Google PlusRSS FeedEmail

KINANA NA UJUMBE WAKE WATINGA NAMTUMBO KIAINA, WAPATA CHAI YA ASUBUHI KWA MJUMBE WA SHINA, WANANCHI KWA MAELFU WAFURIKA MIKUTANONI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika, Nov 17, 2013,  kwenye Uwanja wa Taifa, wa mjini Namtumbo mkoani Ruvuma.

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika, Nov 17, 2013,  kwenye Uwanja wa Taifa, wa mjini Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika, Nov 17, 2013,  kwenye Uwanja wa Taifa, wa mjini Namtumbo mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa mgolole wa kabila la Wayao na mzee wa kabila hilo, kabla ya kuhutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika, Nov 17, 2013,  kwenye Uwanja wa Taifa, wa mjini Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na msafara wake, wakinywa chai nyumbani kwa Mjumbe wa shina namba sita, Saidi Hussein (kulia), katika kijiji cha Mchomora, Nov 17, 2013, alipokwenda kwa balozi huyo wa CCM, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kuzitatua, katika wilyana ya Namtumbo mkoani Tuvuma. Wengine kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mjumbe wa shina namba sita, Said Hussein, wakati Kinana alipofika nyumbani kwa mjumbe huyo na kuzungumza naye pamoja na wananchi wanaoishi kayika himaya ya nyumba kumi za mjumbe huyo
Kinana akipiga stori na mjumbe huyo wa shina, Huku Dk. Asha-Rose Migiro naye akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Namtumbo,  Benjamin Nindi (kushoto).
 Mjumbe huyo wa shina namba sita akimpatia Kinana zawadi ya ndizi baada ya kuvutiwa naye. watatu kushoto ni Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa akishuhudia
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambao unayanyika kutokana na ahadi ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
 Kinana na Vita Kawawa wakipita kwenye msingi wa  ujenzi wa hopitali hiyo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdul Rahman Kinana akiwa amezamia katika mtaro kushiriki ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo. Kulia walioko juu ni Katibu wa NEC, Siaa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye naye alishiriki kikamilifu kwenye ujenzi huo.
 Kinana akikafua sehemu ya majengo ya hospitali hiyo ambayo yamekamilika ujenzi wake
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake wakipata maelezo kuhusu mradi wa umeme kwa ajili ya wananchi wakiwemo wa vijijini katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo hicho cha umeme
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizindua Ofisi ya CCM Kata ya Namtumbo
 Katibu Mkuun wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shina la wajasiriamali la Vijana waendesha bodaboda mjini Namtumbo
Mji wa Namtumbo unavyong'aa kwa barabara nzuri za lami: Imetayarishwa na theNkoromo Blog

This entry was posted in

Leave a Reply