Google PlusRSS FeedEmail
  • AFANYA KIKAO NA WANANCHI
  • AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
 Ndugu Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa North Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina ya wawekezaji na Wanavijiji.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
 Mkurugenzi wa Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi,Magereza,Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio akihutubia wananchi wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao dhidi ya Jeshi la Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki zitapatina.
 Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo wilayani Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo.

NAPE ATIMIZA AHADI NYAMONGO

AFANYA KIKAO NA WANANCHI AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum ch... [Read More]

Rais Jakaya Kikwete akiongea na baadhi ya watanzania waliojitokeza kumuaga jana jioni katika hotel ya Churchill London. Rais Kikwete alikuwa anarejea nyumbani Tanzania mara baada ya kumaliza mkutano wake wa OGP (Open Government Partnership) uliofanyika London nchini Uingereza. Pembeni yake kulia ni Bi Mariam Mungula, Kaitbu wa CCM UK.
Mwenyekiti wa CCM UK Ndugu Maina Owino akiongea jambo na Rais Kikwete
Rais Kikwete akijibu swali la Ndugu Maina Owino 

Rais Kikwete akielekea kusalimiana na watanzania waliojitokeza kumuaga jana jioni
Mwenyekiti wa CCM UK akisalimiana na Rais Kikwete na kumshukuru kwa muda wake aliojitoela kuongea na baadhi ya watanzania waliojitokeza jioni ya jana kumuaga.

Said Surur aksalimiana na Rais Kiwete pembeni yake ni Ndugu Ahmed Dibibi, Hussein Kova na Gonex
Ndugu Kapinga na Mohamed Upete wakisalimiana nakuagana na Rais Kikwete
Hussein Kova na Gonex wakisalimiana na kuagana na Rais Kikwete
Rais Kikwete akisalimana na Diaspora blogger Jestina George Meru
Rahma Lupatu akiwa katika pose na Rais Kikwete mud mchacehe kabla hajaondoka 
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waliojitokeza kumuaga jana jioni katika hotel ya Churchill London.
Baada ya kuagana na Rais Kikwete wadau waliojitokeza kumuaga walipata fursa ya kupiga picha na kubadilishana mawazo na Waziri wa Sheira na Katiba Mhe. Mathias Chikawe (watano kushoto).
Waziri wa Sheira na Katiba Mhe. Mathias Chikawe akiwa katika picha ya pamoja wa watanzania waishio UK kutoka kushoto ni hussein Kove, Mariam Mungula, Mhe. Waziri, Kapinga Kangoma na Mohamed Upete.


Mhe. waziri Chikawe akibadilishana mawazo na wadau
Jestina George, GONEX & Hussein 
Moi & Hussein
Hussein, Said Sururu & Gonex
Moi & Fred Maro (mpiga picha wa Ikulu)
Mariam Mungula, Rahma Lupatu, Mhe. Chikawe & Mrs. Meru
Mhe. Chikawe katika picha ya pamoja ya Ahmed 
Mhe. Chikawe akibadilishana mawazo na Mariam & Ahmed
Mazungumzo yakiendelea
Mariam & Ahmed wakibadilishana mawazo
Nayla, Munira, JwaD, Mariam, Rahma & Ahmed
Picha na Jestina George

WATANZANIA UINGEREZA WALIVYOMUAGA KWA WINGI RAIS JAKAYA KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete akiongea na baadhi ya watanzania waliojitokeza kumuaga jana jioni katika hotel ya Churchill London. Rais Kikwete alikuwa... [Read More]

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO MJINI LONDON

Video: Ikulu Mawasiliano [Read More]


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akifungua semina ya siku 2 iliyoshirikisha Chama Cha Mapinduzi na Chama rafiki cha Kikomunisti cha China  CPC,katika hoteli ya Courtyard mjini Dar es Salaam, Semina hiyo ilikuwa mahususi katika Kuvijengea Vyama Uwezo  na Umuhimu wa Vijana katika vyama.

 Naibu Mkurugenzi wa CPC katika masuala ya Kimataifa Ndugu An Yuejun akitoa salaam za shukran kwa niaba ya wajumbe wenzake kabla ya kuanza kwa semina ya siku mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.

 Profesa Song Li akitoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kiuchumi ikiwa mipango iliyofanywa na CPC tangu kuanza kwake katika kuboresha na kukuza uchumi wa China.
 Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu Anamringi Macha akibadilishana mawazo na Makamu Mkurugenzi katika masuala ya Kimataifa wa CPC Ndugu An Yuejun mara baada ya kumaliza semina kwa siku ya kwanza.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (Zanzibar) Salama Aboud na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Bara wakifurahia jambo na Naibu Mkurugenzi wa masuala ya kimataifa wa CPC Ndugu An Yuenjun.
 Katibu wa Mkoa wa Vyuo Vikuu CCM Ndugu Christopher Ngubiagai akitoa mada juu umuhimu wa vijana katika CCM na matatizo yanayowakabili vijana wengi wa Tanzania na kusini mwa jangwa la Sahara katika semina ya siku mbii iliyoanza tarehe 31 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 1 Novemba katika hotel ya Courtyard jijini Dar es Salaam na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.

 Suleiman Mwenda kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi akielezea namna internet inavyofanya kazi katika kufikisha ujumbe hasa kwa vijana na pia hatua ambazo serikali inazichukua katika kuboresha na kuzuia upotoshaji ama matumizi mabaya ya internet.
 Gift Msuya kutoka Mkoa wa Vyuo Vikuu akifafanua masula mbali mbali yanayohsu mkoa huo wa vyuo vikuu wakati wa semina ilyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Ramadhani Madabida akitoa mada juu ya mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi katika semina ya siku mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
 Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi akiuliza swali linalohusu ubora wa bidhaa kutoka China wakati wa semina ya siku mbili iliyohushisha CCM na CPC kutoka China.
 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mboni Mhita akielezea umuhimu wa Umoja wa Vijana wa CCM katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Hotel ya Courtyard na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka Chama rafiki cha Kikomunist cha China pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Abdilah Mihewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge.


CCM NA CPC WAPEANA SOMO DAR

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akifungua semina ya siku 2 iliyoshirikisha Chama Cha Mapinduzi na Chama ra... [Read More]