora Tanzania.

 Wakati huo huo Viongozi wa CHADEMA NA CUF warejea CCM.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Morogoro,Rajab Ally,Katibu wa chama hicho mkoa wa Morogoro,Abel Ruanda na Mwenyekiti wa CUF kata ya Mkundi,Said Athumani wamejiunga na CCM.
 Viongozi hao, ambao wameeleza kuchoshwa na siasa chafu na kukosekana dira katika kuwatumikia Watanzania,wamejiunga na CCM juzi na kukabidhiwa kadi katika uwanja wa Mashujaa mjini hapa.
Viongozi hao walisema "Ndani ya upinzani tuliingia kwa bahati mbaya,ni kama vile uko barabarani unasubiri gari na linatokea unapanda lakini ukishakuwa ndani na kugundua ni mkweche inabidi ushuke usubiri lingine.Tumeshuka na tumepanda gari la ukweli CCM"

This entry was posted in

3 Responses so far.

  1. ANATAKIWA AJIHUDHURU. TUNATAKIWA KUPIMA NI KWA KIASI GANI WANAWEZA KUTEKELEZA MAMBO MAGUMU KAMA HAYO YA KUMFANYA AJIHUDHURU KWANI WALIWEZA KUWAFUKUZA MADIWANI HUKO ARUSHA JE VIPI NA HUYO, ASIYELIPA KODI, PIA ANAKADI YA CHAMA TAWALA .SWALI NI JE WAKATI AKIPOKEA KADI ZA WATU WANAORUDISHA KADI YEYE YA KWAKE JE? KO AJIHUDHURU AKA. AVUE GWANDA

  2. ANATAKIWA ATURUDISHIE KADI YETU ANATIA GUNDU. PIA KAMA WAO NI CHAMA MAKINI AJIHUDHURU. TUONE KWA VIPI WANAWEZA KUSHUGHULIKIA MAMBO MAGUMU KAMA HAYO. SASA KAMA WANASHINDWA KUMHUKUMU MTU ALIYEKIRI MAKOSA. UKO WAPI UZALENDO. WATAWEZA KUSHUGHULIKIA NINI HUYO NDIE ANAWAUZAGA WANACHADEMA MNATAKIA MMTOE

Leave a Reply