Google PlusRSS FeedEmail

NAPE ATIMIZA AHADI NYAMONGO

  • AFANYA KIKAO NA WANANCHI
  • AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
 Ndugu Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa North Mara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina ya wawekezaji na Wanavijiji.
 Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
 Mkurugenzi wa Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi,Magereza,Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio akihutubia wananchi wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao dhidi ya Jeshi la Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki zitapatina.
 Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo wilayani Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo.

This entry was posted in

Leave a Reply