Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake (katikati) wakiwa wamezungukwa na umati wa wananchi, Kinana alipokuwa akizindua Shina la Wakereketwa Wajasirimali wa Kikundi cha Amani na Maendeleo cha waendesha bodaboda, Katika Kata ya Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi nyumba ya mwalimu katika shule ya sekondari Kaya ya Ikuti, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.Wananchi katika Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Hayupo Pichani) huku wengine wakiwa juu ya miti ili kumuona kiongozi huyo wa CCM, katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Nov 27, 2013, katika kata hiyo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi wa Kata ya Masoko, Rungwe, mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akifurahia jambo na Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano uliofanyika katika jimbo hilo, Kata ya Masoko, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akimkumbatia kwa furaha Mbunge wa Rungwe Magharibi, Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano uliofanyika katika jimbo hilo, Kata ya Masoko,wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013
Wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika soko la Kata ya Ikuti, katika kijiji cha Butonga, wilayani, Rungwe, wakiwa wameacha biashara zao na kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana ili kumweleza kero zao, alipokuwa akipita eneo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua utelezaji ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujaliana nao njia bora ya kuzitatua, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipewa zawadi na Jane James, Mke wa Mjumbe wa Shina namba 2, Butonga, Kata ya Ikuti, Rungwe, James Mbasi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa mjumbe huyo, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza kijana Asimwise mwantebele baada ya kijana huyo kutangaza kuhamia CCM akitokea Chadema, wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizindua shina la wakereketwa wa CCM la Kiwira, wilayani Rungwe, Nov 27, 2013.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akikabidhi mchango wake wa sh. laki moja (100,000) kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbozo Godfrey Zambi, kwa ajili ya kusaidia harakati za maendeleo ya kiuchumi kwa shina la wakereketwa wajasirimali waendesha bodaboda, wa CCM, katika Kata ya Kiwira, wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimhoji jukwaani, Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Crispian Meela (kushoto) ni kwa kiwango gani amesimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, wilayani kwake, wakati wa mkutano wa hadhara kata ya Ikuti, wilayani humo, mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na kinamama wauza ndizi wa Iponjola, wilayani Rungwe mkoaoni Mbeya, Nov 27, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtambulisha Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, kwa kinamama hao wa Iponjola,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtambulisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa kinamama hao wauza ndizi wa Iponjola, wilayani Rungwe mkoaoni Mbeya, Nov 27, 2013.